Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

tehe tehe with all respect jamaa alipokuwa anahojiwa na zamaradi alisema lulu ni kama mdogo wake kumbe jamaa alikua ana kula mzigo behind the scene...hata mm nakatamani haka kalulu....
Pole kameshasema, apaBongo akampendi mtu wala hana mipango na yeyote(may b ur money) kanampenda Justine B yule dogo wa USA so check out
 
Kama amekufa ktk uzinzi i dont hv R.I.P,nafasi ya kutubu ilishapta ashndwe mwnyw sis tutaweza wapi?MUNGU NDO AJUAYE,na awaheremu ndg,jamaa na marafikh.
 
kwel mapnz yn mambo,kam ndivo kwl kanastahl kfungo.

Nani akafunge, alikataka mwenyewe! Kwanza kanaweza kupimwa kajakazito, na unajua wanawake wakiwa wajawazito na mwaka mmoja baada ya kujifungua, kwa kitaalamu huwa wanahesabika wenda wazimu. RIP Kanumba
 
RIP Kanumba.
"Nazishuhudia na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako"
Kumbukumbu la Torati 30:19-20
 
Dah waswahili wanasema asiye funzwa na mamaye ulimwengu utamfunza,kama ni kwel anahusika na sheria ikafatwa kwel huu utakuwa mfano mzur wa wazazi wa aina ya mama lulu kujfunza,bado wema na wengineo wajfunze kutokana na hili
 
Yaani kutokana na chanzo cha kifo chake,basi tu
 
Pamoja na Michael Jackson
kuwa maarufu duniani hakupewa mazishi ya kitaifa hata rais Barack OBAMA hakuudhuria. Tunajua mzee wa mazishi hatakosa!!! C mnamjua?!
 
kama hakuwa freemaso naamin anaweza kusamehewa kwa msaada wa sala zetu.
 
Wakuu nadhani tunamfanyia huyu mtoto a dis-service, nina uhakika kwa sasa hakuna mtu mwenye hard time kama huyu mtoto (nina uhakika sio muuaji na kama kasababisha kifo hakukusudia...) kwangu mimi leo nasikitika kwa kifo cha Kanumba (RIP) na career ya huyu binti ambayo itakumbwa na misukosuko sasa for one so you....

Who knows kama sio haya matatizo mbeleni angekuaje (for one so young she has a long life ahead of her)

Tukumbuke tu, it takes two to tango.., na ugomvi ni wa wawili na hatujui ajali ilikuwaje.., instead of pointing the fingers lets just mourn in peace.
 
kama ndo hivyo bac. Neno state funeral litakosa maana. Si naskia kifo chake kinahusiana na mdada? Alioa au ndo zinaa? A break p'se!
 
Isingekuwa ni huu msiba wa Stephen Kanumba pengine nisingejua kiwango cha akili cha hawa wanaojiita ma 'star' wa Tanzania.

Leo asubuhi Clouds Tv walikuwa wanarusha live kipindi maalum cha mahojiano na watu waliokuwa wanamfahamu vizuri Kanumba.

Cha Ajabu Ray sijui ndiye Vincent Kigosi yeye kashikilia tu ubishoo tena wa kitoto uliogubikwa ushamba.

Wenzake wanaomboleza na kusikitika yeye kashupalia: " .... unajua niliponununua ile Lexus yangu, na Kanumba pia akanunua. Na baadae nikanunua Gari dogo naye akanunua, hivi sasa nina kiwanja Mbezi na utashangaa hata Kanumba alinunua pale jirani yangu kabisa ......................!"

Bongo Movie indeed
 
Tanzania hatuna ubunifu, Nchi za wenzetu sanaa inaingiza kipato kikubwa sana mfano America, carrebean Jamaica. Sisi tumeng'ang'ana na bia na magari. Soko la filam za kitanzania ni kubwa sana Afrika mashariki na kati. Mfano ziara za akina kanumba kongo DRC palikuwa hapatoshi full eskot. Lakini je ni jitihada gani zimefanywa na serikali katika ku exploit soko hili la film?. Tupotupo tu tumekalia politiki ndo maana uchumi unadorora, shilingi anaporomoka thamani na hakuna ubunifu tena. Wakati America uchumi wao unategemea uuzaji wa huduma ( service industry including sanaa ya music na film ss tunaashangaa tuu Tuamke jamani tuwe wabunifu)

Mkuu heshima mbele.

Mkuu unakosea unapoikosoa serikali katika jambo hili na unapofanya hivyo inabidi uje na facts.

Unataka kuniambia serikali ya US inamiliki Hollywood? au serikali ya India inamiliki Bollywood? au serikali ya Nigeria inamiliki Nollywood? jibu ni hapana.

Hizi ni sekta binafsi ambazo zilianzishwa wasanii wenyewe na zimekuwa na kufikia hapo zilipo. Serikali haiwezi kufanya chochote katika kuexploit hii industry isipokuwa katika kutoza kodi na kufanya regulations kulingana na sheria zilizopo.

Serikali imekwishajitahidi imejenga chuo cha taifa cha sanaa na pia imeunda baraza la sanaa la taifa, je hawa wasanii wa aina ya marehemu Kanumba, mzee King Majuto na magwiji wengine wa sanaa wameshiriki kikamilifu kuhakikisha Tanzania nayo inakuwa na eneo maalum la kutengeneza filamu ambalo ndio litakuwa chumbuko la filamu zote zinazotayarishwa Tanzania?

Halafu kuhusu kwamba labda marehemu azikwe na serikali hii ndio sielewi unamaanisha serikali kugharamia maziko yake au kumuenzi kwa kuweka siku moja ya maombolezi.

Mimi binafsi naona kwa kuwa hatujawahi kuwa na utaratibu wa aina hiyo, inabidi kwamba kwa kuwa yeye marehemu alikuwa ni mtu mashuhuri na aliejijenga kisanii kufikia hapo alipo basi maziko yake yanaweza tu kufanya private lakini yakawa na alama fulani kwamba marehemu aliishije akiwa msanii.


Hapa hakuna kuilaumu serikali kila mtu lazima atumie kichwa chake kupanga maana tayari tuna ubunifu mkubwa tu.

RIP Steven Kanumba
 
sasa uyu mtoto under 18 itakuwaje?

hapana ana miaka kumi na tisa huyo mtoto ambaye kwa namna moja au nyingine akionekana amehusika katika mauaji ya huyu mpendwa wetu,basi hii ni pure manslaughter ambayo ni murder case yenye kivuli cha mkono wa sheria.

RIP KANUMBA THE GREAT.
 
Naomba tukatendee haki haka katoto!. Mwenye mamlaka ya kutaja chanzo cha kifo ni daktari, na mwenye mamlaka ya kumtaja mhusika ni jeshi la polisi!.

Nashauri subirini taarifa ya dakitari kuhusu chanzo cha kifo. Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Lulu alimsukuma, inawezekana kwenye purukushani hiyo, ni Kanumba mwenyewe ali bugi step akateleza na kuanguka bila kusukumwa na yoyote!.

Hata kama ni kweli Lulu alimsukuma, chanzo cha kifo sio lazima kiwe kimetokana na kusukumwa!. Inawezekana Kanumba alikuwa na heart problem, pressure etc, hivyo alipokasirika pressure zikapanda, au akapata heart failure ndipo akaanguka!.

Hata kama ni kweli alijigonga, subirini madaktari wathibitishe chanzo cha kifo ndipo tuendelee kujadili!.

Najua msiba huu ni huzuni kubwa, lakini nawaombeni sana, lets not be judgemental kwa Lulu!.

Mimi ni miongoni mwa waumini wakubwa wa the doctrine of "karma", kuwa there is nothing new under the sun, hakuna coincidence wala bahati mbaya, lolote ambalo limetokea, lilikuwa litokee tuu, yaani siku ya mpendwa wetu Kanumba ndio ilikuwa imefika, saa ilipotimia Mungu akamuita, hata asingesukumwa, angefia usingizini!.

After all, there is life after life and life before life!, death ni change tuu ya life form from physical body to spiritual body!.

Rip Kanumba.

Pasco

Maneno ya hekima haya ili kuweka mjadala sawa. Wote hapa ni tulio katika parandesi. Hakuna mwenye haki ya kutoa hukumu kwa katoto haka. Kuanza mambo ya kikubwa kakiwa kadogo si sababu ya kuwa na uwezo wa kufanya mauaji pia. Tupishe uchunguzi ufanyike, yapo mengi yanayoweza kutokea hapa. Kwani kati ya anayemshuku mwenzake na mshukiwa yupi anakuwa na hasira kuliko mwingine. Inawezekana Kanumba aliteleza wakati akitaka kumfunza adabu Lulu. Hakuna anayejua Lulu ameeleza nini kwa undani mpaka sasa kwani yeye na K ndio waliokuwa chumbani peke yao. Kuhusu ukweli wa hii kitu tuwe na subira kidogo. Kwa sasa hatuwezi kusema Lulu ndiyo muuaji.
 
Back
Top Bottom