Tanzania yasaini mikataba minne na Falme za Kiarabu ndani ya mwaka mmoja.
1. Kuendeleza uwanja wa ndege wa KIA
2. Ushirikiano na Posta Tanzania
3. Kuendeleza misitu yote nchini na TFS
4. DP World na TPA
1. Kuendeleza uwanja wa ndege wa KIA
2. Ushirikiano na Posta Tanzania
3. Kuendeleza misitu yote nchini na TFS
4. DP World na TPA
- Tunachokijua
- Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Serikali yake imepewa madaraka ya kushirikiana na kuingia makubaliano na nchi nyingine, Taasisi na Mashirika mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya watu wake.
Katika kuhakikisha kuwa madaraka hayo yanatekelezwa ipasavyo, Bunge ambalo ni chombo cha uwakilishi wa wananchi limepewa madaraka ya kuridhia Mikataba ya Kimataifa iliyoingiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo masharti yake yanahitaji kuridhiwa na Bunge. Madaraka hayo yametolewa chini ya Ibara ya 63(3) (d) na (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977
Mkataba wa Kimataifa ni makubaliano ya kimaandishi yenye nguvu ya kisheria baina ya pande mbili (bilateraltreaty) au zaidi (multilateral treaty) zinazotambulika kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Pande hizo zimehiari kushirikiana katika kufanikisha utekelezaji wa jambo fulani. Katika Mwongozo huu maana hiyo inajumuisha pia Matamko (Declarations), Itifaki (Protocols), Maagano ya Kimataifa (Conventions) na Mapatano (Pacts). Mikataba ya Kimataifa inaweza kuwa baina ya nchi mbili au zaidi.
Mkataba wa Makubaliano/ Memorandum of Understanding(MOU) ni nini?
Mkataba wa maelewano ni makubaliano kati ya pande mbili au zaidi yaliyoainishwa katika hati rasmi. Sio lazima kisheria, ambayo inategemea dhamira ya watia saini na lugha katika makubaliano, lakini inaashiria nia ya wahusika kusonga mbele na mkataba.
MOU inaweza kuonekana kama mahali pa kuanzia kwa mazungumzo kwani inafafanua upeo na madhumuni ya mazungumzo. Memorandam kama hizo mara nyingi huonekana katika mazungumzo ya mikataba ya kimataifa lakini pia zinaweza kutumika katika shughuli za biashara zenye viwango vya juu kama vile mazungumzo ya kuunganisha.
Je, Tanzania ilisaini mikataba minne na Falme za Kiarabu ndani ya mwaka mmoja?
1. Kuendeleza uwanja wa ndege wa KIA 2. Ushirikiano na Posta Tanzania 3. Kuendeleza misitu yote nchini na TFS 4. DP World na TPA?
JamiiForums imefanya mawasiliano na Msemaji wa Serikali pamoja na taasisi tajwa kuhusika na kusaini mikataba na falme za kiarabu, Tanzania ilisaini mikataba ya makubaliano (MoU) pamoja na mashirikiano na Falme za kiarabu Mwaka 2022.
1. Uwanja wa ndege KIA
Mwezi Juni, 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa KADCO alikuwa miongoni mwa waliombatana na Dokta Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania katika ziara ya kiserikali aliyoifanya nchini Oman. Katika ziara hiyo, mnamo tarehe 13, Juni, 2022, KADCO na Kampuni ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege nchini Oman (Oman Airports Management Company – OAMC) walisaini makubaliano (Memorandum of Understanding) yenye muda wa miaka miwili kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu (feasibility study) wa miradi mitatu iliyopo kwenye mpango wa muda mrefu wa uendelezaji wa eneo la KIA (KIA Master Plan). (Soma zaidi)
Miradi hiyo ni;
i Mradi wa Ujenzi wa hoteli ya nyota tano ambao umetengewa eneo lenye ukubwa wa Hekta 32;
ii. Mradi wa ujenzi wa eneo la biashara mchanganyiko (Business Complex) ambao umetengewa eneo lenye ukubwa wa Hekta 195; na
iii. Ujenzi wa jengo la watu/wafanyabiashara mashuhuri (CIP – Terminal) ambao umetengewa eneo la Hekta
Lengo la makubaliano haya ni kuwawezesha OAMC kufanya upembuzi yakinifu ili kubaini kama miradi hiyo italipa kibiashara (Commercially viable). Kama ikibainika kwamba, miradi hiyo italipa italipa, mazungumzo yatafanyika ili kuangalia namna bora ya kushirikiana katika utekelezaji wa wake.
2. Ushirikiano na Posta Tanzania
Tarehe 28 Februari 2022 Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Bw.Macrice Mbodo alikutana na kufanya mazungumzo na Bw. Abdulla Mohammed Alashram, Mtendaji Mkuu wa Posta ya Falme za Kiarabu (Emirates Posts Group) kwa lengo la kukuza na kuendeleza mashirikiano yaliyopo baina ya Mashirika haya mawili na kuanzisha mashirikiano mapya kwa ajili ya ustawi wa pande zote mbili.
Mazungumzo hayo yaliyolenga kukuza mashirikiano katika nyanja kuu tatu za Biashara ikiwemo Duka Mtandao, Huduma za Fedha na Uwakala pamoja na Huduma za usafirishaji wa Mizigo, Nyaraka, Barua na Vifurushi baina ya nchi hizi mbili na nchi za jirani, yamefanyika tarehe 28 Februari, 2022, jijini DUBAI kwenye makao makuu ya Posta ya EMIRATES POSTS GROUP.
Mazungumzo hayo yalifanyika wakati Kaimu Postamasta mkuu Bw. Mbodo akiwa DUBAI kushiriki maonesho makubwa ya biashara Duniani yajulikanayo kama DUBAI EXPO 2020.
Posta Tanzania walifafanua kwa undani juu ya mashirikiano haya waliyofanya na Falme za kiarabu kupitia page yao ya Twiter wakati wakimjibu mdau aliyekuwa kitaka kujua juu ya makubaliano waliyoingia, unaweza kufungua kiungo kuona zaidi( Soma zaidi)
3. Kuendeleza misitu yote nchini na TFS
Serikali ya Tanzania ilisaini hati ya makubaliano (MOU) na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa ajili ya kutusaidia kuendeleza misitu yote nchini, inayosimamiwa na Wakala wa misitu (TFS).
Taasisi ya Blue Carbon UAE na Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) walitia saini Mkataba wa Makubaliano kuashiria kuanza kwa ushirikiano wenye lengo la kuendeleza usimamizi endelevu wa misitu na kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi. Dubai chini ya uenyekiti wa Mfalme Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum.
Dk Jafo alisema hii ni mara ya kwanza kwa makubaliano hayo baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kukamilisha maandalizi ya miongozo ya biashara ya kaboni Oktoba 2022. (Soma zaidi)
4. DP World na TPA
Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Dubai Expo 2020 na kikao alichofanya na Mtawala wa Dubai Februari 2022 kuhusu fursa za uwekezaji nchini Tanzania ambapo ilipelekea Tanzania kuingia mkataba wa makubaliano na Falme za Kiarabu.
Tanzania iliingia Mkataba wa Makubaliano (MoU) kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na DP World (DPW) uliosainiwa katika ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwenye Maonesho ya Dubai 2020 (Dubai Expo) tarehe 28 Februari, 2022.
Moja ya matakwa katika Mkataba wa Makubaliano ni kuhusu maeneo ya ushirikiano kati ya TPA na DPW kwa ajili ya kuendeleza au kuboresha uendeshaji na usimamizi wa miundombinu ya kimkakati ya Bandari za Bahari na Maziwa Tanzania, kanda maalum za kiuchumi, hifadhi za usafirishaji na ukanda wa kibiashara wa Serikali ya Tanzania; (Usome mkataba wa makubaliano)
Kwa Mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesikika katika mtandao wa clubhaouse na Twiter akifafanua kuwa huu si mkataba kati ya TPA na DP World bali ni makubaliano ambayo baada ya kupitishwa na bunge la Tanzania ( Tayari umepitishwa soma, Bunge lapitisha Mkataba wa makubaliano) kwa mkataba huu wa awali Serikali itakaa na wawekezaji waweze kuuchakata kabla ya kuwa mkataba kamili. (Sikiliza Zaidi)