Tanzania yatajwa kwenye orodha ya nchi zitakazopigwa Ban kuingia Marekani mara tu Trump atakapoapishwa!

Tanzania yatajwa kwenye orodha ya nchi zitakazopigwa Ban kuingia Marekani mara tu Trump atakapoapishwa!

Tupe mfano wa hivyo vitu ambavyo tukivikosa Marekani hatuwezi kuvipata China au popote pale duniani.
ARV. Vile vidonge vya kufubaza makali ya Ukimwi na chanjo mbalimbali. Mtakufa Kama kuku. Huo ni mfano mmj katika mengi
 
Kwani bila wao kuna chochote unaweza mkuu?

Wanakupa ARV, chandarua, madawa na kuna baadhi ya vyoo vya primary vina logo yao kuwa wametusaidia

Wanakupa pesa ujenge hizi SGR

Wanakupa pesa za mikakati ya kuzuia na kupunguza umasikini, barabara, madaraja na vivuko

Kiufupi mkuu hakuna jambo lolote utafanya bila wao.
Marekani hawatoi pesa ya SGR, pesa za SGR ni partly za ndani na partly mkopo toka China Exim.

Pesa za ndani zilianza kuwa collected muda mrefu tu kupitia imports kodi inaitwa RDL, Rail way Development Levy.
 
Chadema bwana! Wanachekeeesha kweli kweli na mada zao mfu hizi. Wao Kila wakati wanawaza habari za matesovna matatizo tu ndo maana hata mwenyekiti wao hakuna anachoongeza kwenye uongozi mpaka Sasa zaidi ya kengeza tu.
 
Afu nyie ndo mnasema samia mbaya!! Nyie wenyewe Akili ya kujitegemea hamna😂😂😂 wasomi wa Bongo bhana.. kama wehu
 
Nimemkumbuka “Chuma” alipiga marufuku viongozi kwenda nje bila kibali cha ikulu. Hivi lilie zuio lilishaondolewa ama liliondoka na yeye?
 
Ungekuwa sio mvivu wa kusoma ungebaini kwamba hao jamaa wametumia reference ya travel ban list used when DT became a president for first time, so chances are the list is likely to be reapplied or not.
 
Sema watu mnapenda kuokoteza hio sio taarifa official ya serikali ni tafiti na prediction imefanywa
Actually sio kwamba wanaokoteza taarifa, ila tatizo lao ni kukosa comprehension skills, yaani wamesoma lakini hawajaweza kupata ufahamu wa walichokisoma.
 
ARV. Vile vidonge vya kufubaza makali ya Ukimwi na chanjo mbalimbali. Mtakufa Kama kuku. Huo ni mfano mmj katika mengi
ARV zinatengezwa nchi nyingi sana hata hapa Africa achilia mbali India na kwengineko.
 
Hujjui historia ya hii nchi

Tanzania ilipopata baa la njaa miaka ya 1970s to 1980s nchi gani ilikuja kuwasaidia?

Hamkuletewa UNGA WA DONOR kutoka Marekani kujiokoa na baa la njaa?

Mbona haya ni mambo mepesi sana mkuu kujielimisha
Unga wa" DONOR" ambao walimaanisha msaada tena kilikuwa kipindi cha utawala wa Kennedy Jr.
 
Afu nyie ndo mnasema samia mbaya!! Nyie wenyewe Akili ya kujitegemea hamna😂😂😂 wasomi wa Bongo bhana.. kama wehu

Huyo uliyomtaja hapo ana akili ya kujitegemea?

Kama anayo kwanini na yeye anaendaga Marekani na Ulaya kuomba misaada?
 
We are not americans.
Wakuu,

Nadhani kutokana na mambo yanayoendelea nchini image ya taifa imezidi kuchafuka.

Hivi karibuni nimekutana na listi ambayo inaonesha orodha ya nchi ambazo zinaweza kupigwa ban kuingia Marekani iwapo bwana Trump ataapishwa and yes Tanzania tumo.

List hiyo imetolewa na Cornel University, chuo kilichoanzishwa mwaka 1865 na katika bandiko lao wameonesha orodha ya nchi ambazo iwapo Trump ataingia basi kuingia Marekani itakuwa ni ndoto.

Katika orodha hiyo, Tanzania tumewekwa kwenye kundi moja na Kyrgyzstan, Nigeria, Myanmar, Sudan, Tanzania, Iran, Libya, North Korea, Syria, Venezuela, Yemen, and Somalia.

Hivi kweli leo sisi ni wa kuwekwa kwenye kundi moja na Myanmar, Sudan na North Korea?

Ile Royal Tour ilikuwa na kazi gani kama hata image ya nchi haijasafishika na mambo yako vile vile kama 2017?
 
Hakuna impact
 
Back
Top Bottom