lukubuzo Samsis
JF-Expert Member
- Nov 3, 2014
- 2,947
- 3,466
Pumba,Majungu na umbea.Tangu nipo shule ya msingi tulikua tunaaminishwa kwamba Mlm Nyerere ndio "icon" pekee apa nchini, tulikua tunaimba nyimbo nyingi ni za kumsifu, lakini hatukuwahi kuambiwa kua kuna watu wengine ambao bila wao mwalimu "asingetoboa" na pengine tusingemjua kabisa mwalimu nyerere, au story yake ingekua "short lived". Mmoja wa hao watu ni OSCAR KAMBONA.
Nimezaliwa hapa Tanzania miaka ya 90 mpaka nimekua mtu mzima kila kitu ni Nyerere tu. Kambona nilimsikia badae sana baada ya kuskia kisa cha huyu mtu nikawa interested sana kufuatilia stories zake.
kwa mujibu wa maandiko Kambona alikua bega kwa bega na mwalimu ktk kudai uhuru yaani ilikua akitoka mwalimu anaefuata ni Kambona lakini huwezi sikia hichi kitu kinasemwa waziwazi na pengine bila mawazo na support ya kambona mwalimu "angefeli vibaya mno". Kambona ndio mtu aliezima mapinduzi yalioilenga serikali ya nyerere kutoka kwa askari waliotaka kuasi, yaani kwa ufupi ni kwamba Nyerere asinge endelea kua mtawala wa nchi hii kama sio Kambona.
Kambona aliona mbali kuliko mwalimu Tanzania ya sasa ndio aliyoiona kambona lakini mwalimu alipinga, Kambona aliona ubepari ndio utafanya kazi lakini mwalimu aliona ujamaa ndio unafaa, mwalimu "failed miserably" akatupeleka chaka mpaka leo we still pay for his "grave mistake". Mwalimu alikua mbishi na aliamini kwamba yeye ndio ana maono bora kuliko wengine ,chochote kile ambacho kilikua hakiendani na sera zake alikipinga hata kama kilikua "viable". Fikiria mtu mmoja tu kaenda urusi akafurahishwa na mfumo wa ujamaa akaja kuufanyia "experiment" hapa nchini na ukafeli kwasababu alikataa kusikiliza maoni ya watu wengine, kwa wakati huo mwalimu ndio alikua "kila kitu"
Kambona akatofautiana na mwalimu , yeye alitaka ubepari mwalimu alitaka ujamaa. Kutokana na ushawishi mwalimu alishinda japo kambona ndie aliekua sahihi lakini hawakumskiliza. Baadae mwalimu alijua amekosea akaturudisha kwenye Ubepari na bado akaonekana ni "hero" . Kitu ambacho oscar alikiona miaka kadhaa kabla wakati huo mwalimu alikua "blind" almost everyone was blind except the very few including Kambona
Haya leo 2021 TZ hii ya leo ndio kambona aliyoiona na tumechelewa sana, kwa mtazamo wangu bado tupo nyuma kwa miaka 15 kutokana na sera mbovu za mwalimu nyerere
Wote ni marehemu wapumzike kwa amani lakini, mwisho wa siku Oscar Kambona ndio AMESHINDA!!!!! Kwangu mimi shujaa wa kweli nchi hii ni OSCAR KAMBONA na sio mwalimu! Na ndio mtu muhimu sana sawa na mwalimu lakini ndio aliesahaulikia kuliko wote nchi hii, natamani watanzania wengi tuliozaliwa miaka ya 90 wajue habari za huyu shujaaa
Aliyeweka Nyerere day kama public holiday alitumia vigezo gani ilihali si kweli kwamba Nyerere ndie mtu pekee aliepigania uhuru wa nchi hii
Ukiniambia nichague kati ya Nyerere na Kambona itakua ni Kambona always
"Oscar Kambona was one of the best presidents Tanzania never had"
Oscar Kambona - Wikipedia
Pumba,Majungu na umbea.
Kwani yeye si alikuwa ni rais? Alituacha wapi?Acha uvivu, uzembe na upumbavu. Tangu Nyerere aache urais ni muda mrefu sana na tungekuwa tuna uongozi mzuri nchi unayoitamani wewe ingeshatengenezwa. Nyerere ni mmoja ya viongozi wazuri sana kutokea. Nchi gani za Afrika zilikuwa na viongozi wazuri enzi za Nyerere ambazo unaweza kutoa kama mfano leo? Mimi naona nchi nyingi zina changamoto kuliko Tanzania mara kumi.
Kila mrengo unafaida na hasara zake, Mwalimu kwa Sera ya ujamaa angalau Ardhi, elimu na afya tunafaidi japo kadri miaka inavyosonga Elimu inakuwa ghali kuipata ile nzuri, Ubepari nao unamabaya yake waone Kenya na Zambia baada ya Rais Kaunda ndo utajua kwanini kila Sera inamabaya na mazuri yake
ujamaa kwa kipinde kile ilikuwa njia sahihi ya kuwaweka pamoja maana watu wengi walikuwa hawana elimu, wanaishi maisha duni sana, wanakaa mbali kutoka nyumba moja hadi nyiungine hata kupeleka huduma za kijamii ilikuwa shida sana, barabara mbovu kama tungeendelea na ubepari bas wananchi wangeendelea kuwa watumwa zaidi. ujamaa uliwaletea heshima zaidi baada ya kuanzisha vijiji vya ujamaa na kujenga umoja na kukuza lugha ya taifa na utaifa.
ujamaa ndio ulisaidia sana kujenga utaifa na kuachana na ubaguzi....ukabila uliondoka sabaabu ya ujamaa watu waliweza kujiona wao ni watanzania, utani wa jadi ukaanza.
nchi nyingi zilizoenda kwenye ubepari hasa Africa zina matatizo mengi ukichunguza.
mtoa maada nakushauri usome vizuri ama ongea na wazee walioishi kipindi hicho maana umesema ulizaliwa kipindi cha 90s. bado una mengi ya kujifunza kuhusu historia ya tanzania.
ni kweli walikjuwepo watu wengi walioshiriki kuleta Uhuru wa nchi japo hawakuwa na Elimu na hostoria imewaacha sana.
Ndio maana mkuu amesema watu wafundishwe historia ya nchi yao... hata ww umepata historia ya kambona kwa kuokoteza tu hujui mambo kwa undani wake. usingefanya hitimisho kwenye andiko lako ili watu wawe huru kujadili na ww kupata mwanga.
Mwenye Heri alikuwa na matusi lohWaliishia kumpaka matope.
View attachment 1665493
unaingizaje ubapari kwenye utawala wa machifu? machifu walikuwa watu wenye nguvu ujamaa uliweza kuvunja nguvu zao na kutufanya kuwa wamoja. ndani ya ubepari tusingekuwa wamoja kama hivi leo, utawala wa machifu ndio chimbuko la ukabila na ukanda kila mmoja ana linda mila na tamaduni zake, kwa kipindi kile ujamaa ulikuwa na faida,,, kila kitu huwa kuna sehemu ya kuanzia. inawezeka ilitakiwa tuanzie ujamaa then twende kwenye ubepari ambao tayari watu wana elimu, tungeingia kwenye ubepari na watu hawana elimu tungepata taifa la watu wajinga sana, ubepari haukusomeishei watoto wako kama huna hela unabakia kuwa mjinga. tukumbuke ubepari ni unyonyaji kwa lugha nyingine. ukilinganisha ubepari wa marekani na Tanzania haviendani hata historia ya watu wao ni tofauti sana.Kwa mantiki hiyo mkuu unataka kusema kuwa Serikali inayofuata Ubepari haujali raia wake? Kama ndio, vipi kuhusu Marekani ambao wanalinda raia wao hata kama ni mmoja yupo mahali akapata tatizo.
Watanzania kuwa wamoja haijaletwa na itikadi ya kisiasa, hii hali ya Umoja kuna watu wametoa damu zao kwa sisi kuwa wamoja sio siasa ya jukwaani au kitabuni inayoitwa Ujamaa.
Ujamaa una mazuri na mapungufu yake ila haimaanishi kuwa Ubepari usingefaa au kutufanya wamoja ndani ya hii nchi.
Kuchukua Kenya kama mfano wa madhara ya Ubepari ni kujielekeza vibaya kwanza turudi nyuma tuangalie historia ya Kenya ilivyo;
Kenya walikuwa na Ubaguzi hata kabla ya Uhuru, Mau Mau walikuwa wanapigania ardhi ya kabila lao wakikuyu baadae wakataka sasa uhuru wa Kenya waitawale
Tanzania ukiangali vita vyaMaji Maji vilipiganwa na makabila zaidi ya moja ya huko kusini ili kumtoa mkoloni hii inaonesha wazi watanganyika baadae watanzania walikuwa na umoja hata kabla ya uhuru.
Hii morali ya kuungana ili kupambana ingeweza kuendelezwa na System hata ndani ya Ubepari.
Kuizidi Tanzania ndio kufanikiwa, hivi Ushacheck GDP ya Ethiopia ?kenya.
ukiondoa tofauti zao za kikabila, ulishawahi kujiuliza kwanini kenya inaiacha mbali sana tz kwenye gdp?.
View attachment 1665986View attachment 1665987
Nani aliesema hatuulizani makabila wala dini????Kupanga ni kuchagua! Wengi wa wale walioanza na ideology ya Ubepari wakati nchi zao bado ni changa wameishia kupata matabaka either ya kikanda au kikabila! Inawezekana ukaona kuwa tumechelewa sana lkn amini kuwa misingi aliyoijenga mwalimu ndio leo tupo wamoja hivi unavyoona hatuulizani makabila wala dini. Sasa kama kujenga nchi tuanzie hapo baada ya kujenga Amani na Umoja wa Kitaifa.
Miaka ya 60 bado kiswahili ni lugha ngeni??Jamanieee mwisho wa siku Hata kiswahili chenyewe kulikuwa bado lugha ngeni, mpya na inayo evolve.
Probably hakukuwa na tafsida au misamiati mizuri kwa wakati huo. Na hayo yalikuwa maneno ya kawaida tu labda
Mpaka leo kuna makabila wanaongea Kiswahili kwa shidaaaaaa, unaongelea miaka ya 60 !!!!!!Miaka ya 60 bado kiswahili ni lugha ngeni??
You can't be serious mkuu
Sio kwa misingi mibovu sanaaaaaa ambayo tayari ilishawekwa.Kutoka 1985 mpaka leo ni miaka 35 ambayo ingetosha kabisa “kurekebisha” chochote ambacho unaona mwalimu “alikosea”…..
Wewe ni mpumbavuSio kwa misingi mibovu sanaaaaaa ambayo tayari ilishawekwa.
Miaka 35 ni kidogo mno kuondoa na kufutilia mbali (kisera) yale yote maovu ambayo yalishafanyika
Huoni Leo kila mtu ili apate political mileage lazima amtajetaje mwalimu??? Hizo ni miongoni mwa athari kuu ambazo it will still take years to eliminate