Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro, ameyahakikishia mataifa mbalimbali ulimwenguni kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, utafanyika kwa uhuru, uwazi na haki, kwa mujibu wa sheria mpya za uchaguzi za mwaka 2024.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika sherehe za miaka 79 ya Jamhuri ya Italia—tangu taifa hilo lianzishwe mwaka 1946 baada ya kuondoa utawala wa kifalme na kuweka mfumo wa kidemokrasia—Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa Tanzania ipo tayari kushirikiana na nchi yoyote duniani yenye nia ya dhati ya kusaidia kukuza demokrasia, siasa na masuala ya uchaguzi kupitia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Aidha, Dkt. Ndumbaro ameonya kuwa katika uchaguzi huo, Tanzania haitakubali kuingiliwa katika mipango yake ya uchaguzi, huku akiwahakikishia Watanzania kuwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu utafanyika kwa uhuru, uwazi na haki kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake, Balozi wa Italia nchini Tanzania, Giuseppe Sean Coppola, amesema nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha diplomasia baina ya mataifa hayo mawili, ili kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kitovu cha amani na shughuli za uwekezaji katika ukanda wa Afrika, licha ya changamoto za kiuchumi zinazosababishwa na siasa za kikanda.
Akizungumzia uchaguzi mkuu ujao, Coppola amesema kuwa Italia inatamani kuona Tanzania ikifanya uchaguzi wake kwa amani, huku ikizingatia misingi ya demokrasia, uwazi, haki na uhuru.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Diplomasia ya Uchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ulanga, amesema Italia imeendelea kuwa mdau muhimu wa uchumi wa Tanzania kupitia uwekezaji wake, hasa katika sekta ya utalii na huduma.
Sherehe hizo za miaka 79 ya Jamhuri ya Italia zilizofanyika usiku wa kuamkia leo pia ziliambatana na maadhimisho ya miaka 64 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Italia na Tanzania.