Tanzania yapata fursa nyingine za ajira 4,500 Nchini Qutar

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
๐—ง๐—”๐—ก๐—ญ๐—”๐—ก๐—œ๐—” ๐—ฌ๐—”๐—ฃ๐—”๐—ง๐—” ๐—™๐—จ๐—ฅ๐—ฆ๐—” ๐—ก๐—ฌ๐—œ๐—ก๐—š๐—œ๐—ก๐—˜ ๐—ญ๐—” ๐—”๐—๐—œ๐—ฅ๐—” ๐Ÿฐ,๐Ÿฑ๐Ÿฌ๐Ÿฌ ๐—ก๐—–๐—›๐—œ๐—ก๐—œ ๐—ค๐—”๐—ง๐—”๐—ฅ

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania imepata fursa nyingine za ajira zaidi ya 4,500 kwa ajili ya Watanzania walio tayari kufanya kazi nchini humo kwenye kada mbalimbali.

โ€œTunatarajia kupata nafasi nyingine 4,500 kwa ajili ya Watanzania ambazo ziko katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano ndiyo inaratibu zoezi zima kwa kushirikiana na wizara za kisekta ikiwemo ya Mambo ya Ndani pamoja na ile ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,โ€ alisema.

Tanzania imekuwa ikinufaika na fursa mbalimbali za ajira nchini Qatar ambapo hadi sasa kuna Watanzania 720 walioajiriwa kwenye Kampuni ya Taifa ya Usafirishaji ya Qatar (MOWASALAT) ikiwa ni sehemu ya nafasi za ajira 2,000 zilizotolewa katika awamu ya kwanza. Katika awamu ya pili, kampuni ya Power Holding International imetoa nafasi za ajira zaidi ya 4,000 kwa Watanzania wenye ujuzi mbalimbali.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatatu, Septemba 28, 2026) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ziara yake ya siku tatu nchini Qatar na manufaa ambayo Tanzania imepata kutokana na ziara hiyo. Dkt. Mwigulu alikuwa nchini Qatar kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani.

Akielezea kuhusu mazungumzo yao, Dkt. Mwigulu alisema walijadili kuhusu hati mbili za makubaliano ambazo zilisainiwa jana hiyohiyo na wakaafikiana kwamba hati moja iliyobakia ya kuepusha ukwepaji wa kodi na utozaji wa kodi mara mbili ikamilishwe ili isainiwe mapema iwezekanavyo.

Hati zilizosainiwa jana ni Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika maeneo ya Zimamoto, Uokoaji na Huduma za Dharura baina ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Taifa la Qatar na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nyingine ni Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa Kisiasa na Kidiplomasia baina ya Taifa la Qatar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

โ€œZiara hii kimsingi ililenga kutilia mkazo maeneo yaliyokubaliwa na viongozi wetu wakuu wa nchi wakati walipokutana,โ€ alisema.

Dkt. Mwigulu alitumia fursa hiyo kumwalika Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani afanye ziara nchini Tanzania ili kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili na kufuatilia utekelezaji wa mambo waliyokubaliana.

Alisema katika ziara yake alikutana pia na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika mwaka 2022 nchini Qatar. โ€œLengo lilikuwa ni kupata uzoefu wao katika kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa na yakafanikiwa kwa kiwango cha juu sana. Hii ni fursa kwetu kwa sababu Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoandaa michuano ya Kombe la Mataifa Huru ya Afrika hapo mwaka kesho,โ€ alisema.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu alifuatana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe, Katibu Wakuu (OR-Uwekezaji), Wabunge na watendaji wengine wa Serikali.
 
Attachments

  • VID-20260929-WA0043.mp4
    12.5 MB
  • IMG-20260929-WA0020.jpg
    IMG-20260929-WA0020.jpg
    224 KB · Views: 8
  • IMG-20260929-WA0014.jpg
    IMG-20260929-WA0014.jpg
    209.6 KB · Views: 9
  • IMG-20260929-WA0017.jpg
    IMG-20260929-WA0017.jpg
    212.5 KB · Views: 13
Tengenezeni ajira hapo hapo Tz kwanza....
 
Uarabuni hapana !!!! Sidhani. Hapafai kabisa.

Wanawake watafanywa watumwa wa ngono na wanaume watanyanyaswa kazi ngumu na kunyang'anywa passport kama walivyo wadhalimu hao
 
Mnapokea Watanzania kutoka SA mnapeleka wengine utumwani huko kwa Waarabu tutengeneze ajira hapa hapa Tanzania sio kwenda kufanya kazi za ndani huko kwa Waarabu.
 
Hivi nchi ya Qatar raia wake hawana changamoto ya ajira?
 
Hivi kwanini Lameck madelu na baraza zima plus Rais tusiwatafutie kazi hata Qatar alafu tutafute PM, Rais na Baraza zima la mawaziri kutoka huko huko Qatar waje kutusaidia kutengeneza ajira hapa hapa nchini??!!
Win win situation
 
Hati zilizosainiwa jana ni Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika maeneo ya Zimamoto, Uokoaji na Huduma za Dharura baina ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Taifa la Qatar na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nyingine ni Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa Kisiasa na Kidiplomasia baina ya Taifa la Qatar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hapa naona sana Sana ni maslahi ya wakubwa sioni mwananchi
 
๐—ง๐—”๐—ก๐—ญ๐—”๐—ก๐—œ๐—” ๐—ฌ๐—”๐—ฃ๐—”๐—ง๐—” ๐—™๐—จ๐—ฅ๐—ฆ๐—” ๐—ก๐—ฌ๐—œ๐—ก๐—š๐—œ๐—ก๐—˜ ๐—ญ๐—” ๐—”๐—๐—œ๐—ฅ๐—” ๐Ÿฐ,๐Ÿฑ๐Ÿฌ๐Ÿฌ ๐—ก๐—–๐—›๐—œ๐—ก๐—œ ๐—ค๐—”๐—ง๐—”๐—ฅ

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania imepata fursa nyingine za ajira zaidi ya 4,500 kwa ajili ya Watanzania walio tayari kufanya kazi nchini humo kwenye kada mbalimbali.

โ€œTunatarajia kupata nafasi nyingine 4,500 kwa ajili ya Watanzania ambazo ziko katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano ndiyo inaratibu zoezi zima kwa kushirikiana na wizara za kisekta ikiwemo ya Mambo ya Ndani pamoja na ile ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,โ€ alisema.

Tanzania imekuwa ikinufaika na fursa mbalimbali za ajira nchini Qatar ambapo hadi sasa kuna Watanzania 720 walioajiriwa kwenye Kampuni ya Taifa ya Usafirishaji ya Qatar (MOWASALAT) ikiwa ni sehemu ya nafasi za ajira 2,000 zilizotolewa katika awamu ya kwanza. Katika awamu ya pili, kampuni ya Power Holding International imetoa nafasi za ajira zaidi ya 4,000 kwa Watanzania wenye ujuzi mbalimbali.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatatu, Septemba 28, 2026) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ziara yake ya siku tatu nchini Qatar na manufaa ambayo Tanzania imepata kutokana na ziara hiyo. Dkt. Mwigulu alikuwa nchini Qatar kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani.

Akielezea kuhusu mazungumzo yao, Dkt. Mwigulu alisema walijadili kuhusu hati mbili za makubaliano ambazo zilisainiwa jana hiyohiyo na wakaafikiana kwamba hati moja iliyobakia ya kuepusha ukwepaji wa kodi na utozaji wa kodi mara mbili ikamilishwe ili isainiwe mapema iwezekanavyo.

Hati zilizosainiwa jana ni Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika maeneo ya Zimamoto, Uokoaji na Huduma za Dharura baina ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Taifa la Qatar na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nyingine ni Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa Kisiasa na Kidiplomasia baina ya Taifa la Qatar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

โ€œZiara hii kimsingi ililenga kutilia mkazo maeneo yaliyokubaliwa na viongozi wetu wakuu wa nchi wakati walipokutana,โ€ alisema.

Dkt. Mwigulu alitumia fursa hiyo kumwalika Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani afanye ziara nchini Tanzania ili kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili na kufuatilia utekelezaji wa mambo waliyokubaliana.

Alisema katika ziara yake alikutana pia na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika mwaka 2022 nchini Qatar. โ€œLengo lilikuwa ni kupata uzoefu wao katika kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa na yakafanikiwa kwa kiwango cha juu sana. Hii ni fursa kwetu kwa sababu Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoandaa michuano ya Kombe la Mataifa Huru ya Afrika hapo mwaka kesho,โ€ alisema.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu alifuatana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe, Katibu Wakuu (OR-Uwekezaji), Wabunge na watendaji wengine wa Serikali.
Kazi za uboi na uyaya! Zingekuwa kazi za ukweli wasingetutangazia wangegawana wenyewe wawape ndugu zao. Hizo ni kazi gani zisizo na ujuzi wa elimu kama udakitari, uinjinia, urubani na ubaharia, unakwenda kufanya kazi ambayo ukirudi unajikuta hauna muendelezo wa kujitegemea kutokana na ujuzi ulioupata!
 
Vijana wengi kabisa hapa kwetu wanasota hata ikitangazwa kazi ya laki 2 kwa mwezi wanashindania kinoma - ni bora baadhi wakajaribu bahati zao huko Qatar!
 
๐—ง๐—”๐—ก๐—ญ๐—”๐—ก๐—œ๐—” ๐—ฌ๐—”๐—ฃ๐—”๐—ง๐—” ๐—™๐—จ๐—ฅ๐—ฆ๐—” ๐—ก๐—ฌ๐—œ๐—ก๐—š๐—œ๐—ก๐—˜ ๐—ญ๐—” ๐—”๐—๐—œ๐—ฅ๐—” ๐Ÿฐ,๐Ÿฑ๐Ÿฌ๐Ÿฌ ๐—ก๐—–๐—›๐—œ๐—ก๐—œ ๐—ค๐—”๐—ง๐—”๐—ฅ

WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Tanzania imepata fursa nyingine za ajira zaidi ya 4,500 kwa ajili ya Watanzania walio tayari kufanya kazi nchini humo kwenye kada mbalimbali.

โ€œTunatarajia kupata nafasi nyingine 4,500 kwa ajili ya Watanzania ambazo ziko katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano ndiyo inaratibu zoezi zima kwa kushirikiana na wizara za kisekta ikiwemo ya Mambo ya Ndani pamoja na ile ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,โ€ alisema.

Tanzania imekuwa ikinufaika na fursa mbalimbali za ajira nchini Qatar ambapo hadi sasa kuna Watanzania 720 walioajiriwa kwenye Kampuni ya Taifa ya Usafirishaji ya Qatar (MOWASALAT) ikiwa ni sehemu ya nafasi za ajira 2,000 zilizotolewa katika awamu ya kwanza. Katika awamu ya pili, kampuni ya Power Holding International imetoa nafasi za ajira zaidi ya 4,000 kwa Watanzania wenye ujuzi mbalimbali.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumatatu, Septemba 28, 2026) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu ziara yake ya siku tatu nchini Qatar na manufaa ambayo Tanzania imepata kutokana na ziara hiyo. Dkt. Mwigulu alikuwa nchini Qatar kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani.

Akielezea kuhusu mazungumzo yao, Dkt. Mwigulu alisema walijadili kuhusu hati mbili za makubaliano ambazo zilisainiwa jana hiyohiyo na wakaafikiana kwamba hati moja iliyobakia ya kuepusha ukwepaji wa kodi na utozaji wa kodi mara mbili ikamilishwe ili isainiwe mapema iwezekanavyo.

Hati zilizosainiwa jana ni Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika maeneo ya Zimamoto, Uokoaji na Huduma za Dharura baina ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Taifa la Qatar na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nyingine ni Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano wa Kisiasa na Kidiplomasia baina ya Taifa la Qatar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

โ€œZiara hii kimsingi ililenga kutilia mkazo maeneo yaliyokubaliwa na viongozi wetu wakuu wa nchi wakati walipokutana,โ€ alisema.

Dkt. Mwigulu alitumia fursa hiyo kumwalika Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani afanye ziara nchini Tanzania ili kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili na kufuatilia utekelezaji wa mambo waliyokubaliana.

Alisema katika ziara yake alikutana pia na wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika mwaka 2022 nchini Qatar. โ€œLengo lilikuwa ni kupata uzoefu wao katika kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa na yakafanikiwa kwa kiwango cha juu sana. Hii ni fursa kwetu kwa sababu Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoandaa michuano ya Kombe la Mataifa Huru ya Afrika hapo mwaka kesho,โ€ alisema.

Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu alifuatana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe, Katibu Wakuu (OR-Uwekezaji), Wabunge na watendaji wengine wa Serikali.

wenzetu wanawekeza kwenye kazi za maana na kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta sisi tunapeleka ma housegirl uarabuni
 
Back
Top Bottom