Tanzania yashiriki CHOGM, yalenga kuimarisha Diplomasia ya Uchumi na Ushirikiano

Tanzania yashiriki CHOGM, yalenga kuimarisha Diplomasia ya Uchumi na Ushirikiano

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
π—§π—”π—‘π—­π—”π—‘π—œπ—” π—¬π—”π—¦π—›π—œπ—₯π—œπ—žπ—œ π—–π—›π—’π—šπ— , π—¬π—”π—Ÿπ—˜π—‘π—šπ—” π—žπ—¨π—œπ— π—”π—₯π—œπ—¦π—›π—” π——π—œπ—£π—Ÿπ—’π— π—”π—¦π—œπ—” 𝗬𝗔 π—¨π—–π—›π—¨π— π—œ 𝗑𝗔 π—¨π—¦π—›π—œπ—₯π—œπ—žπ—œπ—”π—‘π—’ π—ͺ𝗔 π—¦π—˜π—žπ—§π—” π—•π—œπ—‘π—”π—™π—¦π—œ

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameshiriki Mkutano wa Viongozi wa Jumuiya ya Madola na Watendaji Wakuu wa Makampuni uliofanyika tarehe 2 Novemba 2026, katika Kisiwa cha Antigua, nchini Antigua na Barbuda.

Mkutano huo wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) umewakutanisha viongozi wa nchi wanachama na watendaji wa sekta binafsi kujadili fursa za kukuza uwekezaji, kuimarisha ustahimilivu wa uchumi na kuongeza ajira katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.

Majadiliano katika mkutano huo yalijikita katika maeneo ya miundombinu, nishati jadidifu, kilimo na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Vilevile, yalisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa vitendo kati ya serikali na wawekezaji pamoja na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

Pembezoni mwa mkutano huo, Waziri Kombo alikutana na kufanya mazungumzo na Mfalme Charles III, Waziri Mkuu wa Uingereza, Mhe. Andy Burnham, Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda, Mhe. Gaston Browne, pamoja na Gavana Mkuu wa Antigua na Barbuda, Mhe. Sir Rodney Williams.

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huo umetoa fursa ya kuimarisha mahusiano ya kimataifa na kuendeleza diplomasia ya uchumi kwa lengo la kuvutia uwekezaji, kukuza ustawi wa pamoja na kuendeleza utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, hususan katika eneo la ushirikishwaji wa sekta binafsi.
 

Attachments

  • IMG-20261103-WA0071.jpg
    IMG-20261103-WA0071.jpg
    111.9 KB · Views: 2
  • IMG-20261103-WA0075.jpg
    IMG-20261103-WA0075.jpg
    136.4 KB · Views: 2
  • IMG-20261103-WA0072.jpg
    IMG-20261103-WA0072.jpg
    195.9 KB · Views: 2
  • IMG-20261103-WA0074.jpg
    IMG-20261103-WA0074.jpg
    232.3 KB · Views: 2
  • IMG-20261103-WA0070.jpg
    IMG-20261103-WA0070.jpg
    82.4 KB · Views: 2
  • IMG-20261103-WA0073.jpg
    IMG-20261103-WA0073.jpg
    242 KB · Views: 2
Back
Top Bottom