Tanzania yaruhusu maziwa na sigara kutoka Kenya, nayo Kenya yaruhusu ngano na gesi kutoka Tanzania

Tanzania yaruhusu maziwa na sigara kutoka Kenya, nayo Kenya yaruhusu ngano na gesi kutoka Tanzania

Kama Tanzania tunafaidikaje kuipelela hiyo gesi Kenya hadi kuleta ugomvi wa kusutana na gesi yenyewe hatuzalishi?

Hiyo gesi inapelekwa na wafanyabiashara binafsi sio na serikali. Ukitaka kufaidika nenda kafanye biashara sio kupiga domo humu.
 
Halafu sisi tuna export gesi , hivi hii gesi yetu hadi sasa ni nani anayefahamu hasa faida yake kwa watanzania?

Gesi hii imetosheleza mahitaji ya tanzania? Tuliambiwa shida ya umeme itaisha lakini bado shida ipo.

Na ku-import maziwa sijaelewa kabisa yaani kwa sababu inaonekana hatuna upungufu wa maziwa. Tulihitaji kitu ambacho kwetu ni adimu sasa maziwa ya nini? Tunaupungufu wa maziwa?

Any way mi naona hayo makubaliano hayata leta tija yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nani kakwambia wewe unaexport gesi? Hiyo ni biashara ya watu binafsi na sio serikali, nenda na wewe kafanye ukitaka kufaidika.
 
Hiyo gesi inapelekwa na wafanyabiashara binafsi sio na serikali. Ukitaka kufaidika nenda kafanye biashara sio kupiga domo humu.

Hujaelewa mantiki ya swali we bi kigagula, kama biashara ni ya watu binafsi na si ya serikali , sasa ina uzito gani hadi kufikia kuhatarisha mahusiano ya hizi nchi mbili ?
 
Ndugu Industry ya Gas inahitaji uwekezaji wa mabilioni ya pesa
Bado serikali yako ipo kwenye Hatua za awali za ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata gesi kule Lindi kitakachogharimu zaidi ya Trillion 60 za Kitanzania. Hapo ndio tutaona faida ya gesi, na huenda ikaenda hadi 2030
Hata hivyo, Hadi sasa zaidi ya asilimia 50 ya Umeme wa grid ya Taifa unazalishwa kwa nishati inayotokana na gesi asilia ndio maana ule mgao wa Umeme uliotusumbua miaka mitano iliyopita haupo tena.
Ujenzi wa mitambo zaidi ya Kufua Umeme kutoka kwenye gesi asilia unaendelea Pale Kinyerezi ambao utaongezea megawati 450 kwenye grid ya Taifa.
Hapo kwenye Maziwa nakubaliana na wewe.
Tuna maziwa ya kumwaga huko vijijini, Mimi binafsi nipo mjini na hayo maziwa yao ya pakiti huwa situmii, natumia maziwa fresh yaliyokamuliwa moja kwa moja.
Serikali iruhusu imports za vitu walau vyenye tija.

Kama hajakuelewa Akapimwe Akili
Maelezo yako yanamtosheleza
 
Ndugu Industry ya Gas inahitaji uwekezaji wa mabilioni ya pesa, Bado serikali yako ipo kwenye Hatua za awali za ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata gesi kule Lindi kitakachogharimu zaidi ya Trillion 60 za Kitanzania. Hapo ndio tutaona faida ya gesi, na huenda ikaenda hadi 2030
Hapo pana typing error au umemaanisha?
 
Hujaelewa mantiki ya swali we bi kigagula, kama biashara ni ya watu binafsi na si ya serikali , sasa ina uzito gani hadi kufikia kuhatarisha mahusiano ya hizi nchi mbili ?


Asante! Ni watu binafsi ndoo wanaleta hizo gas mbaya Kenya, badala ya serikali ya Tz kuwashughulika,ati inaamua kuadhibu Kenya. Mtchew!
 
Kenya had said it would only allow wheat flour and other products milled from grain produced in Tanzania or whose full Common External Tariff rate has been applied.

Azam hapa mkao wa Kula!
 
Kama Tanzania tunafaidikaje kuipelela hiyo gesi Kenya hadi kuleta ugomvi wa kusutana na gesi yenyewe hatuzalishi?
Mkuu gas inaagizwa nje, ikifika hapa oryx, mihans na wengine wanabeba mitubgi yao wanaenda kujaza wanatuuzua sisi.
Hivyo hivyo hawazuiwi kupeleka mitungi yao waliyojaza gas kuuza kenya kwa faida.
Sisi gas yetu bado hatujaweza kuichakata kwa matumizi ya majumbani kama kupikia gas haichimbwi na kutumika moja kwa moja katika majumba gas zina level.
 
Hujaelewa mantiki ya swali we bi kigagula, kama biashara ni ya watu binafsi na si ya serikali , sasa ina uzito gani hadi kufikia kuhatarisha mahusiano ya hizi nchi mbili ?
Mostly serikali haifanyi biashara, serikali inasimamia ukusanyaji wa kodi na kuweka mazingira mazuri ya kufanyika kwa biashara ili iweze kupata kodi yake.
Hivyo hivyo serikali lazima ilinde masirahi ya wafanyabiashara maana bila wao kufanya biashara hakuna kodi.
Mapato yanayopatikana kwa kuuza gas kenya yanarudi nchini na yana boost uchumi mkuu.
 
Asante! Ni watu binafsi ndoo wanaleta hizo gas mbaya Kenya, badala ya serikali ya Tz kuwashughulika,ati inaamua kuadhibu Kenya. Mtchew!
Nani kakwambia serikali haishughulikii, nimeshakuelewesha kwenye post ingine, serikali lazima ishughulikie kwanza, kabla haijafikia consumers, Kenya likewise and other countries.
 
Hapo pana typing error au umemaanisha?

Hamna makosa, kiwanda cha kuchakata gesi (LNG plant) kinachotarajiwa kujengwa Lindi kina gharama ya US$ 30b (kama Tsh trilioni 66). Kiwanda hiki kitakuwa kinageuza gesi kuwa kimiminika kwa ajili ya kuisafirisha. Hapo ndio faida kubwa zaidi ya gesi kiuchumi itakapoanza kuonekana.

Kiwanda hiki kwa taarifa za karibuni kitakamilika mwaka 2029, bado maongezi ya ujenzi yanaendelea kati ya serikali na wawekezaji.
 
He hee, MK254 vipi ile mashine ya kukagua gesi fake inoliopuka toka Tz and other bs. Unyang'au tu ndio mnaweza, na tutawanyoosha, ndio kwaanza kunakucha pande hii. Mtabana na kuja na mashine za kila aina, ila mtaachia tu. Nyinyi hamuwezi isumbua Tz hata kidogo, we have all the advantages.

Akili za kuambiwa uwe unaongeza na zako pia, ufahamu biashara za kimataifa hazifanywi kama unavyofanya kwenye genge lako hapo kitaa. Waziri wenu wa mambo ya kigeni amekuja Kenya kuzungumzia hili suala, hapo lazima busara ingetumika, maana hatuna hulka ya kukomaa na mambo ya kitoto kama mfanyavyo.

Waziri wenu bwana Mahiga na rais wenu wote wameongea na uongozi wa Kenya, hivyo wameingia kwenye makubaliano ya kuachia vikwazo vyovyote wakati mikakati muafaka inapatikana. Hivyo mashini za kupima gesi uchwara bado zitawekwa, kilichotendeka ni kuachia muendelee kama bado tunawekeza kwenye hizo mashini, japo pia najua lazima waziri ameahidi kwamba atahakikisha amedhibiti ukajanja wenu wakati huu ambapo tumeachia kabla mashini kufika.
 
Gesi kwetu haitoshi lakini wanataka waipeleke kenya!!

Basi kama ni hivyo tutaendelea kukata miti ili tuchome mkaa
Mkuu unatumia gesi?,kuna siku umeenda kununua gesi ukakosa kwa sababu haitoshi?
 
Back
Top Bottom