Tanzania yapinga ripoti ya UN ya Tume ya Haki za Binadamu

Hiyo demokrasia ingekuwa inaminywa hata huyu Lissu asingekuwa anaropokaropoka upuuzi kama anavyofanya sasa hivi.
 
Hawa UN wakiendelea kutusumbua tutawafukuza hapa nchini na kuwatimua vibaraka wao wote.
 
Mambo ni mazuri kweli kweli huku, inaonyesha wanatuonea gere jinsi tunavyotenda haki bin haki [emoji4][emoji4]
Kabisa. UN wanatuonea gere sana kwa maendeleo lukuki tunayoyaona. Uchumi wa kati, Reli ya kisasa, meli za kisasa na bwawa la kuzalisha umeme Rufiji.
 
JE KWENYE HIYO RIPOTI YA UMOJA WA MATAIFA,KUHUSU HAKI ZA BINADAMU MAREKANI IMO?

MAUAJI YA POLISI KWA RAIA WAKE WENYE RANGI NYEUSI.

KUWAWEKEA VIKWAZO MAJAJI WA MAHAKAMA YA ICC THE HAGUE.

KUVAMUA NA KUUWA MARAIS HALALI WA NCHI, KAMA IRAQ,LIBYA, NA SASA SYRIA.

BLACK LIFE MATTER!
 
tunaanza tu uchaguzi mkafungia Tanzania daima kabudi mungu anakuona
 
Panya kanaswa mtegoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walipotuambia tumeingia uchumi wa kati uliyasema hayo?
Tujirekebishe,report hiyo itumike kurekebisha kasoro zilizopo kwani wanufaika ni watanzania!
Ni swala la muda tu, hata wasingesema nyakati zigewasuta!

Mazuri ni halali yetu kulingana na juhudi zetu na hatuhitaji kuonewa huruma katika hayo?

Ila uonevu ni mhimu kuupinga
 
Mambo ni mazuri kweli kweli huku, inaonyesha wanatuonea gere jinsi tunavyotenda haki bin haki [emoji4][emoji4]
Kabisa. UN wanatuonea gere sana kwa maendeleo lukuki tunayoyaona. Uchumi wa kati, reli ya kisasa, meli za kisasa na bwawa la kuzalisha umeme Rufiji. 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Hiyo report ipo sahihi ila CCM wanabisha tu kama kawaida yao.
-Ufisadi umekithiri
-Rushwa hasa viongozi wakuu wa nchi Rais Magufuli anawapendelea zaidi ndugu na marafiki zake
-Uhuru wa vyombo vya habari umebanwa
-Huduma za kijamii zinahujumiwa
-kiongozi mkuu wa nchi ni mbabe kwa wananchi
Mleta mada tunaomba mwenye nakala ya hiyo taarifa ya UN aiweke hapa Jamii Forums watanzania tuijadili.
 
Siku zote kukubali kosa ni sehemu ya kujisahihisha! Tusijindanganye kuwa kwenye kila kitu tupo sahihi! Wakitoa riport ya ukuwaji wa uchumi inayoonyesha tupo kushoto, haraka sana tunaipinga! Wakitoa riport ya haki za binadamu inayoonyesha hatuendi sawa nayo pia tunaipinga! Twaweza nao ambao wanaishi hapahapa wakitoa riport kushuka kwa mambo kadhaa, tunawapinga, tunawashambulia, tunamnyang'anya na mkurugenzi wake paspot! Najiuliza hivi Tanzania tumepatwa na ugonjwa gani hata tunajiona tupo sahihi na kutaka kusifiwa tu kwa kila kitu??? Wakati mwingine tukubali madhaifu yetu, hakuna mtu wala taifa linaloweza kuwa kamilifu 100% ndio maana kila siku tunaskia mawaziri wakuu wa mataifa mbalimbali kama Japan,Uk wakijiuzulu kuwajibika, Tujifunze japo hata kukubali tu!
 
Ni swala la muda tu, hata wasingesema nyakati zigewasuta!

Mazuri ni halali yetu kulingana na juhudi zetu na hatuhitaji kuonewa huruma katika hayo?

Ila uonevu ni mhimu kuupinga
Tunapinga uonevu?Yaani kuambiwa tunatesa raia wetu wenyewe wewe unasema tunaonewa!!!!
Mimi ni Mtanzania na nibaishi hapa hapa nchini,nadiriki kusema awamu ya tano imekandamiza sana haki za binadamu hasa wapinzani!
Akina Nusrat Henje wako jela miezi miwili na zaidi kwa jambo ambalo hata UVCCM wamelifanya!Hawafikishwi mahakamani kisa upelelezi na dhamana wamenyimwa!
Hapo kweli nahitaji mgeni aniambie kuwa haki zao zinakandamizwa?
 
Babayo Marekani, mapolice wake ndio wanaongoza kuwashuti watu weusi nchini mwao, Mbona hawasemi, Uonevu huanzia pale mtu mkubwa anapofanya mambo Yale Yale aliyoyafanya mdogo, Adhabu inakuwa ni ya mdogo pekee, huo ndio Uonevu

Napinga kina Nusurat kuwekwa ndani bila kosa, lakini kama wamefanya kosa ni halali Yao na hata wewe ukivunja Sheria ni sharti ushighurikiwe kisheria na utatetewa kisheria

Hivyo nakuomba, nenda ukawatetee hao Kwa mjibu wa sheria
 
CCM wachezeeni wote ila msicheze na UN, mtakuputika vibaya mno within no time.
 
Hiyo ni report ya UN ambapo na sisi ni wanachama,siyo report ya marekani!Lakini pia,ukitaka kujua status ya Marekani nenda katafute report zao kuhusu marekani!Hapa tujadili yaliyoko kwetu!

Kina Nusrat waliimba "Mungu ibariki Chadema",wako jela na hawana dhamana!
UVCCM waliimba "Mungu mmbariki Magufuli",wako wanaendelea na maisha kama kawaida!

Sihitahi mgeni aniambie kuna tatizo nchini kwetu!Maana hilo analoniambia naliona na kuliishi kila siku!
 
Ukweli mchungu.

Kwa sisi tunaoishi hapa nchini mbona tumeyashuhudia mengi tu. Haya yaliyoandikwa ni machache tu.
* Tumeshudia kina Idris Sultan wakiburuzwa mahakamani kwa kosa la uhuru wa habari

* Tumeshuhudia kwa miaka mitano Wapinzani wakizuiwa hata kufanya mikutano ya ndani lakini chama Tawala Kinafanya hadi mikutano ya hadhara

* Inshu ya wasiojulikana kuteka watu na miili ya watu kukutwa kwenye viroba kando ya mto Ruvu

* Pia siku za uchaguzi mkuu uliopita Network ilizimwa na mitandao ya kijamii mfano Jamiiforum iliingiliwa ilkawa haipo hewani

* Gazeti la Tanzania Daima kufungiwa

* Bunge kutoonyeshwa live

* Kuwatumbua watumishi wa umma jukwaani bila kufuata taratibu za kiutawala

* Wazungu watuache tu na mambo yetu ya Africa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…