Tanzania Yazindua Kiwanda Kikubwa cha Vioo Afrika Mashariki na Kati

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

Tanzania Yazindua Kiwanda Kikubwa cha Vioo Afrika Mashariki na Kati

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) amesema uzinduzi wa kiwanda kikubwa cha vioo Afrika Mashariki na Kati ni hatua muhimu katika kuendeleza sekta ya viwanda nchini Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Septemba 20, 2023 Mkuranga, Pwani, Waziri Kijaji amesema uzinduzi wa Kiwanda hicho moja wapo wa viwanda vinne vya kutengeneza Vioo Barani Afrika ni ushindi mkubwa kwa Tanzania kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani nchini.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa na Kiwanda cha Sapphire chenye uwezo wa kuzalisha tani 400,000 za vioo kwa mwaka na
kinatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 1,650 na zisizo za moja kwa moja 6,000

Pia, amebainisha kuwa Kiwanda hicho kinatarajiwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na dolomite, silca sand, limestone, feldspar pamoja na magadi soda yanayopatikana Engaruka na kinatarajia kuuza bidhaa zake katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Serikali ya awamu ya sita ina dhamira ya dhati ya kuendeleza sekta ya viwanda nchini," alisema Waziri Kijaji. "Tutaendelea kutoa mazingira mazuri kwa wawekezaji ili waweze kuwekeza nchini Tanzania."​

Attachments

  • F6fr__BWsAAQ2VZ.jpg
    F6fr__BWsAAQ2VZ.jpg
    190.1 KB · Views: 4
  • F6fr__CXYAAuAnd.jpg
    F6fr__CXYAAuAnd.jpg
    305.6 KB · Views: 4
  • F6fr__CWMAEx8zV.jpg
    F6fr__CWMAEx8zV.jpg
    194.8 KB · Views: 4
  • F6fr__EWAAECXvh.jpg
    F6fr__EWAAECXvh.jpg
    166.5 KB · Views: 4

Tanzania Yazindua Kiwanda Kikubwa cha Vioo Afrika Mashariki na Kati

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) amesema uzinduzi wa kiwanda kikubwa cha vioo Afrika Mashariki na Kati ni hatua muhimu katika kuendeleza sekta ya viwanda nchini Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Septemba 20, 2023 Mkuranga, Pwani, Waziri Kijaji amesema uzinduzi wa Kiwanda hicho moja wapo wa viwanda vinne vya kutengeneza Vioo Barani Afrika ni ushindi mkubwa kwa Tanzania kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani nchini.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa na Kiwanda cha Sapphire chenye uwezo wa kuzalisha tani 400,000 za vioo kwa mwaka na
kinatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 1,650 na zisizo za moja kwa moja 6,000

Pia, amebainisha kuwa Kiwanda hicho kinatarajiwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na dolomite, silca sand, limestone, feldspar pamoja na magadi soda yanayopatikana Engaruka na kinatarajia kuuza bidhaa zake katika masoko ya ndani na nje ya nchi.

Serikali ya awamu ya sita ina dhamira ya dhati ya kuendeleza sekta ya viwanda nchini," alisema Waziri Kijaji. "Tutaendelea kutoa mazingira mazuri kwa wawekezaji ili waweze kuwekeza nchini Tanzania."​

Niliona hii habari
Hivi ndio viwanda tunavotaka sio ile awamu ya cherehani 3 ndio kiwanda [emoji23]
Wapinga serikali habar hizi hawazitak kabisa wao wanataka habari za kuibiwa tuh
 
haya mandeleo chadema hawataki kusikia ukitaka kuamini hawa watu ni hovyo
 
Back
Top Bottom