Tanzania yaingia ‘Top Ten’ mazingira bora uwekezaji Afrika

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
TANZANIA imeshika nafasi ya saba, katika nchi 20 zenye mazingira bora ya uwekezaji barani Afrika. Anaripoti Faki Sosi .

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 28 Oktoba 2019, Geofrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) amesema, utafiti huo huria uliofanywa na Kampuni ya APSA.

Amesema, APSA ni kampuni inayoaminika na wawekezaji kutokana na tafiti zao, na kwamba mwaka huu imetoa tafiti iliyoibeba Tanzania kutoka nafasi ya 15 mwaka jana hadi nafasi ya saba zenye mazingira rafiki ya uwekezaji Afrika.

“Ukilinganisha na mwaka jana tulishika nafasi ya 15, sasa tupo nafasi ya saba kwenye nchi 20 zenyenye mazingira mazuri ya uwekezaji,” amesema. Amesema, ipo ripoti nyingine ya ‘Doing Business’ iliyofanya na Shirika la Kifedha la Kimataifa (IFC), ambayo ni sehemu ya Benki ya Dunia (WB). Kwenye ripoti hiyo, wameshindanisha nchi mbalimbali duniani kwa kutumia vigezo 11 vinavyoanisha nchi yenye mazingira rahisi kufanya biashara.

Na kwamba, ripoti ya IFC imeangalia nchi 190 kubwa duniani ambapo Tanzania imekuwa nchi ya 141, mwaka jana kwenye idadi hiyo ya mataifa, Tanzania ilishika namba 144. Amesema, serikali inafanya juhudi zaidi kuhakisha Tanzania inapanda zaidi kutokana na miradi ya umeme, reli na ujenzi wa miundombinu.

SOURCE: MWANAHALISI ONLINE
 
Tunajitekenya na kucheka wenyewe!
 
Na mwaka 2015 tulikuwa wangapi? Katika vigezo vingi vya ubora, kwa sasa tupo chini kuliko tulivyokuwa 2015.
 
nchi yeyote ambayo ni developing country inatakiwa ivutie wawekezaji.
 
TANZANIA imeshika nafasi ya saba, katika nchi 20 zenye mazingira bora ya uwekezaji barani Afrika. Anaripoti Faki Sosi .

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 28 Oktoba 2019, Geofrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) amesema, utafiti huo huria uliofanywa na Kampuni ya APSA.

Amesema, APSA ni kampuni inayoaminika na wawekezaji kutokana na tafiti zao, na kwamba mwaka huu imetoa tafiti iliyoibeba Tanzania kutoka nafasi ya 15 mwaka jana hadi nafasi ya saba zenye mazingira rafiki ya uwekezaji Afrika.

“Ukilinganisha na mwaka jana tulishika nafasi ya 15, sasa tupo nafasi ya saba kwenye nchi 20 zenyenye mazingira mazuri ya uwekezaji,” amesema. Amesema, ipo ripoti nyingine ya ‘Doing Business’ iliyofanya na Shirika la Kifedha la Kimataifa (IFC), ambayo ni sehemu ya Benki ya Dunia (WB). Kwenye ripoti hiyo, wameshindanisha nchi mbalimbali duniani kwa kutumia vigezo 11 vinavyoanisha nchi yenye mazingira rahisi kufanya biashara.

Na kwamba, ripoti ya IFC imeangalia nchi 190 kubwa duniani ambapo Tanzania imekuwa nchi ya 141, mwaka jana kwenye idadi hiyo ya mataifa, Tanzania ilishika namba 144. Amesema, serikali inafanya juhudi zaidi kuhakisha Tanzania inapanda zaidi kutokana na miradi ya umeme, reli na ujenzi wa miundombinu.

SOURCE: MWANAHALISI ONLINE

Ni kweli kabisa na ni halali kushika nafasi hiyo, kwa hatua za makusudi zilizochukuliwa za kuondoa kero katika uwekezaji Tanzania..
 
Back
Top Bottom