SoC04 Tanzania yenye ajira ya kutosha inawezekana

Tanzania Tuitakayo competition threads

hauleibrahim

Senior Member
Joined
May 17, 2024
Posts
183
Reaction score
125
Tanzania inaweza kumaliza tatizo la ukosefu wa ajira Kwa asilimia mia Kwa wasomi mpka wasio wasomi.
Vitu vifuatavyo vinaweza badili Tanzania iwe ni soko la ajira milele.

Uvuvi.mikoa yote yenye bahari,maziwa Kwa wale vijana wanao penda uvuvi na wanao somea uvuvi wapewe elimu na vifaa vya kisasa wafanye uvivu wa kisasa huko huko makwao kwenye hizo fulsa za uvuvi.

Kilimo: serikali iwekeze upatikanaji wa pembejeo Kwa ubora vijijini hasa Kwa wakulima waliopo kule kulinda ukosefu wa ajira Kwa vijana vijijini mashamba yapo mengi ni kupatikana viwatilifu makini pamoja na elimu sahihi sekta ya kilimo itaajili vijana wengi wasomi na wasio wasomi mikoani bila kuja dar au mijini kuhangaikia ajira Kwa wasomi.

Ufugaji: serikali itoe elimu ya ufugaji wa kisasa vijijini hasa Kwa mikoa inayo fuga ng'ombe mbuzi nguruwe n.k elimu ya ufugaji wa kisasa ili tupate nyama nyingi ZeNye ubora wa kulika na kuuzika nje ya nchi

Pia serikali ijenge masoko ya hivyo vitu kila wilaya ili kupunguza wingi wa ajira kwenye eneo moja na kukosa riziki Kwa watu badala take kila kitu kiwe na soko lake humo humo vijijini

Vitu vingine vitakavyo maliza tatizo la ajira nchini ni hivi. Yawepo masoko kila wilaya masoko hayo yajitegeme mfano. Masoko ya nafaka yawe ya nafaka tu kusiwepo na muingiliano wa kila bidhaa soko mojo.

Ziwepo machinjio kila wilaya: sio lazima ziwe machinjio kubwa ila ndogo tu ZeNye miundombinu rafiki ya kuchakata nyama Kwa haraka na kutunza ngozi vizuri. Hii isasaidia wale vijana wasio penda kilimo uvuvi kupata ajira humo za kuchinja n.k machinjio hizi zisiwe na mlundikano wa kila aina ya wanyama wafugwao kuchinjwa mle ila kila eneo maalum litengwe Kwa machinjio ya wanyama husika Kwa hiyo mlaji atafuata nyama eneo husika Kwa anacho kihitaji hii itaongeza ajira na ushindani wa kuuzwa nyama Bora.

Yawepo masoko kila wilaya ila sio lazima yawe makubwa tunaweza Jenga masoko mfano wa lile la ilala na karume Kwa kila wilaya ili kuwapa fulsa vijana wanao tamani kufanya kazi humo na kujiajiri humo badala ya kutegemea vijana wa mikoani kukimbilia dar wakiamini ndiko kwenye soko na maisha mazuri.

Serikali iyafanye hayo Kwa weledi changamoto ya ajira Kwa miaka kumi mpka 20 itakuwa ni stori sio Tena la kugombana kama ilivyo Sasa hivi.

Lengo langu kugawanya masoko ya bidhaa kuto kuwa na bidhaa nyingi za aina moja ni kuhakikisha fulsa zinakuwa nyingi na kila mtu anapata mahali pa kuweza kutafuta kipato ila pia kugawanya ule mgawanyiko wa fedha bodaboda apate pesa dalaldala apate pesa Kwa vijana pia watakao kuwa wamejiajiri humo wapate

Masoko ya bidhaaa yakiwa mbali mbali ni fulsa hata Kwa vijana wabeba mizigo kila eneo kupata mkate wao bila kugombana gombana na wenzake sababu mle kazi hizo zitakuwa nyingi kila siku.

Tanzania bila ukosefu wa ajira inawezekana tukiamua Kwa pamoja na serikali kuwekeza nguvu katika haya mambo.
 
Upvote 1
Pia serikali ijenge masoko ya hivyo vitu kila wilaya ili kupunguza wingi wa ajira kwenye eneo moja na kukosa riziki Kwa watu badala take kila kitu kiwe na soko lake humo humo vijijini

Vitu vingine vitakavyo maliza tatizo la ajira nchini ni hivi. Yawepo masoko kila wilaya masoko hayo yajitegeme mfano. Masoko ya nafaka yawe ya nafaka tu kusiwepo na muingiliano wa kila bidhaa soko mojo.
Hii sehemu ninataka niibold kabisa.

Halafu kwa kuwa bidhaa huzalishwa kwa wingi na kufurika katika soko la sehemu moja wakati sehemu nyingine ina uhaba. Tunahitaji miundombinu inayofanya soko la mtu kuwa ni nchi nzima. Mfano posta ikichukua jukumu la kusambaza vifurushi na magunia nchi nzima. Soko litatengemaa sana.

Tanzania bila ukosefu wa ajira inawezekana tukiamua Kwa pamoja na serikali kuwekeza nguvu katika haya mambo.
Hakika bro soko, soko, soko.

Soko la kijiji kizima wilaya nzima nchi nzima na dunia nzima.
Soko linalolipa thamani halisi ya jasho la mzalishaji.
Maana kuvutia uzalishaji wa kitu fulani wala huhitaji fizikia za vifurushi (quantum physics) unahitaji tu kuliweka soko imara.
Mfano seremala akiaccess soko linalonunua fanicha_sofa lake kwa mamilioni (mbona ya nje tunanunua?)
Ebhana umelenga penyewe kabisa. Ahsante👊
 
Hii sehemu ninataka niibold kabisa.

Halafu kwa kuwa bidhaa huzalishwa kwa wingi na kufurika katika soko la sehemu moja wakati sehemu nyingine ina uhaba. Tunahitaji miundombinu inayofanya soko la mtu kuwa ni nchi nzima. Mfano posta ikichukua jukumu la kusambaza vifurushi na magunia nchi nzima. Soko litatengemaa sana.

Hakika bro soko, soko, soko.

Soko la kijiji kizima wilaya nzima nchi nzima na dunia nzima.
Soko linalolipa thamani halisi ya jasho la mzalishaji.
Maana kuvutia uzalishaji wa kitu fulani wala hujitaji fizikia za vifurushi (quantum physics) unahitaji tu kiweka soko imara.
Mfano seremala akiaccess soko linalonunua fanicha_sofa lake kwa mamilioni (mbona ya nje tunanunua?)
Ebhana umelenga penyewe kabisa. Ahsante👊
Shukrani sana
 
Mkuu hapa umefanya oversimplification ingawa Imani yangu ndio ni kweli kunaweza kukawa na ujira kwa kila raia lakini sio kama ulivyosema wewe kinachotakiwa kufanyika ni completely overhaul na mifumo yote itegemeane sustainably...

Unaposema uvuvi (kutokana na kwamba demand ni kubwa zaidi mbali na ziwani kuliko pengine kule pengine bei itakuwa kubwa kuliko huku) hivyo muendelezo wa walanguzi / traders ni lazima na hawa ndio wanapata pesa kuliko wanaoingia ziwani...; Pia issue sio kwamba watu hawapendi samaki bali hawana disposable income ya kumudu hivyo vitu.... Vilevile kwenye kilimo same story sio kwamba watu hawana njaa wala hawapendi kula bali kila wanachotoa mara nyingi hakikidhi anayeuza....

Kwahio kwa ufupi wazalishaji wanazalisha na watazalisha kulingana na wanunuzi na wanunuzi watanunua kama wana disposable income na disposable income itapatikana kama watu watapata ajira / shughuli zenye ujira na hilo litafanikiwa tu kama kila need itaweza kwa sustained kwa kumuwezesha mtoa need kujipatia mahitaji yake ya basic need...

Isssue sio kazi tu ili mradi mtu apate cha kufanya bali kazi itakayomuwezesha mtu kupata income ya mahitaji yake muhimu (needs) na disposable income ya luxuries....
 
Ndio maana tunatamani kila mzalishaji aweze kulifikia soko linalomlipa thamani halisi ya jasho lake. Na kila mnunuzi ajipatie bidhaa na huduma atakayojipatia thamani halisi ya sarafu yake.

Exactly, sio kazi tu alimuradi. Hapa tunazungumzia kazi halisi zinazotokeza huduma na bidhaa. Mfano: sio upiga debe au udalali hao wote wakose kazi wakazalishe chochote maana udalali na upigadebe umeuliwa na mifumo imara ya masoko, mteja anamuona muuzaji kirahisi.

Utashangaa ghafla kila mmoja atakimbilia kujificha kuzalisha na kusambaza hitaji fulani la watu na mwisho wa siku wote tutatumikiana na kila mmoja atauza (SOKO) kwa thamani nzuei itakayomruhusu kuwa mnunuzi pia
 
What is true value of a product ? In this day and age huenda sio a better product inayouza bali better salespersons ndio wanauza....

Bila kufanya mfumo mzima sustainable haiwezekaniki system kuwa stable..., na sababu ya automation na nguvu kazi kutokuwa na maana kama zamani wahitaji wa ajira ni wengi hence ujira wanaopata / watakaopata ni mdogo
Exactly, sio kazi tu alimuradi. Hapa tunazungumzia kazi halisi zinazotokeza huduma na bidhaa. Mfano: sio upiga debe au udalali hao wote wakose kazi wakazalishe chochote maana udalali na upigadebe umeuliwa na mifumo imara ya masoko, mteja anamuona muuzaji kirahisi.
Ndio hao madalali ndio angalau wanafanya kijijini angalau bibi wenye gunia moja aweze kuuza sababu wanakusanya kila nyumba kidogo kidogo na kutafuta magari ya kupeleka mijini bila hivyo gunia za huyu bibi zingemuozea
Utashangaa ghafla kila mmoja atakimbilia kujificha kuzalisha na kusambaza hitaji fulani la watu na mwisho wa siku wote tutatumikiana na kila mmoja atauza (SOKO) kwa thamani nzuei itakayomruhusu kuwa mnunuzi pia
Hio information ya nini kizalishwe na wapi na wakati gani inatoka wapi au ndio yale mwaka huu vitunguu vimelipa mwaka kesho kila mtu analima vitunguu hence watu kupata hasara na mwaka keshokutwa kuacha kulima...., Hili suala nilishaelezea hapa kwa mfumo wa riwaya ambapo nimeweka the only way theoretically ya kuhakikisha community inakuwa sustainable...
 
Mkuu hapa umefanya oversimplification ingawa Imani yangu ndio ni kweli kunaweza kukawa na ujira kwa kila raia lakini sio kama ulivyosema wewe kinachotakiwa kufanyika ni completely overhaul na mifumo yote itegemeane sustainably...

Unaposema uvuvi (kutokana na kwamba demand ni kubwa zaidi mbali na ziwani kuliko pengine kule pengine bei itakuwa kubwa kuliko huku) hivyo muendelezo wa walanguzi / traders ni lazima na hawa ndio wanapata pesa kuliko wanaoingia ziwani...; Pia issue sio kwamba watu hawapendi samaki bali hawana disposable income ya kumudu hivyo vitu.... Vilevile kwenye kilimo same story sio kwamba watu hawana njaa wala hawapendi kula bali kila wanachotoa mara nyingi hakikidhi anayeuza....

Kwahio kwa ufupi wazalishaji wanazalisha na watazalisha kulingana na wanunuzi na wanunuzi watanunua kama wana disposable income na disposable income itapatikana kama watu watapata ajira / shughuli zenye ujira na hilo litafanikiwa tu kama kila need itaweza kwa sustained kwa kumuwezesha mtoa need kujipatia mahitaji yake ya basic need...

Isssue sio kazi tu ili mradi mtu apate cha kufanya bali kazi itakayomuwezesha mtu kupata income ya mahitaji yake muhimu (needs) na disposable income ya luxuries....
Kwa upande wa income itapatikana Kwa kila mtu naimani na hiyo sababu income niliyo lenga sio mtu aingize laki hata Kwa siku no ukiingiza elfu 20 au 15 ni nzuri kuhusu walanguzi hiyo Sasa n ishu ya serikali kuweka mifumo rafiki na Bora madalali wapo Kwa sababu n ishu ya mnyororo wa thamani kila mtu ana deal na anapoweza yeye kufanya na kuona anapata faida kubwa .ishu sio Bora kazi naungana nawe ila kila kitu tukubali kuanza kwanza mengine yatarekebishwa ndani tukiona changamoto kuliko tukitaka tungoje vitu viwe sahihi vyote hatuto maliza hili tatizo la ajira milele

Kuna muda vitu hurebishwa ukiwa ndani ya kitu chenyewe vile unaona changamoto za wahusika wakuu zinavyo tokea
 
Kwa upande wa income itapatikana Kwa kila mtu sababu income niliyo lenga sio mtu iungize laki hata Kwa siku ukiingiza elfu 20 au 15
issue sio kuingiza ngapi unaweza ukaingiza laki mbili isitoshe matumizi yaliyokuzunguka au ukapata tshs 5 ikatosha na kubaki baada ya matumizi yaliyokuzunguka..., kinachohitajika ni bottom up approach tuanzie kwenye needs zote ziwe affordable baada ya hapo wants kila mtu atajichotea kulingana na disposable income atakayokuwa nayo...

In short we need to have a large percentage of middle incomes sio have nots wengi kama tunapoelekea
 
Mkuu hapa umefanya oversimplification ingawa Imani yangu ndio ni kweli kunaweza kukawa na ujira kwa kila raia lakini sio kama ulivyosema wewe kinachotakiwa kufanyika ni completely overhaul na mifumo yote itegemeane sustainably...

Unaposema uvuvi (kutokana na kwamba demand ni kubwa zaidi mbali na ziwani kuliko pengine kule pengine bei itakuwa kubwa kuliko huku) hivyo muendelezo wa walanguzi / traders ni lazima na hawa ndio wanapata pesa kuliko wanaoingia ziwani...; Pia issue sio kwamba watu hawapendi samaki bali hawana disposable income ya kumudu hivyo vitu.... Vilevile kwenye kilimo same story sio kwamba watu hawana njaa wala hawapendi kula bali kila wanachotoa mara nyingi hakikidhi anayeuza....

Kwahio kwa ufupi wazalishaji wanazalisha na watazalisha kulingana na wanunuzi na wanunuzi watanunua kama wana disposable income na disposable income itapatikana kama watu watapata ajira / shughuli zenye ujira na hilo litafanikiwa tu kama kila need itaweza kwa sustained kwa kumuwezesha mtoa need kujipatia mahitaji yake ya basic need...

Isssue sio kazi tu ili mradi mtu apate cha kufanya bali kazi itakayomuwezesha mtu kupata income ya mahitaji yake muhimu (needs) na disposable income ya luxuries....
Ishu ya mifumo n vizuri tuhagaikie tukiwa tumeanza kuliko hatujaanza tunahangaika na mifumo ni rahisi kupoteza vyote hata hizo mbinu za kutengeneza ajira.hali iliyopo Kwa tz ukigusa mifumo unawagusa Hadi watu wenye hiyo mifumo na wengine wako n pesa mingi kuharibu wazo lako so watapambana wakwamishe jambo lako rejea ishu ya hussen bashe na BBT watu wa mazingira walimfuata kuwa plan ya mashamba ataharibu mazingira ingawa wanajua inaenda kuwapa vijana ajira ndo mana mm nasema mifumo tutaenda nayo taratibu ila vizuri jambo lianze kwanza.mifumo haitolewi ndani ya siku moja tu ni process.
 
Hadi Sasa hainingii akilini kiloyanyama inauzwa elfu Kumi?

inamaana hadi kufuga tumeshindwa?
 
Ishu ya mifumo n vizuri tuhamgaike tukiwa tumeanza kuliko hatujaanza tunahangaika na mifumo ni rahisi kupoteza vyote hata hizo ajira.ahida iliyopo Kwa tz ukigusa mifumo unawagusa Hadi watu wenye hiyo mifumo so watapambana wakwamishe jambo lako rejea ishu ya hussen bashe na BBT watu wa mazingira walimfuata kuwa plan ya mashamba ataharibu mazingira so ndo mana mm nasema mifumo tutaenda nayo taratibu ila vizuri jambo lianze kwanza
Hata issue ya Hussein Bashe was non starter sababu aliangalia uzalishaji bila masoko (hivyo vinategemeana) tena kweli angetaka ku make a difference huenda bora angewapelekea / angewaongezea wakulima tayari ambao wapo field na sio kuwatoa watu kitaa (kilimo ni way of life) kwahio point yangu bila kutiki box zote jambo halitakuwa sustainable..., ndio maana nimekwambia ukiwa na muda pitia hii riwaya imejaribu kugusa the whole system ili kufanya kazi as a unit na sio kufanya kwa mafungu... (things are interlinked)

Hadi Sasa hainingii akilini kiloyanyama inauzwa elfu Kumi?

inamaana hadi kufuga tumeshindwa?
Kwani unit cost ya kumlisha mpaka kumfikisha mezani huyo ng'ombe / nyama inacost kiasi gani ? unaweza kuona kwamba mara zote unapoponua kwa elfu tano huenda kuna mtu analiwa / anaumia ambaye huenda ni mfugaji...

Kwahio cha kuangalia ni kwamba watu hawana pesa ya kununua nyama au kupata mahitaji yao na sio kilo ya nyama ku cost elfu kumi...

Kuna kipindi England maziwa yalikuwa mengi kuliko soko wakulima waliyamwaga badala ya kuyauza sababu soko bei ilishuka kuliko uendeshaji hivyo wakaona ni bora to create demand....
 
kwahio nisawa kuahivyo mkuu
 
Hadi Sasa hainingii akilini kiloyanyama inauzwa elfu Kumi?

inamaana hadi kufuga tumeshindwa?
Kufuga tumeshindwa ndio jibu sahihi na pia ufugaji hata wa kawaida n ufugaji usioweza kunpekeka mtoto st agre high school
 
Tunaenda sawa
issue sio kuingiza ngapi unaweza ukaingiza laki mbili isitoshe matumizi yaliyokuzunguka au ukapata tshs 5 ikatosha na kubaki baada ya matumizi yaliyokuzunguka..., kinachohitajika ni bottom up approach tuanzie kwenye needs zote ziwe affordable baada ya hapo wants kila mtu atajichotea kulingana na disposable income atakayokuwa nayo...

In short we need to have a large percentage of middle incomes sio have nots wengi kama tunapoelekea
Unarudi nyuma unaenda mbele Naona nimeshindwa kukuelewa point yako kuu ni Nini Kuna hoja uliweka awali nimekujibu naona umekuja Tena na we kujibu kile kile changu ssa nashindwa kuelewa ukiulizia swali la nn Sasa sielewi wwe main point yako haswa hpo kwenye mjadala ebu nenda straight on point nijue nakujibuje
 
Hata issue ya Hussein Bashe was non starter sababu aliangalia uzalishaji bila masoko (hivyo vinategemeana) tena kweli angetaka ku make a difference huenda bora angewapelekea / angewaongezea wakulima tayari ambao wapo field na sio kuwatoa watu kitaa (kilimo ni way of life) kwahio point yangu bila kutiki box zote jambo halitakuwa sustainable..., ndio maana nimekwambia ukiwa na muda pitia hii riwaya imejaribu kugusa the whole system ili kufanya kazi as a unit na sio kufanya kwa mafungu... (things are interlinked)

Kwa hiyo unasema asinge chukua vijana ehe alafu tunalitatiaje tatzo Kwa kumnyima fulsa na kwenda kumpa idea bibi yangu Alie choka alime kisasa azalishe ajira Kwa umri uliosongo.ishu ya masoko Kwa maelezo yake IPO na hata kama umepata kumsikiliza yye mwenyew anajua changamoto ya mkulima wa Tanzania ni soko elimu Bora uya kilimo na pembejeo hoja yako naona ulivyotaka www inaweza kuwa sahihi Kwa muono wako swali inatatuaje tatizo la ukosefu wa ajira impact ya bashe mm nimeielewe tukifanikiwa Kwa vijana taifa limefanikiwa Kwa pamoja pia kijana ataleta ajira Kwa wengine kwenye kilimo hiko hiko mpka sehemu nyingine ssa unapotaka wew angewafikia hao una uhakika tunge tatua tatzo la ajira kama ndio njpe mchoro kidogo Kwa itakavyo kuwa nikuelewe nami.alafu huo mchoro uwe wa miaka 5 mpka kumi bila kuleta malalamiko ya ukosefu wa ajira Kwa no kubwa ya vijana walioko mashuleni.
Kwa kusaidia Kuna waliotoka kitaa ni wakulima kabisa familia zao so hivyo IPO upande ulio taka www na sifa za maombi ilikuwa uwe mkulima so ningemu Kwa asie mkulima kama mtu wa dar jumshikisha tope au mchanga ama jembe n mbegu apate mafunzo
 
Hadi Sasa hainingii akilini kiloyanyama inauzwa elfu Kumi?

inamaana hadi kufuga tumeshindwa?
Katika Beef Production USA ni among the top....

Lakini nimecheki hapa prices average za beef in USA in 2024

Wholesale prices​

In 2024, the approximate wholesale price range for US beef is between US$ 7.04 and US$ 15.88 per kilogram or between US$ 3.19 and US$ 7.20 per pound(lb).

Thus utakubaliana point yangu issue sio kitu kinauzwa bei gani bali issue ni affordability ya hicho kitu kwa wananchi.., sio kwamba wabongo hatupendi korosho au hatuna korosho bali hatuna pesa za kula hizo korosho...
 
Nakubaliana nawe.ila pesa bila kujitafuta ww Kwa kuuza unavipateje uza upate pesa ukanunue nawe kanuni rahisi.marehemu alikuwa anasema tufanye kazi.tukifnya kazi tutapata pesa hata kama sio nyingi ila haitotushinda kununua korosho ssa hufanyi kazi lazima ukose pesa ya korosho Kuna wakati ili umiliki pesa tunasema uza bidhaa yenye uhitaji kama uonavyo mapenzi kwenye mziki ndio bidhaa inayo hitajika sokoni na ndio yenye kukupa fedha ikiwa n Bora kuiandaa na kutafuta walaji
 
Hii sehemu ninataka niibold kabisa.

Halafu kwa kuwa bidhaa huzalishwa kwa wingi na kufurika katika soko la sehemu moja wakati sehemu nyingine ina uhaba. Tunahitaji miundombinu inayofanya soko la mtu kuwa ni nchi nzima. Mfano posta ikichukua jukumu la kusambaza vifurushi na magunia nchi nzima. Soko litatengemaa sana.

Hakika bro soko, soko, soko.

Soko la kijiji kizima wilaya nzima nchi nzima na dunia nzima.
Soko linalolipa thamani halisi ya jasho la mzalishaji.
Maana kuvutia uzalishaji wa kitu fulani wala huhitaji fizikia za vifurushi (quantum physics) unahitaji tu kuliweka soko imara.
Mfano seremala akiaccess soko linalonunua fanicha_sofa lake kwa mamilioni (mbona ya nje tunanunua?)
Ebhana umelenga penyewe kabisa. Ahsante👊
Soko likiwepo hata muuzaji anakuwa huru anajua soko lipo nitaenda kuuza muhimu ni kujali uzalishaji wa bidhaa Bora pia itapunguza madalali mana wengi wa wakulima mazao huuza Kwa madalali wanao leta mijini huku wao wakiwa hawapati pesa nyingi kama dalali so masoko ya kiwepo itafika hatua matajiri watakuja wao wenyewe wakijua mzigo mwingi sehemu ndogo ya Kijiji wanaupata Kwa urahisi tofauti na sasa ukitaka Tani ya maharage mfano Tani elfu moja unaweza zunguka Kijiji kizima hata Tani moja isifike hali hiyo huwavunja nguvu matajiri wenye uhitaji.mfno angalia mo anachukua ngano kutoka nje ndani ngano yetu haijitoshelezi kabisa na mnunuzi tunae hapa hapa japo zamani alikuwa anunua nje ila awamu hii bashe kawalegezea masharti na kumwambia nunueni ngano ya humu humu ndani swali linakuja tuna ngano ya kutosha kumuzia mo na azam hapo ndo wakulima hupishana na fulsa sababu sisi wakulima tuna vilimo vya kizamani ekari mbili moja robo ekari.wkati wenzetu duniani mkulima mdogo humtazama kama mtu anae miliki ekari 50 za Shamba huyo ndio mkulima mdogo wa chini kabisa.bado tuna haki ya kufanya kilimo biashara kuwafunza vijana haswa kuleta mapinduzi ya soko na uzalishaji wa kukizi soko kama la mo na azam Kwa umoja wao pamoja nala nje ya tz
 
Back
Top Bottom