Tanzanian traditional local foods

Tanzanian traditional local foods

Nswalu ndiyo jina lake.Ni mlenda uliokaushwa na kusagwa.
JamiiForums1673568575.jpg
 
Kwa wale wasiyofahamu,hivyo ni viazi vitamu vinavyo hifadhiwa kwa njia mbili.Picha ya kwanza ni viazi vibichi vilivyu katwa katika hali ya vipande bapa na kukaushwa kwa jua(MICHEMBE AU MAKEWE).Picha namba tatu, maandalizi yanafana kiatua naya picha namba 1,ila tofauti ni hapa viazi vinachemshwa kwanza kisha ndiyo vikatwa na kuanikwa(MATOWOLWA AU MATOVOLWA).

Asante sana mkuu huwezi amini hata mie ufahamu huo sikuwa nao juu ya tofauti za uandaaji wa viazi hivi pendwa na majina yake, mie nilikuwa najua kuwa vyote huitwa michembe,

Pili kama unafahamu historia ya makabila au asili ya ukataji au uchongaji huu wa viazi vitamu ulipoanzia na kwanini wavumbuzi walivutiwa kufanya hivyo, unaweza share nasi hapa tujifunze.
 
Vyakula vya mijini zaidi na kiafya havipo vizuri kwa sababu ya mafuta mengi.
Nakubaliana nawe kwa asilimia 100 ni kweli chanzo cha magonjwa mengi yasiyo ya kuambukiza ikiwemo magonjwa yanayosababishwa na uzito uliopitiliza, BP, kisukari, kansa, n.k nimatokeo ya ulaji wa vyakula vya mafuta, sukari nyingi za viwandani, chumvi nyingi, kemikali na mitindo mibovu ya maisha, tunatakiwa kuishi sehemu fulani ya maisha yetu kiasili na kuenzi vyakula vya kijadi hili kurejesha nuru ya afya zetu ambayo imepotezwa na ukisasa.
 
Muhogo huo kijana.
Umekuwa mtu wa kwanza kwenye uzi huu kuutambua ugali huu, tafadhali tuelezee kama unafahamu maandalizi yake mpaka kupelekea muhogo huo kuwa na rangi hiyo, pia unaweza kututanabaisha ugali huu ni maarufu kwa wenyeji wa mkoa gani.
 
Asante sana mkuu huwezi amini hata mie ufahamu huo sikuwa nao juu ya tofauti za uandaaji wa viazi hivi pendwa na majina yake, mie nilikuwa najua kuwa vyote huitwa michembe,

Pili kama unafahamu historia ya makabila au asili ya ukataji au uchongaji huu wa viazi vitamu ulipoanzia na kwanini wavumbuzi walivutiwa kufanya hivyo, unaweza share nasi hapa tujifunze.
MATOWOLWA asili ya utengenezaji wake ni mkoa wa Tabora hasa wilaya ya Sikonge.Ni njia iliyotumiwa tangu zamani na wahenga wa mkoa huo ikiwa ni njia ya kuhifadhi chakula kwa muda mrefu.Matowolwa uweza kuhifadhika kwa miaka hata zaidi ya mitatu bila ya kuharibika wala kubunguliwa.Na ndiyo njia bora zaidi inayokuwezesha kuhifadhi zao la viazi vitamu kwa muda mrefu zaidi.
MICHEMBE/MAKEWE ni njia nyingine inayotumiwa na makabila ya mikoa ya Tabora,Shinyanga na Mwanza ya kuhifadhi viazi vitamu kwa muda mrefu japo hivi vikikaa sana uweza kubunguliwa na wadudu.Nadhani asili ya utengenezaji wa aini hii ni mkoa wa Shinyanga.
N.B
Mkoa wa Tabora unaweza kuwa ndiyo mkoa unaoongoza kwa njia za kuhifadhi mazao ya chakula na mbogamboga kwa muda mrefu zaidi kwa njia za asili.
Unyamwezini utapata mboga za majani zilizo kaushwa kama Nsansa (majani ya kunde yaliyo chemshwa na kisha kuanikwa),Nswalu (Mlenda wa asili uliokaushwa na kusagwa),Ntwili (Karanga zilizokaangwa na kusagwa),Uyoga ulikaushwa kwa jua,Ntole (nyanya chungu za asili)pia ukaushwa kwa jua na kuhifadhiwa.
Nyama uweza kuhifadhiwa kwa kubanikwa au kupakwa chumvi na kuanikwa juani au kuhifadhi nyama mbichi kwa kulowekwa kwenye asali kwa muda wa hadi mwaka.
 
Nakubaliana nawe kwa asilimia 100 ni kweli chanzo cha magonjwa mengi yasiyo ya kuambukiza ikiwemo magonjwa yanayosababishwa na uzito uliopitiliza, BP, kisukari, kansa, n.k nimatokeo ya ulaji wa vyakula vya mafuta, sukari nyingi za viwandani, chumvi nyingi, kemikali na mitindo mibovu ya maisha, tunatakiwa kuishi sehemu fulani ya maisha yetu kiasili na kuenzi vyakula vya kijadi hili kurejesha nuru ya afya zetu ambayo imepotezwa na ukisasa.
Haswa!Upo sahihi mkuu.
 
Back
Top Bottom