Tanzania ya "viwanda" imeishia wapi?

Je una amini ni sahihi kuongoza taifa kwa ndoto ya mtu? Kwanini tusiwe na "ndoto/plan ya taifa"?

Leo hii huyo magufuli hayupo na ndoto yake pia haipo! Je why tusiwe na ndoto ya taifa ili mtu akifa ndoto ibaki?
 
Sera ya taifa haipo Bali sera ya rais,almaarufu maono ya raisi,ndo maana hata somo la historia ya taifa limefutwa maana ilikuwa sera ya Magufuri,na hata hili la Viwanda ilikuwa sera ya Magufuri

Kwa Sasa rais Samia bado sera zake hazijawa wazi japo ameanza na kutembelea nchi majirani kwa lengo ka kukuza diplomasia na pia kuja na tozo nyingi lengo likiwa kukamua watz ili aendeshee serikali yake na watz kwa ujumla.
 
Sera ya taifa haipo Bali sera ya rais.

Na hapa ndio tatizo lilipo.

JK alituamisha kwenye kilimo alipo kuja magu akaja na wimbo wa viwanda..

Tumepoteza miaka 6 tukiimba viwanda sasa tumerudi square 1.
 
Je una amini ni sahihi kuongoza taifa kwa ndoto ya mtu? Kwanini tusiwe na "ndoto/plan ya taifa"?

Leo hii huyo magufuli hayupo na ndoto yake pia haipo! Je why tusiwe na ndoto ya taifa ili mtu akifa ndoto ibaki?
Hata kabla ya Magufuli mambo yalikuwa hayaendi vile inavyopaswa. Tuliomba sana tupate mbeba maono tukapata na kwa hakika alituonyesha njia japo kwa mkono wa chuma. Sasa hayupo tumerudi kwenye arifu A.

Misingi ya kuendesha nchi inapaswa kujengwa na kuwekewa uzio ili pale watawala wanapobadilika misingi iliyojengwa iwe endelevu... Kwa bahati mbaya hapa kwetu, hatutaki kujenga nchi zaidi sana ni kujijenga kwa mtu mmoja mmoja au kikundi katika mfumo wa kibepari.
 
Achana na Njozi za mchana za yule mgonjwa wa Mirembe!
 

Ule utapeli wa Tanzania ya viwanda uliisha toka enzi za dhalimu akiwa hai.

Cc:jingalao
 
Point kubwa sana
 
Obviously wapo,wewe haufahamu hilo?
Walikwepo wanawake ambao walitawala kwa mkono wa chuma, Bi Golda Meir wa Israel na Bandaranaike wa Sri-Lanka. Wengine waliojaribu kuwakaribia ni Indira Gandhi na Margaret Thatcher.
 
Kabla ya kujenga vipya.Vya zamani vilitokomea vipi?.Na je,tunajiaminisha vipi kwamba vikijengwa vipya havitatokomea kusikojulikana kama vya mwanzo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…