econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 25,522
- 40,795
Jina la Kanali Alexis Kanyarwenge sio maarufu Sana Kwa Sasa kwenye siasa za Maziwa Makuu au Afrika Mashariki, ila ndio chimbuko la mabadiliko yaliyopo Rwanda kwa Sasa.
Kanali Alexis Kanyarwenge alikuwa muhutu katika jeshi la Rwanda kipindi Cha utawala wa Rais Habrarimana. Rais Habrarimana alituhumiwa kwa kukaa kimya kuhusu mauaji ya watutsi nchini Rwanda. Makundi mbalimbali ya watutsi yalijitahidi kupambana na Habrarimana kutokea nje ya Rwanda yakashindwa.
Mwaka 1980 jambo la ajabu likatokea. Mhutu Alexis Kanyarwenge akaongoza jaribio la kumpindua Generali Habrarimana ila ikashindikana, na Kanali Kanyarwenge akafanikiwa kukimbilia Tanzania. Kitendo Cha Kanyarwenge kutaka kumpindua Habrarimana Mhutu mwenzake kiliwasukuma RPF kumuomba ajiunge nao mnamo mwaka 1990 na kumchagua kuwa Makamu wa Rais wa RPF, Rais wa RPF wakati huo akiwa Fred Rwigyema. Baada Fred Rwigyema kufariki , Mhutu Alexis Kanyarwenge akachaguliwa kuwa Rais wa RPF aliongoza jeshi la RPA lililokuwa limesheheni wapiganaji wa Kitutsi wakiongozwa na Generali Paul Kagame.
Uongozi wa Alexis Kanyarwenge ndio ilifanya kazi ya kufikia makubaliano ya Arusha mwaka 1992 na pia Chini ya uongozi wake kama Rais wa RPF ndipo RPF ulifanikiwa kusimamisha mauaji ya kimbali huko Rwanda na pia kuipindua serikali ya Rwanda mwaka 1994.
Hivyo basi, Tanzania ya sasa inamuhitaji Kanali Kanyarwenge wake. kwa Sasa, Tanzania inahitaji mwanajeshi au jeshi ndani ya mfumo atakaye weka Taifa mbele na sio chama, udini au ukabila na kusimamia upande wa haki. Kanali Kanyarwenge alikuwa Muhutu na Kanali wa jeshi aliyemsaidia Habrarimana kuingia madarakani mwaka 1973, ila alipoona Habrarimana amekengeuka alikubali kusimama upande wa watutsi kama kiongozi mkuu wa mapambano kama Rais wa RPF na kweli akafanikisha azma hiyo na Leo Rwanda watu wanakula matunda ya jasho lake ikiwa yeye yupo kaburini amepumzika.
Nani ndani ndani ya vyombo vya ulinzi atajitoa kupinga state capture iliyopo hata kama yeye ni sehemu ya jeshi?. Wengi waliopo kwenye mapambano wanaishia kwenye kuongea ila hawana Kanali wa jeshi wa kuwasaidia.
By economist
Kigali, Rwanda