Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Samahani, Mkuu wangu Babati

Usinichukie, tunaelimishana kidogo.

MWALIMU alitoa mchango mkubwa sana kwa zile FRONT LINE STATES.

Queen Elizabeth na waziri wake Winston Churchil waliingia mzozoni juu ya MWALIMU, Na waziri alikinywea.
Upo sahihi mkuu, swali nchi zote Africa alisaidia yeye kupata uhuru? kama alisaidia kwa namna gani? tunampa sifa kupita kiasi, mbona Tz aliiacha masikini kupita kiasi?
 
Upo sahihi mkuu, swali nchi zote Africa alisaidia yeye kupata uhuru? kama alisaidia kwa namna gani?
Ni kwa nchi za Kusini mwa Africa.

Si kwa nchi zote.

Alisaidia kwa kutoa msaada wa kijeshi, Wapambanaji, Kujenga kambi za ukombozi kule Moro Mazimbu, DSM, na baadhi katika Mikoa ya Kusini.

Gharama za vyakula, mavazi, na malazi.

Gharama za ununuzi vifaa na zana za kivita kambini.

Gharama za kuwaandaa walimu wa mafunzo mwanzo hadi kuhitimisha wapambanaji.

Na gharama za kuwasafirisha hadi nchi mwao, n.k
 
Haya yote ulitaja wewe ungekuwa ndiyo Rais ungeshindwa kuyafanya mkuu? yeye alisaidiwa mangapi na baba ake Mbowe?
 
HAYATI MWALIMU Kupewa SIFA ni haki yake ANASTAHILI.

Ni CEO na CO-FOUNDER wa Taifa huyo.

Kila ashindaye, Ndiyo hutengeneza historia.

Ni muasisi wa TAIFA letu huyo, Hivyo sioni kama kuna ubaya kupewa HADHI yake ya uasisi.
Sifa zimezidi, Tz kaicha fukara kabisa mbona alishindwa kusaidia wananchi waondokane na hali mbaya?
 
Sifa zimezidi, Tz kaicha fukara kabisa mbona alishindwa kusaidia wananchi waondokane na hali mbaya?
Nchi kuwa MASKINI si lawama anazo STAHILI kubebeshwa yeye.

Waliopokea VIJITI badala yake ndo wa KULAUMIWA.

Wakati anatoka MADARAKANI, Ameacha MADINI yote, GESI zote na RASILIMALI zote kwa ujumla TELE zikiwa hazijachimbwa.

Waliofuata baada yake ndo WAMEIGEUZA nchi kuwa katika UKATA huu tulionao mpaka sasa.
 
Maanake aliachia mtu dhaifu, pia kwanini hakutengeneza misingi bora? mbona Marekani kila anayeachiwa anafanya vizuri?
 
mbona Marekani kila anayeachiwa anafanya vizuri?
MAREKANI wao walipiga hatua kubwa mapema sana tofauti na sisi ambao TAIFA letu lilikuwa CHANGA na ndo lilikuwa limetoka katika UKOLONI wakati huo.

Wana SERA nzuri & ELEKEZI kwa manufaa yao.

MAREKANI wao walipata uhuru wao 1776 na sisi uhuru tukaupata 1961.

Ina maana wao waliweza kuliandaa TAIFA lao mapema kuwa KAMA lilivyo LEO zaidi ya KARNE na KARNE kwa sababu wao wanatembea na ILANI zao vizuri,

Kama rais wao fulani hakutekeleza MRADI au MPANGO fulani, basi atakayefuata anaanza MRADI huo haweki ya kwake kutoka kichwani kabla ya kukamilisha ile iloishia njiani.

Huku kwetu WAPOKEA VIJITI hawatembei na ILANI za vyama vyao wakishatwaa MADARAKA, Hawakamilishi MIRADI wanayoikuta bali kila mtwaa KIJITI anakuja & lake.

Huku kwetu watwaa VIJITI hawaendi vile KATIBA inasema, WATWAA VIJITI wetu ni WACHUMIA TUMBO, Wajibu wao KUIFILISI nchi wala si KUINUSURU, Wao ni WATAWALA wala si VIONGOZI.
 
Good naona unakubaliana na mimi kuwa hakuweka misingi bora zaidi ya udikteta wake, kila mtawala anakuja na yake, kuna mataifa tumepata nayo uhuru na mengine baada ya Tanzania lakini leo yapo mbali sn na sisi hatuendelei sababu ya sera mbovu na ufisadi
 
Maanake aliachia mtu dhaifu, pia kwanini hakutengeneza misingi bora?
Alitengeneza misingi bora.
Waliofuata ndo walio ibomoa MISINGI hiyo.

Tunashindwa KUTAMBUA, Tofauti iliyopo kati ya UONGOZI na UTAWALA.

Wapokea VIJITI wetu AFRICA wengi wao ni WATAWALA na wala si VIONGOZI.

Waliomzunguka MPOKEA KIJITI baada ya HAYATI MWALIMU huenda hawakumshauri vema.

MADARAKA ni kama MCHEZO WA DRAFT ukiwa nje unaliona sana, lakini ukiingia ndani....

"Taifa pasipo mashauri huanguka; Bali kwa wingi wa MASHAURI huja wokovu".
 
Kwanini iwe ni kwetu tu haswa E.A ukitoa Kenya? misingi aliyoacha ni mibovu ikichangizwa na katiba mbovu aliyotuachia
 
I much-loved the guy, I also being interested in mwl Nyerere thoughts. I stand in there between but I do complain mwal Nyerere for not attending to buried his friend in 1997
 
Kwanini iwe ni kwetu tu haswa E.A ukitoa Kenya? misingi aliyoacha ni mibovu ikichangizwa na katiba mbovu aliyotuachia
Misingi aliyoiacha HAYATI MWALIMU haikuwa mibovu bali iliharibiwa na AWAMU YA PILI, YA TATU, YA NNE, N.K

Hivi wakati HAYATI MWALIMU yuko madarakani MAFISADI au WAHUJU UCHUMI walichekewa kama hivi LEO?

Wakati wa HAYATI MWALIMU uliona au kusikia DHAHABU au NDOVU na PEMBE zake wanabebwa kimagendo kupeleka nje kiholela holela kama leo?

Suala la KATIBA kuwa mbovu ni uzembe wa MARAIS waliofuata, Kwa maana katika kipindi cha HAYATI MWALIMU kwa miaka 24 yaani 1961-1985 Asingeweza kushughulika na KATIBA mya kwa kuwa TAIFA bado lilikuwa na changamoto nyingi za kushughulikia.

HAYATI MWALIMU hapo yuko kwenye UKOMBOZI WA MATAIFA YA KUSINI MWA AFRIKA, Kule vita vya Kagera, Hapa kutatua changamoto na mahitaji ya wananchi, Hivyo KUANDAA KATIBA mpya si suala la kumlaumu yeye bali WALIOFUATA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…