Tanzania yakopa Tsh trilioni 2.4 kutoka IMF

Tanzania yakopa Tsh trilioni 2.4 kutoka IMF

Wakuu nawasalimu kwa jina la JMT..

Serikali ya Tanzania imefikia makubaliano na IMF ya kupatiwa mkopo mwingine wa masharti nafuu wa shilingi Tilioni 2.4..

Hizi ndio zile pesa Rais Samia awaliwaambia kule Tabora waharakishe kumalizia zile za awali maana nyingine nyingi zinakuja..

Nitoe wito kwa Serikali Kuhusu matumizi ya hizi pesa..kwamba this time around bil.400 ziende Zanzibar na Til.2 zibakie Bara..

Huku bara naomba Serikali iangalie uwezekano wa kujenga japo mradi mmja wa Barabara walau km 500 ambapo tunaweza kutumia bil.800 hivi na zitakazosalia zikafanye Kazi kama zilizofanya kwenye mkopo wa awamu ya kwanza..

Tunahitaji Sana Barabara Kati ya Makongolosi-Tabora/Singia via Rungwa,Ifakara-Songea na Njombe-Ifakara..Hizi ni barabara za muhimu sana kufungua fursa za Kiuchumi
Mkuu nakuunga mkono Songea -malinyi -ifakara then waunge malinyi -liwale
Makongorosi -ipole sikonge
 
Siku ya kulipa deni utashangaa hadi hewa unayovuta utailipia kodi, unapimwa uzito na kukadiriwa hewa unayovuta kwa siku, na TRA watakudai kila mwezi kodi ya hewa uliyovuta ili tulipe deni, nyie subirini tu
Acha makasiriko,timesaini $40b gesi..hiyo ni peanut tu,huyo wa Avatar yako alikua kavu Sana kukopa benki za biashara
 
Wakuu nawasalimu kwa jina la JMT..

Serikali ya Tanzania imefikia makubaliano na IMF ya kupatiwa mkopo mwingine wa masharti nafuu wa shilingi Tilioni 2.4..

Hizi ndio zile pesa Rais Samia awaliwaambia kule Tabora waharakishe kumalizia zile za awali maana nyingine nyingi zinakuja..

Nitoe wito kwa Serikali Kuhusu matumizi ya hizi pesa..kwamba this time around bil.400 ziende Zanzibar na Til.2 zibakie Bara..

Huku bara naomba Serikali iangalie uwezekano wa kujenga japo mradi mmja wa Barabara walau km 500 ambapo tunaweza kutumia bil.800 hivi na zitakazosalia zikafanye Kazi kama zilizofanya kwenye mkopo wa awamu ya kwanza..

Tunahitaji Sana Barabara Kati ya Makongolosi-Tabora/Singia via Rungwa,Ifakara-Songea na Njombe-Ifakara..Hizi ni barabara za muhimu sana kufungua fursa za Kiuchumi
Umesahau pia road ya Liwale to Mahenge kisha unatoboa hadi Njombe kama ulivyoandika. Watu wa nyanda za juu kusini hawakupaswa kuzunguka Songea wala Dar kwenda Lindi, Masasi, Liwale au Mtwara na ndio itakuwa the best road kwani itafungua sana eneo Zima la Malinyi, Ifakara, Mahenge, Liwale na Songea na baadae kupelekea kuundwa Mkoa mwingine eneo hili ambalo lipo mbali na makao makuu ya kila Mkoa
 
Thanks kwa kunikumbusha mkuu..

Kuna barabara ni muhimu sana kufungua uchumi..
 
Na mwishowe hili linakuwa hivi....
Kulingana na taarifa kutoka Shirika hilo, mkopo huo ambao ni kupitia Kitengo cha Mikopo ya Dharura unakusudiwa kuboresha mazingira ya Biashara
Sumu tamu na yenye kuvutia kwa harufu "Kuboresha Biashara"
na ushindani
Hapa ndiko sumu ilikojificha.... Ushindani. Watakuja na Sera zao za Uchumi Huria, wakiwa na MNCs zao kukusanya 2.4 zao na kubeba kile kidogo chetu, na kutuachia utumwa na utegemezi uliokomaa kwao.
na kuimarisha ukuaji wa kifedha.

=======
Ni utanuaji wa mirija ya Unyonyaji wao. Na wapumbavu wanakatikia mauno kufanikisha huo utumwa.
 
Kwahiyo hicho ndicho kinachojustify kukopa kama wendawazimu?
Kukopa kama wendawazimu.ndio kukoje huko?

Pili Kukopa ni lazima wala sio swala la kujivuta vita kwa sababu ukikopa unafanya on the spot na unaanza kula faida mda huo huo huku unalipa mdogo mdogo..
 
Ni rahisi sana kuwatawala watanzania akili zetu kama maroboti, natoa mifano

JPM hatukopi kwa mabeberu tunajenga kwa pesa zetu za ndani, watu walishangilia

SSH Tumepata mkopo wa covid-19 tumejenga madarasa nchi nzima, tunashangilia mama anaupiga mwingi sana. Ni mikopo juu ya mikopo,

Watanzania ni STAKI.....NATAkA,
 
Tanzania imefikia makubaliano na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) katika mpango wa muda wa kupata Tsh. 2,400,000,000,000 unaolenga kuendeleza Uchumi wa nchi uliodumazwa na Janga la COVID-19.

Kulingana na taarifa kutoka Shirika hilo, mkopo huo ambao ni kupitia Kitengo cha Mikopo ya Dharura unakusudiwa kuboresha mazingira ya Biashara na ushindani na kuimarisha ukuaji wa kifedha.

=======

Tanzania has reached an agreement with International Monetary Fund (IMF) in a medium term program to secure Sh2.4 trillion, the lender has announced.

In a statement released by IMF, it was revealed that the finalization of this agreement came from meetings between Tanzanian authorities and IMF that were held from May to June 2022 in Dodoma, Dar es Salaam and Zanzibar.

According to the IMF’s statement, this program is set to develop Tanzania’s economy.

“Tanzania’s economy is gradually recovering from the negative effects of COVID-19 pandemic but spillovers from the war in Ukraine are stalling the recovery. IMF emergency assistance under the Rapid Credit Facility (RCF), and additional support from other development partners, supported the authorities’ efforts to step-up the pandemic response, address fiscal pressures engendered by the pandemic response, and close financing needs,” the statement details.

It further disclosed that the medium term program aims at mobilizing domestic revenue and creating space for much needed investment in the country.

According to the communique, the investment will be in human and physical capital increased social spending, advancing the authorities’ structural reform agenda, including to improve the business environment and competitiveness, and strengthening financial deepening and stability.
Kukopa siyo tatizo, ila kuna mchwa unazila hizo fedha za mkopo
 
Kukopa kama wendawazimu.ndio kukoje huko?

Pili Kukopa ni lazima wala sio swala la kujivuta vita kwa sababu ukikopa unafanya on the spot na unaanza kula faida mda huo huo huku unalipa mdogo mdogo..
Trillion 10 tunayolipa kila mwaka kama mikopo na riba juu, yaani ulikopa trillion 6 kwa mwaka, ila unalipa trillion 10 baada ya riba, na bajeti kwa mwaka ni 30 trillion, kama si uwendawazimu, kuna msamiati gani mwingine?
 
Back
Top Bottom