Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

mkuu! Hakuna kuomba hapa, kifo chake kama inasemekana, 7bu ni mapenzi, while huyu lulu c mke wake. Mungu wa kweli hana muda wakusikiliza kelele. Infact, tasnia ya filamu ni 1 ya kitengo cha shetani.! Sorry huo ndo ukweli

Absolutely right!
 
BWANA alitoa, na BWANA ametwaa, jina la BWANA na libarikiwe (Ayubu1:21b).

Poleni wandugu.

R.I.P Kanumba.
 
Haya wanasema si lulu huyo inakuwaje hapo? rip kanumba siamini!
 
Tusimpangie Mungu cha kufanya the guy never involved God in any way,after death judgement hes tomenting and cursing in the abbys now.Tusikitike hilo
Hakuna katika maandiko matakatifu
yanasema mauaji ni mpango wa Mungu huo ni mpango wa shetani labda kama kuna vitabu vipya vimeandikwa karibuni
jamani tuaache kumsingizia Mungu apendi ugomvi na watu waauwane hiyo ni kazi ya iIBILISI SHETANI
 
"women who kill"
kama lulu atakutwa na hatia atakuwa kaingi kwenye hio group ya women who kill
rip kanumba
 
OMG, i cant blv that, though siyo shabiki wake wala bongo muvi, i must say that am totaly shocked..nini mazingira ya kifo chake
 
kifooo kifo, kifoo kifo, kifooo kifo kwanini hauna huruma? RIP REMMY ONGALA & STEVE KANUMBA
 
Inawezekana alijitabiria kifo ktk movie yake ya MOSES (NEVER SAY NEVER) kama amekufa namna hyo kama inavyo daiwa aina tofauti na kile kifo katika ile movie au sio jamani?
anyway rest in peace kanumba.
 
Poleni wafiwa na washabiki wake. Bwana ametwaa na jina la Bwana libarikiwe.Wote tu wasafiri na kifo sio mwisho wamaisha bali tunaamini ni mwanzo wa maisha mengine katika ulimwengu wa roho kama ni uzima wa milele au mauti ya milele.
 
HISTORIA YAKE:


Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.


Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.


Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.


Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.


Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.


Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.


Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na kadhalika.


Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.


Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.


Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.


Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo ni ‘makka' ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin.

Source:
BIN ZUBEIRY: KANUMBA AFARIKI DUNIA, LULU AHUSISHWA NA KIFO CHAKE
 
tujifunze kutafakari angalau hata kidogo. Liyumba ni marehemu na chumbani walikuwa wawili sasa hii simulizi kaitoa Lulu? Give me a break..........ukweli ni kuwa:-
"Do not deceive yourself. God is not mocked. Whatever a man sow that he shall also reap........................." Galatians 6:7

Kwa taarifa nilizonazo hususani baada ya ile movie aliyoicheza Nigeria na TZ kwa pamoja uvumi ulikwisha kuzagaa kuwa afya yake ilikuwa na mushkeli mkubwa.....................cocktail ya kibongo ilimpa siha marejeo ambayo sanasana ilisaidia kuharibu viungo ndani ya mwili wake.......................figo, maini, moyo n.k.....................suala la kuanguka is typical kwa wengi wenye khali yake....................kule malawi Bingu naye alidondoka......sijui Lulu alikuwepo kule kumvisha kaputula?

Mkuu, unamuongelea Kanumba au Liyumba?

Ni ngumu kuamini na kuelewa kama Kanumba amekufa. Naona kama sinema hivi!. Siamini

R.I.P Kanumba.
 
Magazeti ya Udaku utashangaa wanaanza oooh.. "free masons"..
 
Back
Top Bottom