Tetesi: Tanzania yaondolewa kwenye mradi wa kimataifa kuhusu nishati endelevu kikwazo kikiwa ni sheria ya takwimu

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Tanzania imeondolewa katika mradi wa kimataifa unaohusu mambo ya nishaji endelevu (sustainable energy management) sababu ikiwa ni matatizo ambayo wafadhiri wa mradi wanaona watapambana nayo kutokana na sheria ya Tanzania ya takwimu.

Mradi huo unahusu pia kuzifanyia upembuzi taarifa na takwimu zinazotolewa na serikali kuhusu nishati, na pale zinapoonekana zina makosa kutumia njia nyingine ziakazoonyesha nini kinapaswa kuwa kweli (interpolation/extrapolation methods). Wafadhiri wa mradi huo walielezwa kwamba sheria ya Tanzania kuhusu takwimu haitawaruhusu kutoa maoni mbadala juu ya takwimu za Tanzania, hata kama zinaonekana kuwa hazisemi kweli.

Zaidi ya hilo, wataalamu hao walikabiliana na tatizo la Tanzania kuhudhuria mikutano na semina za mradi huo pale ambapo zilifanyika nje ya Tanzania, kutokana na ugumu wa Watanzania kupata ruhusa ya kutoka nje ya nchi.

Hatimaye wafadhiri wa mradi huo, baada ya majadiliano na wahusika wa mradi upande wa Tanzania, waliamua kuiondoa Tanzania kwenye huo mradi.

NB: Siwezi kuweka source kwa kuogopa kuichongea hiyo taasisi ya kimataifa na watu walio kwenye wizara walioridhia Tanzania kuondolewa kwenye huo mradi.
 
Tanzania imeondolewa katika mradi wa kimataifa unaohusu mambo ya nishaji endelevu (sustainable energy management) sababu ikiwa ni matatizo ambayo wafadhiri wa mradi wanaona watapambana nayo kutokana na sheria ya Tanzania ya takwimu.

Mradi huo unahusu pia kuzifanyia upembuzi taarifa na takwimu zinazotolewa na serikali nishai, na pale zinapoonekana zina makosa kutumia njia nyingine zutakazoonyesha nini kinapaswa kuwa kweli (extrapolation methods). Wafadhiri wa mradi huo walielezwa kwamba sheria ya Tanzania kuhusu takwimu haitawaruhusu kutoa maoni mbadala juu ya takwimu za Tanzania, hata kama zinaonekana kuwa hazisemi kweli.

Zaidi ya hilo, wataalamu hao walikabiliana na taizo la Tanzania kuhudhuria semina za mradi huo pale abampo zilifanyika nje ya Tanzania, kutokana na ugumu wa wahudhuriaji wa semina kupata ruhusa ya kutoka nje ya nchi.

Hatimaye wafadhiri wa mradi huo, baada ya majadiliano na wahusika wa mradi upande wa Tanzania, waliamua kuiondoa Tanzania kwenye huo mradi.

NB: Siwezi kuweka source kwa kuogopa kuichongea hiyo taasisi ya kimataifa na watu walio kwenye wizara walioridhia Tanzania kuondolewa kwenye huo mradi.

Mungu Baba; tunakiri kuwa tumekosa. Tunakuomba utusamehe na utuondolee kikombe hiki.
 
Kila kitu kina hasara zake, waliwahi kusifia uwepo wa strong institutions, wakasahau zinaweza kukosea in general.
 
Pamoja na kuwa sina haja ya kubishana nawe Synthesizer ila Sheria ya Takwimu haikatazi kuksoa takwimu za NBS! Wala haikatazi kuchukua takwimu kwa matumizi ya taasisi au mtu binafsi! Ni kawaida wadau kukosoa kwa data takwimu rasmi kama 10 fundamental principle of official statistics. Tatizo ni watu wankurupuka na kutangaza takwimu zisizo na uhalisia kwa kutumia sample ambayo si representative of the population.
 
Mkuu, ubishane na mimi kwa sababu gani hasa, kwa kuwa wewe una asili ya ubishi tu au vipi? Mie naandika kilichotokea wewe unataka kubishana na mimi?
 
Sibishani nawe ila najaribu kuwaeleza ukweli katika hii sheria mnayoshadidia kila ukicha bila kuijua
 
Inawezekana basi unavyoitafsiri wewe sio wanavyotafsiri wengine. Kumbuka ninachosema siku zote - akili ndogo mamlaka makubwa. Kwani Tanzania tuna sheria ya kuzuia maandamano ya vyama vya siasa baada ya uchaguzi?
 
Akikujibu hili swali aweke nakifungu husika
 
Pamoja na kuwa sina haja ya kubishana nawe Synthesizer ila Sheria ya Takwimu haikatazi kuksoa takwimu za NBS! Wala haikatazi kuchukua takwimu kwa matumizi ya taasisi au mtu binafsi! Ni kawaida wadau kukosoa kwa data takwimu rasmi kama 10 fundamental principle of official statistics. Tatizo ni watu wankurupuka na kutangaza takwimu zisizo na uhalisia kwa kutumia sample ambayo si representative of the population.
We unajifanya unaakili na kujua kuitafsiri sheria ya takwimu kuliko serikali yetu tukufu iliyotunga hiyo sheria?
 
Hii nayo ni hadithi pia,

Eti siwezi kuweka source taonekana nawachongea

What the https://jamii.app/JFUserGuide!
 
Back
Top Bottom