Tanzania yazindua rasmi Ubalozi wake Jijini Algiers, Algeria

Tanzania yazindua rasmi Ubalozi wake Jijini Algiers, Algeria

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Serikali ya Tanzania imezindua rasmi ubalozi wake jijini Algiers, Algeria.

Ufunguzi huo umefanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax na kuhudhuriwa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Algeria, Ahmed Attaf, Balozi wa kwanza wa Algeria kuhudumu nchini Tanzania, Noureddine Djoudi na Jumuiya ya Wanadiplomasia nchini Algeria.

Kiwango cha ubadilishaji wa biashara kati ya Tanzania na Algeria ni cha chini ikilinganishwa na fursa nyingi zilizopo. Algeria yenye eneo lake la kimkakati na uchumi inatoa fursa kubwa kwa biashara za Tanzania.

Akihutubia kwenye ufunguzi wa ubalozi huo Waziri Tax ameeleza kuwa Tanzania na Algeria zimejizatiti kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kwa lengo la kukuza ushirikiano wenye maslahi kupitia sekta za kipaumbele kama vile sekta za kilimo, madini, utalii, mafuta na gesi, vifaa tiba, viwanda, nishati pamoja uchumi wa buluu.

Naye Attaf ameeleza kuwa ziara ya Waziri Tax imekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa wamepata fursa ya kuzungumza masuala ya ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji na sekta nyingine muhimu kwa maendeleo ya mataifa hayo mawili.

“Balozi zinafaa kuendelea kuwa madaraja ya muhimu kati ya watu, nchi na mataifa. Balozi zetu zinawajibika na kukuza, kuimarisha ushirikiano na uhusiano kati ya nchi na nchi ili kuleta tija zaidi na kuziwezesha nchi zetu kunufaika kiuchumi,’’ amesema Attaf.

Uhusiano kati ya Algeria na Tanzania uliasisiwa mwaka 1963 mara baada ya uhuru wa Tanganyika. Tangu wakati huo nchi hizi zimeendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa maslahi ya pande zote. Vilevile katika kuimarisha ushirikiano huo Tanzania imefanya ufunguzi wa ubalozi wake nchini Algeria ambao ulianza kutekeleza majukumu yake tangu mwaka 2017.

Chanzo: Habari leo

====

Nawakumbusha tuu Tanzania Sasa ina Ubalozi wa Kudumu Mjini Algers Nchini Algeria kwa Waarabu.

Haya Watanganyika Njooni mtoe mapovu mengine.
 
Algeria ni dada wa Tanzania. Nchi mbili kongwe Africa ambazo zilishikana pamoja bega kwa bega kusaidia mataifa ya afrika kupata uhuru.

Kipindi cha uhuru Tanganyika, na baada ya uhuru, Tanganyika (Viz Mwalim Nyerere) na Algeria walikua wakifanya vikao vya siri vya kijeshi na kimapinduzi kusaidia nchi za Afrika zote ambazo zilizokua bado zinatawaliwa kikoloni.

Vikao viliendelea kwa siri miongo kadhaa na wakaweka "KAMBI (BASE)" za kijeshi mbili, moja kambi ya kijeshi ikawekwa Tanganyika pale Bagamoyo (Baadae zikaongezwa Morogoro, Kongwa n.k) na nyingine ziliwekwa Algeria. Ambazo zilikua zikiwafua na kuwanoa kisawasawa wanajeshi kisiri wanaotaka kupigania Uhuru katika nchi zao Afrika.

Mwalimu alikua akipeleka Algeria wanajeshi wa Tanganyika, Mozambique, South Africa, Angola, Congo kwenda kupewa mafunzo ya kijeshi. Walikua wanatoka katika nchi zao kisiri na kuja kuweka kambi kwa muda Tanganyika na kisha kuelekea Algeria kwa awamu.

Baada ya Cuba kufanya mapinduzi ya kijeshi kupitia kwa Kamanda Fidel Castro na Ernesto Guevara De La Serna (Che Guevara), Cuba wakaungana pamoja na Tanganyika na Algeria kutoa mafunzo ya kijeshi ili kusaidia baadhi ya nchi za Afrika zilizokua zikitawaliwa kimabavu, moja wapo ilikua Congo, kusaidia watu kufanya mapinduzi ya kijeshi, kudai uhuru na kui
kimbiza Ufalme Wa Belgium uliokua ukitawala kwa mabavu.

Che Guevara alitua tanganyika na kuwafua wanajeshi wa tanganyika na congo, na kisha kuelekea congo msituni kuwanoa zaidi wanajeshi kwenye swala la vita za msituni.

Baadhi ya wakoloni baada ya kuona vuguvugu hilo, waliamua kuwapa uhuru baadhi ya mataifa ya Afrika bila mapinduzi wala kumwagika kwa damu.

Algeria na Tanganyika wana historia nzuri na ndefu sana, Afrika nzima hakuna mataifa yenye historia nzuri na kusisimua kama mataifa haya mawili!!!

#Kwanza Ni Jambo La Aibu Sana Tanzania Kufungua Ubalozi Wa Kudumu Algeria Mwaka 2023. Ilitakiwa Kufunguliwa Miaka Ya 60 au 70 huko!
 
Algeria ni dada wa Tanzania. Nchi mbili kongwe Africa ambazo zilishikana pamoja bega kwa bega kusaidia mataifa ya afrika kupata uhuru.

Kipindi cha uhuru Tanganyika, na baada ya uhuru, Tanganyika (Viz Mwalim Nyerere) na Algeria walikua wakifanya vikao vya siri vya mapinduzi kusaidia nchi za Afrika zilizokua bado zinatawaliwa kikoloni.

Wakaweka KAMBI (BASE) za kijeshi mbili, moja Tanganyika pale Bagamoyo na nyingine Algeria.
Namkumbuka Ahmed Ben Bella alikuwa mmoja wa mashujaa wa Africa
 
Watuuzie mafuta basi


 
Uliwahi waona wanaojiita Waburushi? Wako kwenye Jumuiya ya Waarabu na hata WB inawatambua kama sehemu tofauti na huku Kwa SubSaharan Africa.

Kama Algeria ni Waburushi wa Oman na Iran watajiitaje?
Kws sasa wanakimbilia Ulaya!
 
Kama wewe ulivyo nguruwe jike
Overview. In terms of market size, Algeria has the tenth-largest proven natural gas reserves globally, is the world's fourth-largest gas exporter, and has the world's third-largest untapped shale gas resources. It also ranks sixteenth in proven oil reserves and exports roughly sixty percent of its total production.
*
*
*
*
*
Along with gas, Algeria is a large oil producer with 12.2 billion barrels of proven oil reserves. The country exports 540,000 b/d of its total production of about 1.1 million b/d.



Bado unabisha wewe sio Ng'ombe???
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezindua rasmi Ubalozi wake Jijini Algiers, Algeria.

Ufunguzi huo umefanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Stergomena Tax na kuhudhuriwa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Algeria, Ahmed Attaf, Balozi wa kwanza wa Algeria kuhudumu Nchini Tanzania, Balozi Noureddine Djoudi na Jumuiya ya Wanadiplomasia nchini Algeria.
e1e017f7-e35d-4c44-8fe4-fc6dc169183e.jpg

Kiwango cha ubadilishaji wa biashara kati ya Tanzania na Algeria ni cha chini ikilinganishwa na fursa nyingi zilizopo. Algeria yenye eneo lake la kimkakati na uchumi inatoa fursa kubwa kwa biashara za Tanzania.

Akihutubia kwenye ufunguzi wa Ubalozi huo Waziri Tax ameeleza kuwa Tanzania na Algeria zimejidhatiti kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kwa lengo la kukuza ushirikiano wenye maslahi kupitia sekta za kipaumbele kama vile sekta za kilimo, madini, utalii, mafuta na gesi, vifaa tiba, viwanda, nishati pamoja uchumi wa buluu.

“Ni imani yangu kuwa uzinduzi wa ubalozi huu ni ishara ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria na kutakuza na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina ya mataifa yetu…..

“Katika Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Algeria tulikubaliana kuhusu maeneo ya kipaumbele kwa manufaa ya pande zote mbili na tulisaini Hati nane (8) za Makubaliano ya Ushirikiano katika maeneo ya mafuta na gesi, nishati, elimu, kumbukumbu na nyaraka, uhusiano wa kidiplomasia.
50807357-2ebd-4cb0-9e97-4468667f8c2b.jpg

“Aidha, pamoja na kusainiwa kwa hati hizo za makubaliano, pia tulikubaliana kutoa kipaumbele katika sekta za mafuta na gesi, nishati, kilimo, dawa pamoja na masuala ya amani na usalama.”

Naye Attaf ameeleza kuwa ziara ya Waziri Tax imekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa wamepata fursa ya kuzungumza masuala ya ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji na sekta nyingine muhimu kwa maendeleo ya mataifa hayo mawili.

“Balozi zinafaa kuendelea kuwa madaraja ya muhimu kati ya watu, nchi na mataifa. Balozi zetu zinawajibika na kukuza, kuimarisha ushirikiano na mahusiano kati ya nchi na nchi ili kuleta tija zaidi na kuziwezesha nchi zetu kunufaika kiuchumi,” amesema Attaf.
ac60235e-8ce6-4b2b-a8b7-3dfeb8d67f0c.jpg

Ufunguzi wa Ubalozi umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Algeria ambao umemalizika kwa mafanikio na kuwezesha kusainiwa kwa Hati 8 za Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta za nishati, mafuta na gesi, elimu na teknolojia, mafunzo ya diplomasia, kumbukumbu na nyaraka, ulinzi na usalama, ushirikiano wa kidiplomasia, kilimo na afya.
d3ed5458-403f-43e8-9921-d304941d5343.jpg

Uhusiano kati ya Algeria na Tanzania uliasisiwa mwaka 1963 mara baada ya uhuru wa Tanganyika. Tangu wakati huo nchi hizi zimeendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa maslahi ya pande zote. Vilevile katika kuimarisha ushirikiano huo Tanzania imefanya ufunguzi wa Ubalozi wake nchini Algeria ambao ulianza kutekeleza majukumu yake tangu mwaka 2017.

Viongozi wengine waliohudhuria ufunguzi huo ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, Naibu Makatibu Wakuu kutoka Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia, Nishati na Mambo ya Ndani ya Nchi.
 
Back
Top Bottom