Tanzania yatinga Robo fainali COSAFA

Tanzania yatinga Robo fainali COSAFA

Tukipona sana kwa South , ni 4-1 soka letu bado kabisa yaani hawajiamini watu wanamamiili makubwa kama huyo Maguri na Ulimwengu lakini bure kabisa
 
South africa hawatishi kivile, tutawafunga tu hata mbili
 
Ni baada ya kutoka sare ya bao 1- 1 na timu ya Mauritius huku Angola ambao
walikuwa wanafukuzana nao kwa karibu wakitoka sare ya bila kufungana na
Malawi. Mechi ya Robo fainali watakutana na SOUTH AFRICA. Kila laheri Vijana.
mwisho ushafika....
 
19511616_1538350179562255_7921010814408957517_n.jpg

Taifa Stars imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Cosafa 2017 licha ya kupata sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Mauritius kwenye mechi ya mwisho ya Kundi A mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Moruleng Stadium Afrika Kusini.

Stars imemaliza ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Kundi A ikiwa na pointi tano sawa na Angola (ambao walilazimishwa sare ya 0-0 na Malawi kwenye uwanja wa Royal Bafokeng) lakini Tanzania inasonga mbele kwa faida ya wastani wa magoli.
Hakika sasa timu yetu imeanza kutupa matumaini ya kulipenda soka la bongo.
 
tushafika ukingoni hapo haiwezekani timu mbovu ya mauritius tukatoa nayo sare
 
bora tungepeleka SERENGETI BOYS si kwa utumbo ule wanaotuonyeshna
watu hawajiamini hadi kwa Mauritio?
Kweli soka letu lina pepo dume, tutegemee muujiza kuifunga Azania
 
Magazetini

Malinzi haifikisha T. Stars robo fainali akiwa mahabusu
 
South africa hawatishi kivile, tutawafunga tu hata mbili
Labda walete kikosi cha pili, lakini wakikileta kilichoiua Nigeria kwao wala hatutoki. Tuache kujidanganya. Mauritius tu, ulimi nje.
 
Kwa mpira niliouona wakicheza dhidi ya Angola juzi, sina matumaini hata ya kupata sare na Bafanabafana.

Vv
Usemalo ni kweli kabisa, safari yetu katika michezo bado ni ndefu.

Kama taifa, kama kweli tunataka kuwa na timu itakayokuwa na upinzani huko mbele ya safari tunapaswa kuwekeza kwenye soka la vijana kama hawa Serengeti boys (waliotoka Gabon) na inapaswa kuwe na mpango hata kama ni wa kikanda wa hawa vijana kuwa na mechi nyingi kadiri iwezekanavyo (zikiwa za kimataifa haitakuwa mbaya ndani ya huu ukanda wetu) ili soka la taifa na hata ukanda huu likue, ila tukitegemea wakue waingie Vilabu vyetu hivi vya mtaa wa TWIGA na MSIMBAZI bado sidhani kama kutakuwa na unafuu wowote katika siku za karibuni.
 
Hapo ndio mtaona wanasiasa wanaanza kujiingiza kwenye team, mara harambee, mara ahadi za milungula kwa wachezaji wakiingia fainale
 
Back
Top Bottom