Tanzania ya "viwanda" imeishia wapi?

Tanzania ya "viwanda" imeishia wapi?

Nakumbuka miaka ya mwazo ya mwendazake wimbo wa viwanda uliimbwa sana na tukaambiwa mtu ukiwa vyerehani vinne basi unakiwanda.

Wakaenda mbele zaidi na kusema kila mkoa unaviwanda zaidi ya 100 (hapa figure siikumbuki vizuri ila ilikua kubwa). Na tukaambiwa mpaka mwaka jana Tz kuna viwanda zaidi ya 8400!

Sasa najiuliza je viwanda siku hizi vimeishia wapi? Mbona wanasiasa hawaimbi tena wimbo wa viwanda?
Sasa ni Tanzania ya tozo, sio viwanda tena
 
.
Changamoto moja anayoa Rais wetu wa sasa SSH ambayo pia alikuwa nayo JPM; kuna sehemu ya wasaidizi kwa level ya mawaziri au wasaidizi wa ofisi ya Rais, wanafikiri kizamani sana kwenye namna ya kufikia lengo la kujenga uchumi wa kisasa.

Hapa ofisini nnapofanya kazi kuna siku nilileta wazo mbadala ambalo linahitaji matumizi ya software za kisasa katika ufanyaji kazi lakini mpaka leo hamna anayetaka kufanyia kazi wazo.
 
Shhhhiiiiii shhhhiiiiii nyamaza ww.. Keep quite..!! [emoji210][emoji210][emoji210][emoji210][emoji210] nyonya pipi hizi utulie [emoji516][emoji517][emoji516][emoji517][emoji87]
Kama Bashe alivyo pewa unaibu waziri ili asisumbue bungeni sio?
 
Ni bora kuchochea biashara ili kupanua tax base hata kama kuna mpango wa kukaa madatakani milele, ila kuna means za ku-support development projects bila kubinya sana mifuko wa wananchi kwa kile kodogo walicho nano;

Ila kama wanajua nini cha kufanya na hawafanyi, basi msoto upo mpaka kwa ndugu zao, maana kama ajira ni tight, basi kuna watu kibao ikiwamo wajimba, binamu, wapwa nao watasota.

Ila kama kuna neema ya kujenga uchumi jumuishi, si haba kuna wapwa nao watapata kazi private sector au public sector,

Imagine, kama private sector inakuwa kwenye sekta ya viwanda kwa mfano, lazima atoe ajira; wakati huo huo mahitaji ya ajira public sector nayo yataongezeka kwa supporting sector kama TBS, NSSF, OSHA, NEMC, TANESCO, taasisi za maji (DAWASCO, MWAUWASA et la) ili kuendana na kuhudumia mahitaji ya sekta binafsi.

Mfumo wa zamani ulilenga kupanua empire, hata sasa US na CHina wanagombana kupanua empire kibiashara. Kama serikali haina fikra za kuwa sehemu ya kuijenga sekta binafsi ili kupanua empire za kikodi kwa uzalishaji endelevu, basi tuna watu ambao hawakutakuwa kabisa kuwa kwenye nyadhifa walizonazo.
Tunawaza kuongeza tozo!
 
Nakumbuka miaka ya mwazo ya mwendazake wimbo wa viwanda uliimbwa sana na tukaambiwa mtu ukiwa vyerehani vinne basi unakiwanda.

Wakaenda mbele zaidi na kusema kila mkoa unaviwanda zaidi ya 100 (hapa figure siikumbuki vizuri ila ilikua kubwa). Na tukaambiwa mpaka mwaka jana Tz kuna viwanda zaidi ya 8400!

Sasa najiuliza je viwanda siku hizi vimeishia wapi? Mbona wanasiasa hawaimbi tena wimbo wa viwanda?
Imeishia Chato

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Hapa ofisini nnapofanya kazi kuna siku nilileta wazo mbadala ambalo linahitaji matumizi ya software za kisasa katika ufanyaji kazi lakini mpaka leo hamna anayetaka kufanyia kazi wazo.
Taasisi nyingi za kibiashara huwa zina kitu inaitwa "enterprise mindset that is open to change for the future"
Tunaweza kujifunza kwa wakoloni baada ya kuona raw materials zimepungua Ulaya wakaja Africa, wakenda Asia na Latin America kutengeneza makoloni ili ku-tap rasilimali.
Baada ya vuguvugu la uhuru kushika kasi, wakaja na neo colonialism strategy.

Msikize Dr. Arikana akionesha dhana ya ukoloni mambo leo unavyofanywa na Ufaransa model ambayo UK, US, Germany, China nao kwa namna moja ua nyingine wanazidi kukandamiza bara la Afrika.

Pole sana kwa changamoto, ila sio kwako peke yako; Afrika kwa ujumla nchi nyingi zimekosa kuwa na futuristic thinking au kama ipo, basi imezimwa ili tubaki tukishangaa shangaa tu japo ndio namna ukoloni mambo leo unazidi kushamiri kati ya nchi ambazo ilitakiwa ziwe huru holistically.
 
Yani rais anaagiza viwanda vijengwe? Duuh!
Naam, ilikuwa amri hiyo! Na vikajengwa kweli, kwa maelfu. Kila mkuu wa mkoa alijenga viwanda. Viwe vya mabua, vya karatasi, juu yake. Na hiyo kazi ilishakamilika. Tanzania ni nchi ya viwanda sasa! Magufuli oyee!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
magufuli wangu nakukumbuka kwani faili lambowe LA ugaidi lakubuni ulikataa wezako wamelibeba kama lilivo na kikwete hajui

Pumzika kwa amani

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Umenikumbusha huyu mama aliekuwa Rais wa Sri Lanka (1994-2005) Chandrika Bandaranaike Kumaratunga.

Tanzania tutafanya kosa kubwa kwa kumwona mama Samia kama Rais mwanamke. Urais hauna jinsi (Presidency has no sex);

Suala ni Rais kuwa shupavu kwenye kuhakikisha wasaidizi wake wanafanya kazi kutimiza malengo yenye kuakisi utimilifu wa Dira ya maendeleo.
Changamoto moja anayoa Rais wetu wa sasa SSH ambayo pia alikuwa nayo JPM; kuna sehemu ya wasaidizi kwa level ya mawaziri au wasaidizi wa ofisi ya Rais, wanafikiri kizamani sana kwenye namna ya kufikia lengo la kujenga uchumi wa kisasa.

Uchumi wa kisasa kukua kwa biashara za bidhaa na huduma ili kupanua tax base. Sasa tuulizane, ni mpaka lini tutategemea uwekezaji wa nje hata kwenye kubangua mchele?
Wakati tukiweza kubangua mchele na kuufanyia polishing na grading, soko la mashariki ya kati pekee hatutaweza kulifikia. Uwekezaji kama huu wahitaji strategy ya kutumia bank ya Kilimo au bank ya uwekezaji kutoa financial instrument kwenye ili wanawekeza (Watanzania) wakopesheke equipment na fedha ya kununua malighafi kwa wakulima, leseni ya international exports na TBS wakiwa ni wakaguzi wa ubora wa chakula wakisimamia shoo vema, foreign envoy walioko Saudia, Oman wakicheza nafasi yao, mbona mambo haya yanawezekana.

Wakati Rais Magufuli anapokea Boeng balozi wa US alikuwepo, hali kadhalika wakati anapokea Bombadier balozi wa Canada alikuwepo.

Hata kuzalisha mchele kwa packaging kama hii hapo chini, napo mpaka aje mwekezaji toka nje? Kuna pahala akili zetu tumezifungia kwenye makabati, ndio kinachonishangaza unakuta waziri msomi na mavyeti kibao, badala ya kuja na strategic policies ili tufanya majamboz kwenye exports kwenye dunia hii ambayo ina upungufu wa chakula ikiwemo mchele unaonukia toka Tz, ahh sijui wanamsaidia vip Mhe. Rais kwa kujenga uchumi jumuishi.
Halafu ukienda Bank ya uwekezaji unasikia, kuna fedha zimekosa wakopaji simply kuna masharti magumu ambayo wanaokidhi ni chini ya 20%. (Fuatilia hotuba ya wizara ya fedha 2019/20. Benki ya uwekezaji alitumia less than 20% kukopesha ili kukuza uwekezaji)

View attachment 1923677
KILIMO KWANZA ndiyo ilikuwa dira mama.Lakini ujuaji mwingi wa mwendazake ndiyo umeirudisha nyuma nchi katika kilimo ambacho ndiyo chachu ya kujengwa viwanda.
Huku Mngeta Morogoro kulikuwa na kiwanda cha KPL ambacho kililima zaidi ya ekta 50000 kipindi cha Kilimokwanza na huku kikinunua pia mpunga wa raia.
Kiwanda kilitoa ajira pia za kutosha kwa raia.
Lakini kikauwawa kipindi cha serikali ya awamu ya 5.
Kifupi ujuaji na chuki za Magu kwa mtangulizi wake zimerudisha nyuma kilimo ambacho ndiyo UTIWAMGONGO WA TAIFA.
 
Nakumbuka miaka ya mwazo ya mwendazake wimbo wa viwanda uliimbwa sana na tukaambiwa mtu ukiwa vyerehani vinne basi unakiwanda.

Wakaenda mbele zaidi na kusema kila mkoa unaviwanda zaidi ya 100 (hapa figure siikumbuki vizuri ila ilikua kubwa). Na tukaambiwa mpaka mwaka jana Tz kuna viwanda zaidi ya 8400!

Sasa najiuliza je viwanda siku hizi vimeishia wapi? Mbona wanasiasa hawaimbi tena wimbo wa viwanda?
Haipo yupo tu anazurura kutangaza utalii hewa ambao haupo[emoji16]
 
Njoo mkoa wa Pwani ujionee Tanzania ya viwanda inavyomeremeta.

Ukifungia na gaidi ufipa hutaelewa chochote.
Kada wa ccm ilala hamza mwanaccm kindakindaki,ccm mmepata gaidi no.1 kutokea tanzania,waulize policeccm wenu kawatwanga za kutosha
20210825_220518.jpeg
 
KILIMO KWANZA ndiyo ilikuwa dira mama.Lakini ujuaji mwingi wa mwendazake ndiyo umeirudisha nyuma nchi katika kilimo ambacho ndiyo chachu ya kujengwa viwanda.
Huku Mngeta Morogoro kulikuwa na kiwanda cha KPL ambacho kililima zaidi ya ekta 50000 kipindi cha Kilimokwanza na huku kikinunua pia mpunga wa raia.
Kiwanda kilitoa ajira pia za kutosha kwa raia.
Lakini kikauwawa kipindi cha serikali ya awamu ya 5.
Kifupi ujuaji na chuki za Magu kwa mtangulizi wake zimerudisha nyuma kilimo ambacho ndiyo UTIWAMGONGO WA TAIFA.
Kilimo kwanza hakijawahi kuwa na matokeo chanya zaidi ya magari GX V8, VX V8, tractors na power-tiller; na hapakuwa na mkakati wa masoko wa nini kinahitajika sokoni, soko lipi na soko lahitaji nini kwa ubora upi na wingi upi?

Mathalani, kama ni mpunga wakati wa kilimo kwanza, wakulima walihamasishwa ili walime mbegu gani ili soko lake liwe wapi?

nakumbuka enzi za kilimo kwanza kuna wakati wakulima walivuna mpunga wa kutosha halafu kuna jamaa wizara ya kilimo wakatoa vibali mchele toka Pakistani ukaingizwa na kuchanganywa na mchele wa ndani na wakulima wa Tanzania wakakosa soko.

Kilimo kibiasha ndio ingekuwa mpango mzima, ambapo soko la walaji wa mwisho ndilo liwe kichocheo cha nini kizalishwe shambani, kichakatwe kiwandani na kusindikwa kisha kiuzwe ikiwa ni siko la Tanzania, Comoro, EA, SADC, GCC au kwingineko.

Anyway, awamu ya 4 ishapita na awamu ya 5 ishapita; sasa ni wakati wa awamu ya 6; tujipange kwa mkakati wa kimasoko kuona tunalisongeshaje ili kuifikishia wakulima neema ya kila wanacholima kinachakatwa na kuuzwa na hiyo ndo dhana halisi ya kilimo-biashara. Tunakuwa na control ya product ya mwisho tokea mwanzo.
 
Back
Top Bottom