Tanzania yote tukimpenda Yesu Kristo tutakua na amani ya moyoni ambayo huleta amani ya nje (utulivu yaani bila ghasia)

Tatizo imani ya kikristo imevamiwa na matapeli na wasaka ngawira kuliko dini nyingine yoyote.

Ni muhimu sana wanaotaka kufuata huu ushauri wako wawe makini sana kwa kuwa ni vigumu kuipata hiyo amani kutoka kwa matapeli wa kiroho.
 
Siyo kweli Yesu alituambia Mafarsayo na waalimu wa sheria wamekaa ktk kiti cha Musa wasikilizeni maneno yao lakini tusitende watendayo kwani wanatafuta mtu mmoja kumfanya mwongofu alafu wanamgeuza kuwa mbaya mara mbili yao.
Wewe mtazame Yesu Kristo usitazame watu.
 
Tatizo imani ya kikristo imevamiwa na matapeli na wasaka ngawira kuliko dini nyingine yoyote.

Ni muhimu sana wanaotaka kufuata huu ushauri wako wawe makini sana kwa kuwa ni vigumu kuipata hiyo amani kutoka kwa matapeli wa kiroho.
Dini haijavamiwa tatizo ni watu hawasomi neno la Mungu. Kama husomi neno la Mungu utadanganywa kwasababu huna elimu ya Mungu.
 
Umpende mtu ambae wakati anatandikwa bakora pale juu alikuwa anaita mungu wake amuokoe,cha ajabu makondoo wake wanamfanya yeye ndio mungu,
 
Yesu yupi? Au yule mzungu mlevi picha zake kuna watu wanazibandika kwenye magari
 
Dini haijavamiwa tatizo ni watu hawasomi neno la Mungu. Kama husomi neno la Mungu utadanganywa kwasababu huna elimu ya Mungu.
Unaposema haijavamiwa sikuelewi!

Angalia wahubifi feki walivyo wengi siku hizi(mfano, Kiboko wa wachawi) na asilimia kubwa wanaojiita manabii na mitume ni Matapeli.

Kusoma na kuelewa inategemea pia na kiwango cha elimu.
Bahati mbaya elimu ya wafuasi wengi iko chini....hali .hiyo haistahili kuwa fimbo ya kuwachapa kwa kuwatapeli kidogo walicho nacho..
Kumbuka Yesu Kristo alilisha watu 500 wenye njaa, ila siku hizi hao matapeli wamepindua na kufanya watu hao wenye njaa wanamlisha mtu mmoja aliyeshiba.
 
Kwanini watu waende kwa wahubiri feki? Wao ndio wenye shida. Wamekosa elimu ya Mungu. Mtu mwenye elimu ya Mungu hawezi kuangukia kwa wahubiri feki.
 
Una uhakika gani? Kwani kabla ya kuletewa ukristu wazee wetu waliombaje?Waislamu nao watasema ni Mohamedi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…