May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Katika Mataifa ya kusini mwa Africa huwa nawahofia SA wenyewe, Zambia na Angola. Hawa waliobaki kama Botswana, Namibia, Malawi ni saizi yetu. Msumbiji wana utata kidogo lakini si kivile.
=========
TANZANIA imefufua matumaini ya kwenda Robo Fainali ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Namibia, bao pekee la kiungo Farid Mussa Malik dakika ya 65 akimalizia pasi ya mchezaji mwenzake wa Yanga, Ditram Nchimbi katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa Limbe, Cameroon.
Baada ya sare ya 1-1 katika mchezo uliotangulia jana jioni, sasa Guinea na Zambia zinalingana kwa pointi, nne kila timu zikifuatiwa na Tanzania yenye pointi tatu, wakati Namibia imeaga mashindano baada ya kufungwa mechi zote mbili za mwanzo.
Sasa Tanzania watatakiwa kushinda mechi yao ya mwisho ya kundi hilo dhidi ya Guinea Jumatano Uwanja wa Reunification, Douala ili kwenda Robo Fainali.