ANAUPIGA MWINGI
JF-Expert Member
- Apr 14, 2022
- 389
- 757
Kumekuwa na hamasa nyingi sana tangu awamu zilizo pita kuhusu Tanzania ya Viwanda, na kumekuwa na mikakati mingi sana ya Tanzania ya viwanda, awamu ya 5 ilifikia wakati tukawa tunapewa na idadi ya viwanda kabisa na tukaambiwa kwamba ukiwa na vyerehani 4 basi ni kiwanda na ukiwa na mashine ya kusaga matunda nyumbani kwako yaani Blander tiyari ni kiwanda, hizi ni aina ya story ambazo nchi nyingine zilizo fanya mapindizi ya viwanda hawaku na aina hii na story. Hizi zilikuwa zinawezekana tu Tanzania yetu.
Ukija kwenye uhalisia hizi ni stories na hakuna Tanzania ya viwanda wala mapinduzi ya viwanda Tanzania hii, Wanasiasa wamekuwa sana wanahadaa raia na kutumia elimu duni kuhadaa kwamba tuko kwenye Tanzania ya viwanda kitu ambacho sio kweli kabisa, Tanzania ya viwanda ilikufa enzi za Mwinyi na ndio wakati Tanzania ya viwanda ilikufa kifo cha mende na haitakaa itokee tena na ni baada ya ujamaa kufa rasimu na kuruhusu soko huria na viwanda vyetu vichache vikashindwa kupambana na bidhaa za nje ambapo wenzetu walikuwa walisha jiandaa kitambo sana na Tanzania ya viwanda.
Kwa nini hakuna Tanzania ya Viwanda na huenda isitokee hivi karibuni? Sababu ni kama zifuatazo hapa chini;
HAKUNA TANZANIA YA VIWANDA BILA MAPINDUZI YA ELIMU-Tanzania tunajaribu kutanguliza mkokoteni mbele then punda nyuma kwenye mpinduzi ya viwanda, huwezi zungumzia mapinduzi ya viwanda wakati hakuna mapinduzi ya elimu ambayo ndio huibua wanasayansi wa kuleta mapinduzi ya viwanda, Nchi nyingi hasa za Asai ambazo sasa zinainukia kiviwanda ziklianza kwanza na mapunduzi ya elimu zao na hapo sasa ndio wakaanza kufanikisha mapinduzi ya viwanda. Enzi za Baba wa taifa kulikuwa kweli na mapinduzi ya elimu na ndio maana tukawa na viwanda ambayo asilimia 90 vilisha kufa sasa.sisi tunakwepa elimu na tunataka mapinduzi ya viwanda haiwezekani kamwe.
TUSHA KUBALI SOKO HURIA NO WAY OUT-Kariakoo ndio kitovu cha bishara Tanzania, ila sasa ukitembelea kariakoo asilimia 99 ya bidhaa zinatoka nje ya nchi, zinatoka China, India, Ulaya na baadhi ya nchi zingine za Asia kama Pakistani, Malaysia, Singapore, Thailand, Vietnam na kadhalika. Hii ni kinyume cha mapinduzi ya viwanda Dunia nzima, haiwezekani kitovu cha biashara cha nchi husika kiwe na bidhaa za nje kwa asilimia 99, ni sawa ufike Thailand ukute asilimia 99 ya bidhaa zinatoka nje hapana, au kwamba kule Mumbai India ukute asilimia 90 ya product zao ni za kutoka nje, Pale Kariakoo ni kielelezo tosha kwamba hatuna Tanzania ya viwanda na sio leo wala kesho tutakuwa nayo,Kwanza kwa kariakoo ni asilimia 100 ya bidhaa ni za kutoka nje.
HATUWEZI HUBIRI MAPINDUZI YA VIWANDA KWA KUAGIZA MSHINE CHINA- Kule juu nilisema mapinduzi ya viwanda huanza na elimu, sasa leo hii tunaagiza mashine China na India then tunakuja kusema tuko kwenye Tanzania ya viwanda, hapana, tunapaswa kuwa na mashine zetu, tunapaswa kuvumbua mitambo yetu wenyewe, jambo ambalo ni gumu sana kwa sasa kwa sababu ya elimu pia ambayo ndio ingetupa tekinolojia.
VIONGOZI WANAHUBIRI MAJI WANAKUNYWA WINE-Leo hii thamani kwenye ofisi za umma asilimia 99 zinatoka nje, nenda hadi ofisi za SIDO utakutana na viti vya kukalia kutoka China, sasa hiki ni kichekesho kikubwa sana, haiwezekani tuhubiri mapinduzi ya viwanda au Tanzania ya viwanda ilihali tunaagiza kila kitu kutoka nje ya nchi, hata ambavyo tungeweza kuzalisha wenyewe bado tunaagiza kutoka nje, haitawezekana kabisa hii Tanzania ya viwanda.
MAPINDUZI YA VIWANDA MAANA YAKE NI VIWANDA VYA MASHINE- Hivi viwanda vya juice na maji ya kunywa sio mapinduzi ya viwanda, kwenye ataifa ya viwanda huwa hivyo haviko kwenye orodha ya viwanda, tukisema viwanda India tunazungumzia viwanda vya mashine, viwanda vya madawa viwanda vya magari kama Tata hivyo ndio viwanda, Viwanda vya maji na juice huwa havihesabiwi kama viwanda.
TUNADHARAU VYA KWETU- Mapinduzi ya viwanda huendana na uzalendo wa kiwango cha juu kabisa, sasa sisi tunapenda bidhaa za nje sasa inawezekana vipi tukawa kwenye mapinduzi ya viwanda? Nguoa asilimia 100 zinayoka nje, hakuna anaye taka kuvaa hata batiki zetu, kila mtu anapiga nguo za kutoka Uturuki na China na kwingineko, hatuwezi kuwa na mapinduzi ya viwanda kama uzalendo ni zero kwetu, hivyo lazima kwanza tuwe na uzalendo.
Nini tunaweza fanya?

- Kabla ya yote lazima tuwekekeze kwenye elimu, bila elimu hakuna viwanda tusidanganyane, Serikali lazima iwekeze kwenye elimu na sio bora elimu bali ni leimu kweli, elimu ndio itakayo tuletea mapinduzi ya viwanda Tanania na wala sio hizi hadaa za viongozi wetu kwamba tuna Tanzania ya viwanda.
- Kuna baadhi ya bidhaa ni kupiga marufuku- Mfano hivi hatuwezi anza hata na Midoli? Kwa nini hadi midoli tuagize China na kutumia pesa za kigeni kuagiza midoli? Tuanze na vile vitu rahisi sana tuzalishe wenyewe, wakati tunapambana na elimu yetu.
- SIDO inahitaji kubadilishwa fikra, ujue wazo la SIDO baba wa Taifa alitoa India, make kule pia kuna SIDO kama ya kwetu, ila SIDO ya India ndio imeleta mapinduzi ya viwanda India wakati sisi SIDO yetu hadi leo unakuta wana fanicha za kutoka China.SIDO ibadilike kifira na pia iwezeswe sana ili ijue wajibu wake.
- Tuwekezekweye wabunifu wa mashine za ndani ya nchi, tuachane kuagiza mashine china na kuita mapinduzi ya viwanda, tuwekeze kwenye mashine zetu wenyewe hizo ndio maana ya mapinduzi ya viwanda na si vinginevyo.
- Serikali iwe mfano wa kwanza wa mapinduzi ya viwanda, haiwezekani ihubiri viwanda wakati wao offisi zao zimejaa fanicha za china, wanavaa viatu kutoka china, suti za kutoka uturuki, un akuta kiogozi asilimia 100 ya alicho vaa kinatoka China then anahubiri viwanda.
Upvote
0