Tanzania yaendelea kuwa sikio la kufa viwango vya FIFA

Tanzania yaendelea kuwa sikio la kufa viwango vya FIFA

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Habari wanaJF,

Tanzania yetu imeendelea kuwa sikio la kufa lisilo sikia dawa katika masuala ya soka, hii leo shirikisho la soka duniani FIFA limetoa viwango vipya vya ubora wa soka kwa mataifa yote wanachama wa shirikisho.

Basi taifa letu pendwa limeshika nafasi ya 144 hii inamaanisha kuwa Tanzania yetu imeporomoka kwa nafasi 12 kutoka nafasi ya 132 tuliyokuwa tukishikilia hapo awali.

Kwa mujibu wa FIFA kuanzia taifa la 56 mpaka la 1 hao ndio wapo katika kundi la walio bora zaidi, huku kuanzia mataifa yaliyoshika nafasi kuanzi ya 139 ndio wako katika hali mbaya sana.

Majirani zetu wako katika nafasi zifuatazo;

DR Congo - 49
Uganda - 72
Kenya - 85
Zambia - 94
Maawi - 100
Rwanda - 107
Burundi - 138


Tanzania tunatakiwa kujitafakari upya

FIFA.png
 
Kwa mpira huu wa weny vtambi tutaendeleaa kushuka tu mpaka tuwe wa mwisho
 
Nchi hii inaharibiwa na uswahili. Mpaka tutakapouacha USWAHILI tunaweza ku perform
 
Bado tupo juu kwa nafasi hiyo kwa mpira gani tulionao mpaka tuwe wa 144? Mikakati hakuna lipualipua jazz band unategemea nini?
 
Back
Top Bottom