Tanzania yakabidhiwa gawio la Tsh. bilioni 100 kutoka Kampuni ya Twiga

Hili gawio ni baada ya muda gani, mwezi, mwaka, tuna hisa Twiga kwa zaidi ya miaka mitano lakini sijawahi kusikia tukipewa gawio au huwa tunapokea kimya kimya. Sasa hivi kwa vile ni kipindi Cha kampeni wameona itangazwe mubashara. Anayejua ukweli aweke hapa, vipi kulikuwa na gawi ,2015, 2016, 2017, 18,19? Au ni gawio mabeberu wakijisikia tu?
 
Idadi ya michango hasi/chanya kwenye uzi huu unaohusu ustawi wa Mama Tanzania imenifanya nitambue umuhimu wa Jamii formu kwa mustakabari wa ustawi wa nchi yetu......
Kumbe napoteza bando langu hapa!
 
Ripoti ya makinikia iliyoleta matunda haya,

Mgombea wa Urais kupitia Chadema Bwn. Lisu aliiita takataka.

Sasa ndio mtaona kuwa Lisu hana judgement nzuri, na hafai kuongoza nchi.
Ukisikia kufanywa wajinga ndio huku. Kampuni imeanzishwa January 2020, Leo in the middle of October tayari imesha fanya funga hesabu za mwaka, wakaguzi wameshapitia na tayari kutoa GAWIO lake?
Hii kampuni inaendeshwa kama genge LA Biriani la Mariamu Biriani pale Ilala?
Huwezi kufanya ubia mkubwa namna hiyo na kampuni ya kimataifa kama Barrick kisha mkaendesha mahesabu kihuni namna hiyo ambavyo ambavyo hata kampuni mbovu kama TAZARA tuu hawawezi fanya huo uhuni.
Wapi ripoti ya Bodi ya wakurugenzi kuhusu kupitisha gawio hilo?
Anyway, hesabu za TWIGA zinafungwa kila baada ya mwezi au miezi sita badala ya mwaka?
Sisi sio washamba kama nyie!
View attachment 1598875
 
Mada ni kuhusu Tanzania kukabidhia gawio la faida ikiyopatikana kati ya ubia wa Tanzania na Barrick, kupitia kampuni ya madini ya Twiga. Wewe unaibua hoja nje ya mada.

Kwa taarifa yako muda si mrefu utajua ukweli wahusika na uhakifu huo ni nani. Aibu utakayoipata itabaki moyoni mwako milele kwa kuwa unajificha nyuma "keyboard".
 
Mzee wa faru John anazikodolea macho hatari.Sio za saccos hizi, ni za watanzania kamanda. Wewe tafunaga ruzuku na michango ya wabunge wako.
 
Na mimi nasema acha kazi iendelee, nitamchagua tena Magufuli, nakushauri na wewe mchague Magufuli.
 
Kampeni hii!

Hii huenda ni chenji tu ya makinikia yaliouzwa nje baada ya kuzuiwa humu nchini maana tuliambiwa mchanga ule ilikuwa na madini ya thamani kubwa .
Hqkuna kitu. Ni hila na janjajanja ya kampeni tu. Hakuna hela yoyote inayolipwa. Mtaambulia kuona hundi bandia ikioneshwa, ama fedha toka benki kuu ikihesabiwa mbele ya waandishi wa habari na kisha kurudishwa tena.
 
Yote usemayo yanawezekana kabisa!
 
Inawezekana makubaliano kati ya Tanzania na Barrick ni mazuri sana kwa sasa, hofu yangu ni nguvu aliyo nayo rais kwa mujibu wa katiba yetu, inawezekana rais ajaye hata kutoka ccm akaamua kuuvunja na kuunda watakavyo, Maana hakuna wa kumuuliza.
 
Hizo ni flyover ngapi ?

Achana na ma-Flyovers ya bei kubwa, zungumzia vile vituo vya Afya kila Kata vya TZS 400 - 500M tutapata Vituo almost 200. There we go, tumecheleweshwa sana. Tukutane trh 28.
 
Inawezekana makubaliano kati ya Tanzania na Barrick ni mazuri sana kwa sasa, hofu yangu ni nguvu aliyo nayo rais kwa mujibu wa katiba yetu, inawezekana rais ajaye hata kutoka ccm akaamua kuuvunja na kuunda watakavyo, Maana hakuna wa kumuuliza.
Umeona mkataba?
 
Mzee wa faru John anazikodolea macho hatari.Sio za saccos hizi, ni za watanzania kamanda. Wewe tafunaga ruzuku na michango ya wabunge wako.
Mungu aliyetuletea John Pombe Magufuli kuwa rais ni Mungu anayeishi
 
Mungu aliyetuletea John Pombe Magufuli kuwa rais ni Mungu anayeishi
Mungu anayeishi hataki mtu muaji, mtekaji, anayepora wafanyabiashara fedha zao, anayepiga watu risasi, anayebagua majimbo yalichagua upinzani, n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…