Tanzania yakopa Tsh trilioni 2.4 kutoka IMF

Mkuu nakuunga mkono Songea -malinyi -ifakara then waunge malinyi -liwale
Makongorosi -ipole sikonge
 
Siku ya kulipa deni utashangaa hadi hewa unayovuta utailipia kodi, unapimwa uzito na kukadiriwa hewa unayovuta kwa siku, na TRA watakudai kila mwezi kodi ya hewa uliyovuta ili tulipe deni, nyie subirini tu
Acha makasiriko,timesaini $40b gesi..hiyo ni peanut tu,huyo wa Avatar yako alikua kavu Sana kukopa benki za biashara
 
Umesahau pia road ya Liwale to Mahenge kisha unatoboa hadi Njombe kama ulivyoandika. Watu wa nyanda za juu kusini hawakupaswa kuzunguka Songea wala Dar kwenda Lindi, Masasi, Liwale au Mtwara na ndio itakuwa the best road kwani itafungua sana eneo Zima la Malinyi, Ifakara, Mahenge, Liwale na Songea na baadae kupelekea kuundwa Mkoa mwingine eneo hili ambalo lipo mbali na makao makuu ya kila Mkoa
 
Thanks kwa kunikumbusha mkuu..

Kuna barabara ni muhimu sana kufungua uchumi..
 
Na mwishowe hili linakuwa hivi....
Kulingana na taarifa kutoka Shirika hilo, mkopo huo ambao ni kupitia Kitengo cha Mikopo ya Dharura unakusudiwa kuboresha mazingira ya Biashara
Sumu tamu na yenye kuvutia kwa harufu "Kuboresha Biashara"
na ushindani
Hapa ndiko sumu ilikojificha.... Ushindani. Watakuja na Sera zao za Uchumi Huria, wakiwa na MNCs zao kukusanya 2.4 zao na kubeba kile kidogo chetu, na kutuachia utumwa na utegemezi uliokomaa kwao.
na kuimarisha ukuaji wa kifedha.

=======
Ni utanuaji wa mirija ya Unyonyaji wao. Na wapumbavu wanakatikia mauno kufanikisha huo utumwa.
 
Kwahiyo hicho ndicho kinachojustify kukopa kama wendawazimu?
Kukopa kama wendawazimu.ndio kukoje huko?

Pili Kukopa ni lazima wala sio swala la kujivuta vita kwa sababu ukikopa unafanya on the spot na unaanza kula faida mda huo huo huku unalipa mdogo mdogo..
 
Ni rahisi sana kuwatawala watanzania akili zetu kama maroboti, natoa mifano

JPM hatukopi kwa mabeberu tunajenga kwa pesa zetu za ndani, watu walishangilia

SSH Tumepata mkopo wa covid-19 tumejenga madarasa nchi nzima, tunashangilia mama anaupiga mwingi sana. Ni mikopo juu ya mikopo,

Watanzania ni STAKI.....NATAkA,
 
Kukopa siyo tatizo, ila kuna mchwa unazila hizo fedha za mkopo
 
Kukopa kama wendawazimu.ndio kukoje huko?

Pili Kukopa ni lazima wala sio swala la kujivuta vita kwa sababu ukikopa unafanya on the spot na unaanza kula faida mda huo huo huku unalipa mdogo mdogo..
Trillion 10 tunayolipa kila mwaka kama mikopo na riba juu, yaani ulikopa trillion 6 kwa mwaka, ila unalipa trillion 10 baada ya riba, na bajeti kwa mwaka ni 30 trillion, kama si uwendawazimu, kuna msamiati gani mwingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…