Tanzania ya "viwanda" imeishia wapi?

Sasa ni Tanzania ya tozo, sio viwanda tena
 
.
Changamoto moja anayoa Rais wetu wa sasa SSH ambayo pia alikuwa nayo JPM; kuna sehemu ya wasaidizi kwa level ya mawaziri au wasaidizi wa ofisi ya Rais, wanafikiri kizamani sana kwenye namna ya kufikia lengo la kujenga uchumi wa kisasa.

Hapa ofisini nnapofanya kazi kuna siku nilileta wazo mbadala ambalo linahitaji matumizi ya software za kisasa katika ufanyaji kazi lakini mpaka leo hamna anayetaka kufanyia kazi wazo.
 
Shhhhiiiiii shhhhiiiiii nyamaza ww.. Keep quite..!! [emoji210][emoji210][emoji210][emoji210][emoji210] nyonya pipi hizi utulie [emoji516][emoji517][emoji516][emoji517][emoji87]
Kama Bashe alivyo pewa unaibu waziri ili asisumbue bungeni sio?
 
Tunawaza kuongeza tozo!
 
Imeishia Chato

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Hapa ofisini nnapofanya kazi kuna siku nilileta wazo mbadala ambalo linahitaji matumizi ya software za kisasa katika ufanyaji kazi lakini mpaka leo hamna anayetaka kufanyia kazi wazo.
Taasisi nyingi za kibiashara huwa zina kitu inaitwa "enterprise mindset that is open to change for the future"
Tunaweza kujifunza kwa wakoloni baada ya kuona raw materials zimepungua Ulaya wakaja Africa, wakenda Asia na Latin America kutengeneza makoloni ili ku-tap rasilimali.
Baada ya vuguvugu la uhuru kushika kasi, wakaja na neo colonialism strategy.

Msikize Dr. Arikana akionesha dhana ya ukoloni mambo leo unavyofanywa na Ufaransa model ambayo UK, US, Germany, China nao kwa namna moja ua nyingine wanazidi kukandamiza bara la Afrika.


Pole sana kwa changamoto, ila sio kwako peke yako; Afrika kwa ujumla nchi nyingi zimekosa kuwa na futuristic thinking au kama ipo, basi imezimwa ili tubaki tukishangaa shangaa tu japo ndio namna ukoloni mambo leo unazidi kushamiri kati ya nchi ambazo ilitakiwa ziwe huru holistically.
 
Yani rais anaagiza viwanda vijengwe? Duuh!
Naam, ilikuwa amri hiyo! Na vikajengwa kweli, kwa maelfu. Kila mkuu wa mkoa alijenga viwanda. Viwe vya mabua, vya karatasi, juu yake. Na hiyo kazi ilishakamilika. Tanzania ni nchi ya viwanda sasa! Magufuli oyee!
 
Naam, ilikuwa amri hiyo! Na vikajengwa kweli, kwa maelfu. Kila mkuu wa mkoa alijenga viwanda. Viwe vya mabua, vya karatasi, juu yake. Na hiyo kazi ilishakamilika. Tanzania ni nchi ya viwanda sasa! Magufuli oyee!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
magufuli wangu nakukumbuka kwani faili lambowe LA ugaidi lakubuni ulikataa wezako wamelibeba kama lilivo na kikwete hajui

Pumzika kwa amani

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
KILIMO KWANZA ndiyo ilikuwa dira mama.Lakini ujuaji mwingi wa mwendazake ndiyo umeirudisha nyuma nchi katika kilimo ambacho ndiyo chachu ya kujengwa viwanda.
Huku Mngeta Morogoro kulikuwa na kiwanda cha KPL ambacho kililima zaidi ya ekta 50000 kipindi cha Kilimokwanza na huku kikinunua pia mpunga wa raia.
Kiwanda kilitoa ajira pia za kutosha kwa raia.
Lakini kikauwawa kipindi cha serikali ya awamu ya 5.
Kifupi ujuaji na chuki za Magu kwa mtangulizi wake zimerudisha nyuma kilimo ambacho ndiyo UTIWAMGONGO WA TAIFA.
 
Haipo yupo tu anazurura kutangaza utalii hewa ambao haupo[emoji16]
 
Njoo mkoa wa Pwani ujionee Tanzania ya viwanda inavyomeremeta.

Ukifungia na gaidi ufipa hutaelewa chochote.
Kada wa ccm ilala hamza mwanaccm kindakindaki,ccm mmepata gaidi no.1 kutokea tanzania,waulize policeccm wenu kawatwanga za kutosha
 
Kilimo kwanza hakijawahi kuwa na matokeo chanya zaidi ya magari GX V8, VX V8, tractors na power-tiller; na hapakuwa na mkakati wa masoko wa nini kinahitajika sokoni, soko lipi na soko lahitaji nini kwa ubora upi na wingi upi?

Mathalani, kama ni mpunga wakati wa kilimo kwanza, wakulima walihamasishwa ili walime mbegu gani ili soko lake liwe wapi?

nakumbuka enzi za kilimo kwanza kuna wakati wakulima walivuna mpunga wa kutosha halafu kuna jamaa wizara ya kilimo wakatoa vibali mchele toka Pakistani ukaingizwa na kuchanganywa na mchele wa ndani na wakulima wa Tanzania wakakosa soko.

Kilimo kibiasha ndio ingekuwa mpango mzima, ambapo soko la walaji wa mwisho ndilo liwe kichocheo cha nini kizalishwe shambani, kichakatwe kiwandani na kusindikwa kisha kiuzwe ikiwa ni siko la Tanzania, Comoro, EA, SADC, GCC au kwingineko.

Anyway, awamu ya 4 ishapita na awamu ya 5 ishapita; sasa ni wakati wa awamu ya 6; tujipange kwa mkakati wa kimasoko kuona tunalisongeshaje ili kuifikishia wakulima neema ya kila wanacholima kinachakatwa na kuuzwa na hiyo ndo dhana halisi ya kilimo-biashara. Tunakuwa na control ya product ya mwisho tokea mwanzo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…