joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
- Thread starter
- #21
Mkuu boda boda za Tanzania na Kenya zinafanya Safari za kuvuka mpaka zaidi ya safari 500 kwa siku kusafirisha wananchi na bidhaa, kumbuka kwamba chini ya Km 20 wananchi wa mipakani wanaruhusiwa kuingia na kutoka bila vibaliSwala ni kuachiwa tu au kujua wana kosa gani na sheria zao zinasemaje?.
Kwani kwa mfano Mkenya akiingia kwetu akafanya Uhalifu tutamuachia arudi kwao kwa sababu sio Mtanzania?
Pale Namanga na Terakea, wakenya huvuka mpaka kila jioni kuja Tanzania kunywa bia, wakiwemo POLISI wa Kenya, je mnataka nao pia tuwazuie, wananchi wa Taveta huvuka kuja Tanzania kutafuta huduma za Afya bila vibali, je mnataka tuwazuie
Anachouliza mkuu wa mkoa ni kwamba hizi sheria mnataka na upande wa Pili pia tuwe "strict?". Kama kweli Kenya inafuata sheria, basi wasiwaachie, hiyo itatusaidia na sisi kuwa strict, tuone nani watakaolalamika.