Tanzania yenye Amani bila Uonevu

Tanzania yenye Amani bila Uonevu

The bump

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2019
Posts
1,488
Reaction score
2,908
Kuna Jambo nimekua nikiliwaza mara kwa mara akilini mwangu lakini naona kadri siku zinavyoenda linazidi kukomaa na kushika mizizi.

Tunaishi Tanzania ambayo ni nchi inayosifika kwa amani,lakini ukweli ni kwamba hii nchi amani inayoongelewa ni kukosa vita tu na wala si amani ya mtu mmoja hadi mwingne.

Tanzania ni nchi yenye uonevu mkubwa sana hasa ukiwa unahitaji fatilia vitu vyako vya maana,hasa unapotaka Haki katika jambo flani.

Nimewaza kuna Polisi kuna Mahakama kuna Viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya mtaa mpk taifa lakini mtu mmoja mwenye PESA akiamua kukuonea anakuonea na Huna cha kumfanya (hii ndio tanzania ninayoijua)

NINI KINAHITAJIKA?

Nimewaza muda mrefu inahitajika Taasisi yakusimamia haki za watanzania ambayo haitoangalia wadhifa wa mtu wala uwezo wa mtu bali kauli mbiu iwe ni "HAKI SAWA KWA WOTE tanzania yenye Amani"

Taasisi hiii inahitaji sio waongeaji tu ila itahitaji Watu wenye PESA na USHAWISHI na tutakaodhamiria kufanya jambo na likatimia.

Tutakua na Team ya wanasheria (wenye pesa na ushawishi) Hatutoingilia kazi ya polisi ila kazi yetu ni kufatilia jambo litakalofika polisi mpka lifike mwisho.

KESI nyingi sana zinapotezewa polisi na mahakamani kutokana na kuegemea upande mmoja, Hasa hizi kesi za NDOA na wana ndoa, watu wengi wakiskia ugomvi unaohisi mume na mke hata kama kweli kuna anae onewa Hujiweka pembeni na kuwaacha wahusika watunishiane misuli.

Si sawa wala si haki,KESI ya DOKTA MWAKA ni moja ya mambo yaliyonitia HASIRA SANA na kuwaza hili jambo kwa upana. Sipo upande wa mwanamke lakini kinachoendelea katika hili sakata ni DOKTA MWAKA kumtishia mke wake kwasababu ANA PESA.

Huwez kwenda kumuwekea mtu majeneza getini, tena majeneza hadi ya watoto waliotoka viunoni mwako,Hii maana yake ni nini? kwangu naona ni uonevu.

KESI imefikishwa mpaka polisi lakini unaona wazi kabisa namna MWAKA anavyotoa pesa kutokana na mwenendo unaoendelea.

HAPO JUU ni mfano HAI, Kwa hiyo nataka taasisi itakayoweza kusimamia haki ya mtu mmoja mmoja mpka mwisho na Hii taasisi itatoa HUDUMA BURE bila malipo, japo kama utapenda kutoa shukrani zako BASI ruksa lakini kesi zote zitakazoletwa OFISINI zitasimamiwa mpka haki ipatikane.

sifa za hii taasisi ninayoiongelea ni watu wanaotaka AMANI lakini pia sio amani mdomoni ila katika matendo kwasababu kila muajiriwa wa hii taasisi ana PESA na Ana ushawishi (ndio mana nikasema huduma zitatolewa FREE)

Hatutotegemea pesa ya mtu,kazi yetu itakua ni kusimamia HAKI na kesi zote zitakazo fikishwa Polisi tunazifatilia hadi hukumu itoke haki ipatikane.

Hatutokua upande wa yeyote yule ila HAKI ITASIMAMA, tutakusanya kesi zote zilizopo TANZANIA kuanzia kwenye mitandao ya kijamiiii (kama hii ishu ya mwaka) mpaka huko mitaaani, Yeyote ataekuja kutoa malalamiko ofisini Kazi yetu ni kumsimamia HAKI yake na yawezekana anataka kumuonea mwenzake hivyo tutamuelewesha na kumuonyesha haki yake ni ipi.

Tunahitaji chombo cha namna hiii katika nchi yetu,BINAFSI Nimeliona hili ni wazo linalohitaji utekelezaji hasa wa zile kesi za kiuonevu onevu wa wazi wazi, KESI itakayofika OFISINI kwetu basi hiyo itapatiwa ufumbuuzi tu,kama Hakimu anasema JALADA halionekani mwaka wa 8 huu KESI ikifika KWETU tukiingia hapo MAHAKAMANI jalada wataliona tu sio kwa namna tutasimamia hiyo kesi.

KAZI YETU NI kusimama nyuma ya mlalamikaji (tukiwa kama guardian angel) kuhakikisha anapata HAKI zake, hatutoingilia maamuzi ya mahakama wala Polisi wala vyombo vya sheria,ila tutakua nyuma ya muhusika kusimamia na kuhakikisha anapata haki yake.

Nadhani hili linawezekana.
 
Back
Top Bottom