Tanzania yatoa tamko la muongozo kwa Watanzania waliopo Nchini Ukraine

Tanzania yatoa tamko la muongozo kwa Watanzania waliopo Nchini Ukraine

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
379
Reaction score
1,412
Serikali ya Tanzania imesema kuwa hakuna Mtanzania ambaye amepata madhara yoyote nchini Ukraine kutokana na taifa hilo kushambuliwa na majeshi ya Urusi, ambapo imewataka kuzingatia maelekezo kutoka kwa mamlaka za Ukraine.

Aidha, wametakiwa kuwasiliana na Ubalozi wa Tanzania Nchini Sweden ambao unawakilisha Ukraine kwa jambo lolote la dharura. Kwa wanafunzi wametakiwa kuzingatia muongozi kutoka kwenye vyuo wanavyosoma na wakubali utaratibu wa kuwarejesha itakapobidi.

Tamko hilo limetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

FMbeyaBWYCkzSLi.jpg
 
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imewataka watanzania walioko Ukraine kama wanafunzi, wafanyakazi na wafanyabiashara kuwa watulivu kipindi hiki cha mzozo wa Ukraine na Urusi

Wameshauriwa kufuata maelekezo yanayotolewa na Ukraine kwa raia, na wanafunzi kufuata maelekezo ya uongozi wa vyuo. Aidha wametakiwa kuendelea kuwasiliana na Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden kwa kuwa ndio unawakilisha Ukraine

Aidha serikali inaendelea kufuatilia hali za watanzania walioko huko lakini hadi sasa hakuna mtanzania aliyepata madhara yoyote.

Ukraine.JPG
 

Attachments

Badala wapeleke bombadia kuwaokoa watu wao, wanajiongelesha tu.
 
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imewataka watanzania walioko Ukraine kama wanafunzi, wafanyakazi na wafanyabiashara kuwa watulivu kipindi hiki cha mzozo wa Ukraine na Urusi

Wameshauriwa kufuata maelekezo yanayotolewa na Ukraine kwa raia, na wanafunzi kufuata maelekezo ya uongozi wa vyuo. Aidha wametakiwa kuendelea kuwasiliana na Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden kwa kuwa ndio unawakilisha Ukraine

Aidha serikali inaendelea kufuatilia hali za watanzania walioko huko lakini hadi sasa hakuna mtanzania aliyepata madhara yoyote

Kwamba wasikilize maelekezo ya serikali ya Ukraine na au vipi kuwasiliana na ubalozi Sweden?

What a joke?

Si bora wayasikie maneno ya wanaume wa shoka hawa?



Au hayo kama machungu mno si heri wakamsikiliza Putin mwenyewe?

Hiiiiii bagosha!
 
Mama anaendelea kuupiga mwingi, anakomesha Sukuma gang wote 😂…
Monalisa pambana peke yako mtoto wako atoke Ukraine, Rais wetu huku mtupu.
 
Wakati nchi za magharibi zinawambia raia wake waondoke sisi tulikuwa wapi.
 
What they are doing is underestimation of the situation on the ground, na madhara yakitokea watakuja hapa kusema ni bahati mbaya na blah blah kibao na hakuna kiongozi atawajibika kwa namna yoyote ile, hii ndo bongolala orijino nyingine ni photocopy.......
 
Hebu serikali lipien ndege ikachukue watu wenu maana kikianza kunuka haya ambayo mnaandika hayana ishu vuta picha adui anajibu mashambulizi analipua vituo mlivyo tenga kuficha watu si mnajua nguvu ya nyuklia lakini?
tatizo putin keshateka anga lote la ukraine. Kwasasa ndege ikijipitisha tu inaliwa kichwa. Sasa Tanzania nayo haitaki kula hasara ya ndege ambayo bado ni mpya kabisa hata mwaka hazijafikisha.
 
tatizo putin keshateka anga lote la ukraine. Kwasasa ndege ikijipitisha tu inaliwa kichwa. Sasa Tanzania nayo haitaki kula hasara ya ndege ambayo bado ni mpya kabisa hata mwaka hazijafikisha.
Hakika mkuu...ndege zinasafiri vipi kipindi cha vita?!!!

Putin kaizunguka Ukraine pande zote....wanafanya maskhara hao wanaoikosoa serikali yetu adhimu....
 
Putin analinda Aman luhansk na donesky ambako baado hata Vita yenyewe kuanza..hakuna kitisho kikuubwa..kyiev Pana Amani tele
 
tatizo putin keshateka anga lote la ukraine. Kwasasa ndege ikijipitisha tu inaliwa kichwa. Sasa Tanzania nayo haitaki kula hasara ya ndege ambayo bado ni mpya kabisa hata mwaka hazijafikisha.
Wakodi si kuna ubalozi huko wawasiliane nao
 
Hii nchi ina maajabu.

Wana chuo wako kwenye mahandaki

Simu zimeshazima chaji

Hawana pesa hawana chakula.

Hata wakati wa covid ilikuwa late late ikafikia watu kufungiwa.

What's kipau mbele it's expo trade.
 
Hebu serikali lipien ndege ikachukue watu wenu maana kikianza kunuka haya ambayo mnaandika hayana ishu vuta picha adui anajibu mashambulizi analipua vituo mlivyo tenga kuficha watu si mnajua nguvu ya nyuklia lakini?

Walipelekwa na serikali?
 
Back
Top Bottom