Tanzania yashika nafasi ya 6 Duniani kwa watu ambao wanaoishi na umasikini

Tanzania yashika nafasi ya 6 Duniani kwa watu ambao wanaoishi na umasikini

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Taasisi ya World Data Lab imetoa takwimu mpya zinazoonyesha nchi zenye idadi kubwa zaidi ya watu wanaoishi katika hali ya umaskini uliokithiri duniani kwa mwaka 2026.

Kulingana na data hizo, Nigeria inongoza orodha hiyo kwa kuwa na watu milioni 73.1 wanaoishi katika umaskini uliokithiri, ikifuatiwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yenye watu milioni 71.6.

Nchi nyingine zilizoorodheshwa ni Afghanistan (milioni 35.2), Msumbiji (milioni 25), Yemen (milioni 24.2), na Tanzania inashika nafasi ya sita kwa kuwa na watu milioni 23.9.
Orodha kamili ya nchi kumi za juu ni kama ifuatavyo:
1. Nigeria – milioni 73.1
2. DRC – milioni 71.6
3. Afghanistan – milioni 35.2
4. Msumbiji – milioni 25
5. Yemen – milioni 24.2
6. Tanzania – milioni 23.9
7. Madagascar – milioni 20.1
8. Uganda – milioni 18.2
9. India – milioni 14.46
10. Ethiopia – milioni 14.3
Taasisi hiyo imeeleza kuwa takwimu hizo zinatokana na uchambuzi wa hali ya sasa ya umaskini ulimwenguni.


Chanzo: Bongo five



Taasisi ya World Data Lab imetoa takwimu mpya zinazoonyesha nchi zenye idadi kubwa zaidi ya watu.jpg
 
Back
Top Bottom