Umenikumbusha huyu mama aliekuwa Rais wa Sri Lanka (1994-2005)
Chandrika Bandaranaike Kumaratunga.
Tanzania tutafanya kosa kubwa kwa kumwona mama Samia kama Rais mwanamke. Urais hauna jinsi (Presidency has no sex);
Suala ni Rais kuwa shupavu kwenye kuhakikisha wasaidizi wake wanafanya kazi kutimiza malengo yenye kuakisi utimilifu wa Dira ya maendeleo.
Changamoto moja anayoa Rais wetu wa sasa SSH ambayo pia alikuwa nayo JPM; kuna sehemu ya wasaidizi kwa level ya mawaziri au wasaidizi wa ofisi ya Rais, wanafikiri kizamani sana kwenye namna ya kufikia lengo la kujenga uchumi wa kisasa.
Uchumi wa kisasa kukua kwa biashara za bidhaa na huduma ili kupanua tax base. Sasa tuulizane, ni mpaka lini tutategemea uwekezaji wa nje hata kwenye kubangua mchele?
Wakati tukiweza kubangua mchele na kuufanyia polishing na grading, soko la mashariki ya kati pekee hatutaweza kulifikia. Uwekezaji kama huu wahitaji strategy ya kutumia bank ya Kilimo au bank ya uwekezaji kutoa financial instrument kwenye ili wanawekeza (Watanzania) wakopesheke equipment na fedha ya kununua malighafi kwa wakulima, leseni ya international exports na TBS wakiwa ni wakaguzi wa ubora wa chakula wakisimamia shoo vema, foreign envoy walioko Saudia, Oman wakicheza nafasi yao, mbona mambo haya yanawezekana.
Wakati Rais Magufuli anapokea Boeng balozi wa US alikuwepo, hali kadhalika wakati anapokea Bombadier balozi wa Canada alikuwepo.
Hata kuzalisha mchele kwa packaging kama hii hapo chini, napo mpaka aje mwekezaji toka nje? Kuna pahala akili zetu tumezifungia kwenye makabati, ndio kinachonishangaza unakuta waziri msomi na mavyeti kibao, badala ya kuja na strategic policies ili tufanya majamboz kwenye exports kwenye dunia hii ambayo ina upungufu wa chakula ikiwemo mchele unaonukia toka Tz, ahh sijui wanamsaidia vip Mhe. Rais kwa kujenga uchumi jumuishi.
Halafu ukienda Bank ya uwekezaji unasikia, kuna fedha zimekosa wakopaji simply kuna masharti magumu ambayo wanaokidhi ni chini ya 20%. (Fuatilia hotuba ya wizara ya fedha 2019/20. Benki ya uwekezaji alitumia less than 20% kukopesha ili kukuza uwekezaji)
View attachment 1923677