Unachosema ni sawa, (simple logic). Lakini tunakusanya na kutumia vyema kadiri ya mahitaji yetu muhimu? Je, nini vipaumbele vyetu kama taifa? Na je matumizi yetu yanazingatia vipaumbele?
Mfano katika bajeti karibu kila wizara mwaka huu wa fedha 2013/2014, Jumla ya fedha inayotengwa kwa ajili ya Mishahara ya watumishi na MAENDELEO ni ni chini ya fedha inayotengwa kwa ajili ya matumizi mengine (kwa maana nyingine fedha inayotengwa kwa ajili ya matumizi mengineyo ni kubwa kuliko bajeti ya mishahra + Maendeleo), unategemea kuendelea kweli??? Utaendelea vipi wakati unatumia zaidi kuliko kuwekeza kwenyemaendeleo?