Taarifa kutoka Barani Afrika zinaeleza kwamba , Tanzania imepata Heshima kubwa Duniani baada ya kupanda juu kwenye orodha ya nchi zinazoongoza kwa Ushirikina , huku ikiwa imezidiwa na nchi ya Cameroon Pekee ambayo ndio namba 1 , Tanzania imepanda hadi nafasi ya Pili
Kupanda juu kwa Tanzania kwenye List ya Uchawi barani Africa kunatokana na juhudi kabambe za mauaji yanayotokana na imani za kishirikina ya Wazee 117 , takwimu hii ya kujivunia inaanzia July 2017 hadi May 2018 .
Taarifa zaidi zinaonyesha kwamba kati ya waliouawa wamo wanaume 91 na wanawake 26 , huku Mkoa wa Tabora ukiongoza kwa mauaji hayo .
Jambo hili limefichuliwa na Ofisa wa Kituo cha sheria na Haki za binadamu ( LHRC ) , Fundikira Wazambi .
Chanzo : Mwananchi