Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Na zimeshatumika shilingi bilioni nne za Kitanzania kama matayarisho ya awali.

Ni hivi wafanye marekebisho yao lakini kamwe Nyerere hawezi kutangazwa.
Hata kama mpango ulikuwepo, Nyerere amesha feli kwenye hatua za awali mchakato mzima.

MARK MY WORDS.
 
Suala la pesa lilikuwa ni stori tu baada ya tukio lenyewe la Kambona kukimbilia uhamishoni.

Maana hata huyo Kambona alikuwa anasema Nyerere alificha pesa nyingi sana nje ya nchi, jambo ambalo mpaka leo inaonekana siyo kweli.
Kwani timu ya AC MILAN inayoshiriki ligi kuu ya Italia inamilikiwa na nani?
 
Video haina sauti
 
Nimeangalia mifano ya nchi zilizoendelea We unaleta mifano ya nchi za kifisadi hizi.China ni makomunist kwenye Utawala na sio kwenye uchumi.
China ni tajir kuliko Democratic Taiwan? Taiwan wako mbele ya china kwa maendeleo
 
duuu, nani anatoa hizo hela?
Kwani kuna shughuli yoyote inayoweza kufanyika na Kanisa Katoliki bila ya pesa?

Jibu ni hakuna! Hata kwa sakramenti ya ubatizo lazima kuna chochote utachangia, sembuse hii shughuli ya kumfanya HAYATI kuwa mtakatifu!

Wanaotoa hizi pesa za kufanikisha hii shughuli ni [...].

Kisheria inakuwa sio salama kuwataja hadharani lakini ukifuatilia utagundua ni wakina nani wanaotoa hizo pesa.

Huo ni mkakati ulioratibiwa kwa umakini mkubwa sana na utachukua miaka mingi hata zaidi ya miaka ishirini [ 20 ] kuanzia sasa ili lengo tu litimie.

Na lengo litatimia kwa sababu, tayari HAYATI ameshafanyika kuwa ni MWANAHERI.
 
tuwaache wafu wawatukuze wafu wenzao
 
Suala la pesa lilikuwa ni stori tu baada ya tukio lenyewe la Kambona kukimbilia uhamishoni.

Maana hata huyo Kambona alikuwa anasema Nyerere alificha pesa nyingi sana nje ya nchi, jambo ambalo mpaka leo inaonekana siyo kweli.
Ni kweli! Kwani ni nani anayemiliki hisa za asilimia hamsini [ 50% ] kwenye kiwanda cha kutengeneza magari kilichopo India kinachoitwa TATA?
 
Ni hivi wafanye marekebisho yao lakini kamwe Nyerere hawezi kutangazwa.
Hata kama mpango ulikuwepo, Nyerere amesha feli kwenye hatua za awali mchakato mzima.

MARK MY WORDS.
Muda ndio hakimu mzuri, ukifika utaamua wenyewe lakini bado ni mapema sana kusema mchakato mzima umeshafeli.
 
Nyerere alikuwa baba wa amani. Halaf uchumi angemuachia mwingine aujenge.

Vijiji Vya ujamaa hata kama vingeanzishwa kama vilivyoanzishwa lakini uendeshaji wake na mipangilio yake ilitakiwa iwe tofauti na tulivoiona

Watu (wanavijiji) wanaakili, na maono pia.

Na Mawazo ya kuanzia na baadhi ya vijiji baadhi ya maeneo ingekuwa wazo bora - piloting? Jaribu kwa vijiji vichache na ikifanikiwa endelea kwa vijiji vingine.

Hii ingefanya hata serikali iwe na uwezo wa kupeleka huduma za kijamii za kutosha kwa hivyo vijiji Vya kuanzia navyo. Hapo uwezekano wa kufanikiwa ungeweza kuwa mkubwa. Halaf vijiji vingine vingefuata.

Hata kitu kiwe kizuri kiasi gani lakini mkikosea katika mipangilio au utekelezaji au usimamizi wake lazima mkose matokeo mazuri.

Hii kitu ni kama ilikuwa ya Nyerere peke yake. Waliofuata siwasikii wakitaka kuijaribisha kwa vijiji hata 20 tu Tanzania nzima. Binafsi siioni kama idea mbaya ni kuwa tu siamini kama sehemu zote (Tanzania nzima) inahitaji vijiji Vya aina hii. Sababu ni kuwa watu wengine wapo kwenye maeneo - vijiji walimo tangia miaka ya 1910 huko sasa hawa utawahamishaje maana wameshajijenga kwenye maeneo yao
 
Kambona alikuwa na nafasi nzuri ya kumpindua Nyerere lkn kwa bahati mbaya hakufanya hivyo.

Laiti yeye ndiye angekuwa kiongozi wetu leo hii Tanzania tungekuwa tunacheza ligi moja kiuchumi na Nigeria, SA, Egypt, Algeria na Morocco, tusingekuwa "Shithole" kama tulivyo leo.

Nyerere alikuwa na ka-tabia ka umungu mtu ka kupenda kuabudiwa ili kuonyesha kuwa bila yeye kusingekuwa na Tanzania tabia ambayo Magufuli naye ameirithi.
 
Pesa ndio kila kitu!

Kanisa linaangalia mambo mawili.

1. Ulikuwa Mtakatifu kweli n.k
2. How far have you gone for the church. Siamini kama Constantine alikuwa Mtakatifu kwa matendo lakini kitendo cha kuifanya Katoliki kuwa dini rasmi ya Roma, alitangazwa kuwa mtakatifu.
 
Kanisa linaangalia mambo mawili.
Ni kweli!
1. Ulikuwa Mtakatifu kweli n.k
Jibu ni HAPANA!
2. How far have you gone for the church.
He was only using church for political purpose and no otherwise.
Siamini kama Constantine alikuwa Mtakatifu kwa matendo lakini kitendo cha kuifanya Katoliki kuwa dini rasmi ya Roma, alitangazwa kuwa mtakatifu.
Ndio! Lakini kwa upande wa HAYATI hakuna jambo lolote ndani ya KANISA KATOLIKI alilolifanya mpaka awe MTAKATIFU, labda iwe ni SIRI ambayo haijawahi kuwekwa hadharani mbele ya jamii.
 

[emoji1666]Angalau tungeona effect yake
 
hata kambona alishauri hivo hivo, lakini mwalimu akakurupuka tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…