Tanzania yakabidhi msaada wa chakula kwa Msumbiji

Tanzania yakabidhi msaada wa chakula kwa Msumbiji

TANZANIA YAKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA NCHI YA MSUMBIJI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi msaada wa tani 500 za mahindi kwa Serikali ya Jamhuri ya Msumbiji kufuatia mafuriko yaliyoikumba nchi hiyo kutokana na mvua kubwa zilizonyesha.

Msaada huo umekabidhiwa Machi 24, 2026 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Shehena hiyo ya mahindi iliwasili jijini Maputo na ndege ya mizigo ya Shirika la Ndege la Tanzania na kupokelewa na Ujumbe wa Serikali ya Msumbiji uliongozwa na Waziri wa Mipango na Maendeleo, Mhe. Salim Cripton Valá,

Akikabidhi msaada huo, Mhe. Kombo alielezea uhusiano wa karibu na wakindugu uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji ulioasisiwa tokea enzi za waasisi wa mataifa hayo mawili, Baba wa Taifa, Hayati Mwl. Juliaus Kambarage Nyerere na Hayati Edward Mondlane. Waziri Kombo alisema kufuatia udugu huo, Rais Dkt. Samia amemtuma kufikisha msaada huo ili uweze kuwapunguzia adha waathirika wa mafuriko hayo.

"Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Rais Samia anatoa salamu za pole kwa Rais wa Msumbiji, Mhe. Daniel Chapo na watu wa Msumbiji kwa ujumla kutokana na madhila yaliyosababishwa na mafuriko haya na ameahidi kuwa Tanzania ipo tayari kundelea kutoa msaada kwa Msumbiji katika nyakati zote", Waziri Kombo alisema.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kombo alipata nafasi ya kukutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Maria Belvinda Levy kuhusu kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili, hususani kwenye masuala ya kiuchumi.

Serikali ya Msumbiji imetoa shukrani za dhati kwa kupokea msaada huo kutoka kwa ndugu zao Watanzania ambao unabainisha taswira ya ukaribu na ushirikiano wa kweli uliopo baina ya nchi mbili hizi.

View attachment 3562354View attachment 3562361View attachment 3562370View attachment 3562377View attachment 3562379View attachment 3562386
well done serikali sikivu ya CCM,
KAZI NA UTU, TUSONGE MBELE
 
Wala haisafishi October 29 , muuaji aliua watu wake waliomkataa.
downloadfile-354.jpg
 
Neno limetumika Tanzania, Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mahindi yamelimwa Tanganyika, pesa zilizotumika ni za Tanganyika kwani Zanzibar haichangii chochote. Nieleze chuki iko wapi wakati mtu w Zanzibar anagawa rasilimali zinazotoka Tanganyika labda kama wewe ni mnufaika.
Nimesoma katikati ya mistari hiyo sentensi yako nimeuona ubaguzi fulani, kinachofanyika Tanganyika kinafanyika pia Zanzibar huo unaitwa muungano.
 
Nimesoma katikati ya mistari hiyo sentensi yako nimeuona ubaguzi fulani, kinachofanyika Tanganyika kinafanyika pia Zanzibar huo unaitwa muungano.
unaweza kuniambia Zanzibar wanachangia shilingi ngapi kuendesha muungano, ila kinachotoka bara ndio kinatumika kama Tanzania.
 
unaweza kuniambia Zanzibar wanachangia shilingi ngapi kuendesha muungano, ila kinachotoka bara ndio kinatumika kama Tanzania.
Mwalimu Nyerere alisema angekuwa na uwezo angevisogeza visiwa vile mbali na pwani ya Bara, jiulize kwa kina kwanini alisema vile.

Msikilize Marehemu Lukuvi video yake kuhusu Zanzibar inatembea sasa hivi whatsapp.
 
Mwalimu Nyerere alisema angekuwa na uwezo angevisogeza visiwa vile mbali na pwani ya Bara, jiulize kwa kina kwanini alisema vile.

Msikilize Marehemu Lukuvi video yake kuhusu Zanzibar inatembea sasa hivi whatsapp.
Mwalimu Nyerere alishagundua alifanya kosa kuungana na watu ambao wana ubinafsi lakini hakutaka kurudi nyuma ila kuungana na watu kama hao ni tatizo kubwa.
 
Sisi ni majirani wa kweli kwa Msumbiji hatuachi kuwa nao kila mara wanapokuwa katika changamoto.
 
Back
Top Bottom