Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Poleni wafiwa. Leo ndo nimeona picha ya Lulu humu ndani, na watoto wananiuliza Kanumba ndiyo nani? Walipoona picha wakasema wamemuona kwenye matangazo. Am very far from bongo movies na hao celebrities wao sijui. Kwa kumsikia habari zake Kanumba alijitahidi katika tasnia ya filamu Tanzania.

Siseni alale pema peponi sasa, maana maisha ya mtu yanamfuata mara anapokufa kwahiyo yupo pale anapostahili kwa sasa hata tuombe mara ngapi.
Poleni wafiwa kwa majonzi, hasa wazazi na ndugu. Kifo chake kinaonyesha kuwa cha ghafla na utata huu wa chanzo unaongeza huzuni.
 
Usishangae Kanumba anaigiza filamu ya yesu, na kesho akafufuka. Yule ni mburudishaji maarufu vuteni subira mpaka j3 ndio tuamini

RIP mburudishaji
 
'mimi nilikua the greatest yeye ni the Great'RAY ON CLOUDS
 
Alikuwa great kwa wapenda maigizo na mashost wote. Nasikia party zote zimecanceliwa, kisa mashost wote wameenda sinza kwenye msiba.
RIP the Great!
hata wewe ni great kwako...ndio maana unauza nyago kwenye thread yake....kudadadeki
 
Bwana ametwaa na jina la Bwana libarikiwe.Tuliobaki hai tukumbuke mshahara wa dhambi ni mauti.
 
uzuri wa Tanzania bwana..hakuna mochwari za masuperstar, wala viongozi, wala matajiri..wote mochwari yetu ni ile ile..
tutadharauliana sana huku kitaa ila kule tunakutana na hakuna dharau!
REST IN PEACE KANUMBA..WE ARE COMING!!!
Kuna mochwari za ma VIP mkuu...moja ipo mikocheni.
 
Hivi ni source of his death au ni cause of his death unconfirmed? Kina Nyani Ngabu na Dada yangu Sweety Radhia tusaidieni hapo!
 
attachment.php

Kwa habari ambazo kiukweli sina uhakika nazo sana eti Bongo Movie Super Star Steven Kanumba amefariki Dunia usiku wa Ijumaa kuamkia J'mosi. Na mwili wake unapelekwa Muhimbili kuhifadhiwa.

More updates to follow...
  • JF has confirmed his death
  • Source of his death unconfirmed
  • Taarifa ambazo hazijathibitishwa ni kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.
    ‘Inasemekana’ Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.
  • Lulu ameshikiliwa Polisi Oysterbay, inadaiwa ana majeraha pia.
  • Mwili wa marehemu uko katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya Muhimbili.

Hivi ni source of his death au ni cause of his death unconfirmed? Kina Nyani Ngabu na Dada yangu Sweety Radhia tusaidieni hapo!
 
lakini bado taarifa rasmi za mazingira ya kifo chake bado zinachunguzwa,
 
Back
Top Bottom