Tanzania ya viwanda ilikuwa na bado inabaki kama lengo jema la kukuza uchumi wetu kwa kupunguza imports na ikiwezekana kukuza exports.
Ili tufikie hapo, serikali (ofisi ya AG, hazina, wizara za uwekezaji na wizara ya viwanda) zingetengeneza financial instruments/soft financial leverage ili mkakati huo uwe halisi.
Bahati mbaya, waziri yule aliedai vyerehani 4 au machine za tofali ni kiwanda alikosa maono na mkakati mahsusi wa kufikia lengo.
Imagine nchi ndogo kama Sri Lanka yenye aneo la mraba 65,000 sqkm wanauza products za pamba (finished well designed cloths) kwenda soko la USA na EU.
Sri Lanka wanauza consumable tea ikiwamo Dilma moja ya brand 10 bora za chai duniani.
Mkoa wa Moro una eneo la 72,000SqKM.
Inatupa dhana Tz tunafanya kulimo cha mwaka '47 badala ya kufanya kilimo-biashara na viwanda vikiwa sehemu ya kuchakata mazao ghafi kwa kuwa na technology ya kisasa, mtiririko wa fedha utagusa sekta kibao kama fedha (banking, insurance and pension)
Logistics kwa magari kusafirisha raw products kwenda viwandani na kutokea viwandani kwenda bandarini kwa ajili ya exports.
Ni aibu Waziri wa fedha anawaza kodi na tozo badala ya kuja na mkakati mkubwa wa kukuza uchumi mkubwa.
Iko haja ya kuwa na think tank inayojenga mazingira ya private sector kukua kwa kuzalisha zaidi basics za soko la ndani, soko la SADC , soko la GCC watu walio jangwani na then soko la magharibi.
Napata tabu kusikia hata upanuzi wa bandari ya Tanga, debe ya kurejea kwenye drawing board ya Bagamoyo port husikii akili au mkakati kukuza uzalishaji ili kukuza exports.
Kinachosikika ni containers nyingi zitakuja toka China; containers zenyewe baadhi zina toothpick, leso, chupi, soft brooms, magunia ya kusindikia korosho, mifagio ya buibui hata nyama za ng'ombe na maziwa ya kusindika.
Uwepo wa mkakati wa kifedha ili kununua technology na know-how vingekuwa msingi wa Tanzania ya viwanda inayozalisha bidhaa, ajira na kukuza exports kwa kupunguza imports inakuwa halisi.
Tanzania ya viwanda ikitimia many of us will win; ikidoda kama sasa many amongst us are losing.
Ni aibu kusikia story graduates wa masters wanaendesha bajaji; haikuwa na maana kupeleka mtoto university then aishie kuendesha bajaji mtaani, sio sawa.
Weekend njema.