Tanzania ya "viwanda" imeishia wapi?

Tanzania ya "viwanda" imeishia wapi?

Kilimo kwanza hakijawahi kuwa na matokeo chanya zaidi ya magari GX V8, VX V8, tractors na power-tiller; na hapakuwa na mkakati wa masoko wa nini kinahitajika sokoni, soko lipi na soko lahitaji nini kwa ubora upi na wingi upi?

Mathalani, kama ni mpunga wakati wa kilimo kwanza, wakulima walihamasishwa ili walime mbegu gani ili soko lake liwe wapi?

nakumbuka enzi za kilimo kwanza kuna wakati wakulima walivuna mpunga wa kutosha halafu kuna jamaa wizara ya kilimo wakatoa vibali mchele toka Pakistani ukaingizwa na kuchanganywa na mchele wa ndani na wakulima wa Tanzania wakakosa soko.

Kilimo kibiasha ndio ingekuwa mpango mzima, ambapo soko la walaji wa mwisho ndilo liwe kichocheo cha nini kizalishwe shambani, kichakatwe kiwandani na kusindikwa kisha kiuzwe ikiwa ni siko la Tanzania, Comoro, EA, SADC, GCC au kwingineko.

Anyway, awamu ya 4 ishapita na awamu ya 5 ishapita; sasa ni wakati wa awamu ya 6; tujipange kwa mkakati wa kimasoko kuona tunalisongeshaje ili kuifikishia wakulima neema ya kila wanacholima kinachakatwa na kuuzwa na hiyo ndo dhana halisi ya kilimo-biashara. Tunakuwa na control ya product ya mwisho tokea mwanzo.
Hivi wewe ni mkulima?Ulilima kweli wewe kipindi hicho?Au wewe ndiye wale wasomi karirishwa na field hampataki?.
 
Sasa hivi tupo Kwenye Tanzania ya "Royal Tour"
Rais linapenda safari za anasa hadi wasaidizi wake wamemuelewa wanamdanganya na kumuandalia ma tour ya ajabu ajabu
 
Hata kabla ya Magufuli mambo yalikuwa hayaendi vile inavyopaswa. Tuliomba sana tupate mbeba maono tukapata na kwa hakika alituonyesha njia japo kwa mkono wa chuma. Sasa hayupo tumerudi kwenye arifu A.

Misingi ya kuendesha nchi inapaswa kujengwa na kuwekewa uzio ili pale watawala wanapobadilika misingi iliyojengwa iwe endelevu... Kwa bahati mbaya hapa kwetu, hatutaki kujenga nchi zaidi sana ni kujijenga kwa mtu mmoja mmoja au kikundi katika mfumo wa kibepari.
Katiba itakayo mtaka kila rais aliyepo madarakani kusimamia malengo na sera za Taifa ndiyo suluhisho

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Sasa hivi tupo Kwenye Tanzania ya "Royal Tour"
Rais linapenda safari za anasa hadi wasaidizi wake wamemuelewa wanamdanganya na kumuandalia ma tour ya ajabu ajabu
Huu ndio muda wasaidizi wa Rais wananeemeka, sio msukuma yule alikuwa anawapeleka maporini kwenye miradi wakang'atwe na mbug'o na makolokolo mengine🤣
 
Nakumbuka miaka ya mwazo ya mwendazake wimbo wa viwanda uliimbwa sana na tukaambiwa mtu ukiwa vyerehani vinne basi unakiwanda.

Wakaenda mbele zaidi na kusema kila mkoa unaviwanda zaidi ya 100 (hapa figure siikumbuki vizuri ila ilikua kubwa). Na tukaambiwa mpaka mwaka jana Tz kuna viwanda zaidi ya 8400!

Sasa najiuliza je viwanda siku hizi vimeishia wapi? Mbona wanasiasa hawaimbi tena wimbo wa viwanda?
Tz ya kupambana na CHADEMA
 
So tumetoka kilimo kwanza, Tz ya viwanda na sasa tuko Tz ya utalii?
Kilimo kwanza, ilikuwa sera nzuri sana iliyoandaliwa na SUA. Tatizo, SUA wenyewe walitaharuki pale "final version" ya Kilimo Kwanza ilipotoka hadharani. Kilikuwa kitu tofauti kabisa. Hujuma kubwa ilifanyika ili kuwatajirisha wajanja. Ndio ukawa mwisho wa kilimo kwanza.
Huyu "kichaa" wa viwanda alidanganywa kwamba inawezekana "kuindustrialise" bila mapinduzi ya kilimo. Yeye alijenga viwanda kwa kutoa amri. Sasa hivi hata hawataki kusikia neno "viwanda".

Kuhusu utalii, Tunahitaji kujiuliza maswali ya msingi kwanza. Ni nini kinafanya Morocco iwe Namba 1 kwa utalii Afrika, wakati Tanzania yenye vivutio vikubwa zaidi ya Morrocco ikiwa chini ya namba 10? Baada ya hapo tutajua la kufanya kwa uhakika zaidi.
 
Una hoja ya msingi!! Ila safari tuliyo nayo ni ndefu.
 
Kama kichwa cha habari kinavyosema hapo juu, slogan ile ya Tanzania ya viwanda je shangaz ana hoja?

View attachment 1827986
Ukweli mtupu,Kuna fala mmoja alikuwa anapiga kelele kipindi Cha mwendazake,anatoa maagizo kwa kila mkuu wa mkoa ajenge viwanda 200!
Sasa hv hata hasikiki amepeleka ufala wake huko ofisi ya Makamu wa Raisi,Jafo
 
Aina za viwanda nayo ni issue, Mwalimu Nyerere alijenga viwanda vikubwa kabisa tokea vya kuchambua pamba hadi kutengeneza nguo mbali mbali.Bahati mbaya baada ya vita ya Kagera, IMF,na benki ya dunia walimkalia kooni,wakitaka viwanda vibinafsishwe na ndipo vilikufa kabisaa.
Viwanda hivyo vilitengeneza ajira kwa malaki ya watanzania.
Magufuli labda nae alitaka kufufua viwanda hivyo lakini akakosa mtaji kwa kuwa alitamani kila kitu kufanya lakini akakosa vipaumbele vya taifa.
Laiti hiyo pesa inayozikwa Dodoma ya kujenga makao makuu,ingepelelekwa kufufua viwanda vya nguo labda maana halisi ya viwanda ya Mwalimu Nyerere ingekamilika mapema mno.
 
Mbwembwe na takwimu hewa moja ya legacy kubwa ya Mwendazake.
Jamaa aliwajulia sana Watz, Watz wanapenda sana kusikia kuliko kusoma. Mtz akisikia atasimulia huyoo hata kama si kweli. Jamaa alitupiga kamba nyingi sana, na alipambana na yeyote anayejitia kutafuta taarifa sahihi.
 
Back
Top Bottom