Kuhusu animation ya
Good Guy,
PICHA/MICHORO
Kuna tofauti kubwa (chanya) ukilinganisha na kazi zilizopita (mwaka jana?) za
stick figures.. hizi ni bora sana. Maendeleo makubwa.
UHUISHAJI/ANIMATION
Cha kwanza nilichopenda ni kuwepo kwa kopo la juisi lilikanyagwa.. hii inasaidia kutajirisha mandhari na kujenga udadisi kwa kuanza filamu kutokea pembe/upande (angle) usiotarajiwa.. ni rahisi sana kusahau kuweka vitu kama hivi..
details.. safi.
Nimependa pia details za watu katika magari eg nywele za jamaa kwenye gari nyekundu kutikisika na
facial expressions za mdada (Eye blinking and mouth movements), car speeds and camera moves and angles eg from above etc.
SAUTI/SOUND
Sauti ni nzuri pia. Sina malalamiko.
MAPUNGUFU
Huyo trafiki aisee hajakulia mkoa wa Mara, sauti yake inaonekana anatokea maeneo ya baridi lakini si kusini mwa Tanzania. Ubunge wa Tarime atausikia tu redioni.
TECH STUFF
Inaonekana katika options za kurender katika hatua fulani uliset video kuwa
Interlaced, kwa sababu inaonesha vimistari horizontal (interlace combing effect) angalia mfano wa picha chini. Watu wanaotumia screen za migongo/visogo (CRT) hawatagundua hilo ila wa Flat screen itakuwa dhahiri kwao. Kwa kuwa teknolojia inaelekea kwenye flat screens na broadcast equipment zimekuwa faster na more powerful badala ya kurender "interlace" scan tumia "Progressive." Naamini hizo options zitakuwepo kwenye software yako.
Kielelezo, Interlace Combing effect:
ALAMA
76%
Adios.