Kilimo kwanza hakijawahi kuwa na matokeo chanya zaidi ya magari GX V8, VX V8, tractors na power-tiller; na hapakuwa na mkakati wa masoko wa nini kinahitajika sokoni, soko lipi na soko lahitaji nini kwa ubora upi na wingi upi?
Mathalani, kama ni mpunga wakati wa kilimo kwanza, wakulima walihamasishwa ili walime mbegu gani ili soko lake liwe wapi?
nakumbuka enzi za kilimo kwanza kuna wakati wakulima walivuna mpunga wa kutosha halafu kuna jamaa wizara ya kilimo wakatoa vibali mchele toka Pakistani ukaingizwa na kuchanganywa na mchele wa ndani na wakulima wa Tanzania wakakosa soko.
Kilimo kibiasha ndio ingekuwa mpango mzima, ambapo soko la walaji wa mwisho ndilo liwe kichocheo cha nini kizalishwe shambani, kichakatwe kiwandani na kusindikwa kisha kiuzwe ikiwa ni siko la Tanzania, Comoro, EA, SADC, GCC au kwingineko.
Anyway, awamu ya 4 ishapita na awamu ya 5 ishapita; sasa ni wakati wa awamu ya 6; tujipange kwa mkakati wa kimasoko kuona tunalisongeshaje ili kuifikishia wakulima neema ya kila wanacholima kinachakatwa na kuuzwa na hiyo ndo dhana halisi ya kilimo-biashara. Tunakuwa na control ya product ya mwisho tokea mwanzo.