Ndugu Industry ya Gas inahitaji uwekezaji wa mabilioni ya pesa
Bado serikali yako ipo kwenye Hatua za awali za ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata gesi kule Lindi kitakachogharimu zaidi ya Trillion 60 za Kitanzania. Hapo ndio tutaona faida ya gesi, na huenda ikaenda hadi 2030
Hata hivyo, Hadi sasa zaidi ya asilimia 50 ya Umeme wa grid ya Taifa unazalishwa kwa nishati inayotokana na gesi asilia ndio maana ule mgao wa Umeme uliotusumbua miaka mitano iliyopita haupo tena.
Ujenzi wa mitambo zaidi ya Kufua Umeme kutoka kwenye gesi asilia unaendelea Pale Kinyerezi ambao utaongezea megawati 450 kwenye grid ya Taifa.
Hapo kwenye Maziwa nakubaliana na wewe.
Tuna maziwa ya kumwaga huko vijijini, Mimi binafsi nipo mjini na hayo maziwa yao ya pakiti huwa situmii, natumia maziwa fresh yaliyokamuliwa moja kwa moja.
Serikali iruhusu imports za vitu walau vyenye tija.