Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
Mipichaa imekuwa mingi kulikoHiyo mipichapicha sass😂
Punguzeni mawazo ya kitoto hili jukwaa la watu wenye umri mkubwa na akili timamu.kwanini wasikabidhi na karafuu, wanachukua mazao ya Tanganyika na kuyagawa
Tanzania tuna Ndege ya mizigo yenye uwezo wa kubeba Tani 500?TANZANIA YAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA NCHI YA MSUMBIJI
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi msaada wa tani 500 za mahindi kwa Serikali ya Jamhuri ya Msumbiji kufuatia mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo kutokana na mvua kubwa zilizonyesha.
Msaada huo umekabidhiwa Machi 24, 2026 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Shehena hiyo ya mahindi iliwasili jijini Maputo na ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania na kupokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Msumbiji uliongozwa na Waziri wa Mipango na Maendeleo, Mhe. Salim Cripton Valá,
Akikabidhi msaada huo, Mhe. Kombo alielezea uhusiano wa karibu na wakindugu uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ulioasisiwa tokea enzi za waasisi wa mataifa hayo mawili, Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Juliaus Kambarage Nyerere na Hayati Edward Mondlane. Waziri Kombo alisema kufuatia udugu huo, Rais Dkt. Samia amemtuma kufikisha msaada huo ili uweze kuwapunguzia adha waathirika wa mafuriko hayo.
"Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Rais Samia anatoa salamu za pole kwa Rais wa Msumbiji, Mhe. Daniel Chapo na watu wa Msumbiji kwa ujumla kutokana na madhila yaliyosababishwa na mafuriko haya na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari kundelea kutoa msaada kwa Msumbiji katika nyakati zote", Waziri Kombo alisema.
Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kombo alipata nafasi ya kukutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Maria Belvinda Levy kuhusu kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili, hususani kwenye masuala ya kiuchumi.
Serikali ya Msumbiji imetoa shukrani za dhati kwa kupokea msaada huo kutoka kwa ndugu zao Watanzania ambao unabainisha taswira ya ukaribu na ushirikiano wa kweli uliopo baina ya nchi mbili hizi.
View attachment 3562354View attachment 3562361View attachment 3562370View attachment 3562377View attachment 3562379View attachment 3562386
Au tani 5Tanzania hatuna Ndege ya mizigo yenye uwezo wa kubeba hata tani 100. Wewe mleta mada Tani 500 unafiri mchezo?
Au ulimaanisha Tani 50?
Unabisha ulikuwepooo🤣🤣Si mbaya ndio ujirqni mwema, lakini hapo kwenye ndege mkuu,Labda wamesafirisha kwa masemi, yale si ni tani 30 hivyo yakiwa 17 hivi tayari tani 500, lakini ndege, hhmm, tunayo ya tani 500 kweli?
Upo sahihi. Ndege ya kwanza ya Tanzania ya mizigo Boeing 767-300 ina uwezo wa kubeba tani 54 kwa mara moja. Hata ile ndege kubwa ya Mizo ya Ukraine iliyolipuliwa na Urusi Antonov An-225, ambayo ndo ilikuwa ndege kubwa ya mizigo duniani, iilikuwa na uwezo wa kubeba tanii 250 tu.Tanzania hatuna Ndege ya mizigo yenye uwezo wa kubeba hata tani 100. Wewe mleta mada Tani 500 unafiri mchezo?
Au ulimaanisha Tani 50?
NipoUnabisha ulikuwepooo🤣🤣
Tanzania hatuna Ndege ya mizigo yenye uwezo wa kubeba hata tani 100. Wewe mleta mada Tani 500 unafiri mchezo?
Au ulimaanisha Tani 50?
Kwani nyinyi mliishia darasa la ngapi?Upo sahihi. Ndege ya kwanza ya Tanzania ya mizigo Boeing 767-300 ina uwezo wa kubeba tani 54 kwa mara moja. Hata ile ndege kubwa ya Mizo ya Ukraine iliyolipuliwa na Urusi Antonov An-225, ambayo ndo ilikuwa ndege kubwa ya mizigo duniani, iilikuwa na uwezo wa kubeba tanii 250 tu.
wewe unajiona una akili timamu?Punguzeni mawazo ya kitoto hili jukwaa la watu wenye umri mkubwa na akili timamu.
Shehena hiyo ya mahindi iliwasili jijini Maputo na ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania na kupokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Msumbiji uliongozwa na Waziri wa Mipango na Maendeleo, Mhe. Salim Cripton Valá,
Ulivyo uliza swali watu watahisi wewe msomi.. Kabla ya kuuliza swali umesoma Thread?Kwani nyinyi mliishia darasa la ngapi?
Umeandika chuki zisizo na msingi.wewe unajiona una akili timamu?
Neno limetumika Tanzania, Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mahindi yamelimwa Tanganyika, pesa zilizotumika ni za Tanganyika kwani Zanzibar haichangii chochote. Nieleze chuki iko wapi wakati mtu w Zanzibar anagawa rasilimali zinazotoka Tanganyika labda kama wewe ni mnufaika.Umeandika chuki zisizo na msingi.