Tanzania yapitisha Tani 455,000 za mizigo Mombasa mwaka 2024; Economic Intelligence iko wapi?

Tanzania yapitisha Tani 455,000 za mizigo Mombasa mwaka 2024; Economic Intelligence iko wapi?

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
9,818
Reaction score
14,585
20250628_154159.jpg

Pamoja na kuwa na bandari 3; Tanga, Dar es Salaam na Mtwara kwa mujibu wa kijarida cha CHANZO, kwa mwaka 2024 Watnzania wamepitisha Tani 455,000 za mizigo kwenye bandari ya Mombasa.

Je tunakosea wapi kama Taifa?
 
View attachment 3386839

Ngoja kwanza kabla sijacomment nikasome kile kitabu cha

The Confessions of The Economic Hitmen"
 
View attachment 3386839

Pamoja na kuwa na bandari 3; Tanga, Dar es Salaam na Mtwara kwa mujibu wa kijarida cha CHANZO, kwa mwaka 2024 Watnzania wamepitisha Tani 455,000 za mizigo kwenye bandari ya Mombasa.

Je tunakosea wapi kama Taifa?
Ulishawahi fanya biashara ya import and export mbwa wewe? Unajua mambo ya logistics ? Vitu gani vya kuzingatia ili bussiness ipate profit?
 
Bandari ya Dar es Salaam na Mombasa zinavyohudumia nchi jirani 2021-2024:

🔴 Shehena kubwa ya mzigo unaopita Tanzania unatoka DR Congo, na biashara hii imeendelea kukua. Hata hivyo shehena ya DRC inayopita Kenya imeendelea kuongezeka pia kutoka Tani 546,954 mwaka 2020 mpaka Tani Milioni 1.5 mwaka 2024.

🔴Uganda ndio mteja mkubwa wa Bandari ya Mombasa, biashara kidogo ya Uganda iliyokuwa ikipita Tanzania imeendelea kukauka.

🔴Rwanda inaendelea kutegemea bandari ya Dar es Salaam, hata hivyo shehena ya Rwanda inayopita Mombasa imeendelea kuongezeka pia, hii ikionesha ushindani mkali.

🔴Shehena ya Tanzania inayopita bandari ya Mombasa imeendelea kuongezeka kutoka Tani 232,101 mwaka 2021 mpaka Tani 455,000 mwaka 2024.

🔴Kati ya 2021 mpaka 2024, Bandari ya Dar es Salaam imehudumia Tani Milioni 32.7 ya shehena za nchi jirani na Bandari ya Mombasa imehudumia Tani Milioni 44.4 ya shehena ya nchi jirani.
 
Samia kutuharibia Nchi.Ameuza bandari zetu zote Kwa wajomba wake waarabu Kwa kutudanganya itakuwa fanisi na kuvutia watu wengi kumbe uongo mtupu.Huyu hakustahili kabisa kugombea Tena kuwa kiongozi maana atauza Kila kitu Kwa wajomba zake
 
Inawezekana kuna shida katika takwimu?? Kuna haja ya kuifuatilia hiki chanzo
Hapana ni kweli, na tatizo ni barabara mbovu kinyama upande wa Uganda, japo mara ya mwisho ilikuwa inafanyiwa ukarabati.

Kwa sasa mizigo ya Rwanda, Burundi na DRC upande wa juu waichukulie Dodoma, utaona mizigo itakuja mingi

Hilo gape la Uganda kupitisha mizigo mingi kuliko yote iliyopitishwa na landlocked ni noma
 
View attachment 3386839

Pamoja na kuwa na bandari 3; Tanga, Dar es Salaam na Mtwara kwa mujibu wa kijarida cha CHANZO, kwa mwaka 2024 Watnzania wamepitisha Tani 455,000 za mizigo kwenye bandari ya Mombasa.

Je tunakosea wapi kama Taifa?
Tupungeze tozo na ushuru.ili kuagiza gari na kupitisha Dar es Salaam iwe sawa na Mombasa.
 
Kama upo Mara mpaka mwanza je ni rahisi kupitia Dar ? Hio ni moja ila pia issue za Ukiritimba wewe kama mnunuzi unachoangalia mwisho wa siku ni gharama na uharaka...

Pia kuna volumes na uharaka wa mzigo kufika kama mtu unaagiza kutoka nje je CIF (Cost including Price) ya Mombasa na Dar ipoje ?

Kwahio bila kuchunguza taarifa kwa kina na kufanya due dilligence ni vigumu kuja na majibu ya jumla jumla
 
View attachment 3386839

Pamoja na kuwa na bandari 3; Tanga, Dar es Salaam na Mtwara kwa mujibu wa kijarida cha CHANZO, kwa mwaka 2024 Watnzania wamepitisha Tani 455,000 za mizigo kwenye bandari ya Mombasa.

Je tunakosea wapi kama Taifa?
We nani kakuambia ni kosa kupitishia mizigo bandari ya Mombasa? Mombasa ni karibu sana na kanda ya kaskazini, la muhimu ushindani serikali iimarishe bandari ya Tanga na miundo mbinu hasa barabara na reli ya kaskazini
 
Back
Top Bottom