Napenda sana vyakula asili basi tu nilipo kuvipata ni kipengele, majiji makubwa hayana hizo vitu vya asili kwa wingi km huko vijijini, nikienda home msosi unakuwa hivi, na huwa natangaza kabisa sigusi ngano
asubuhi viazi vitamu/mihogo/magimbi/maboga ya kuchemsha kwa chai yenye mchai chai na mdalasini au tangawizi, ama maziwa mgando,
mchana ni ugali nyama choma, dagaa nk ama ndizi zile zipikwe kienyeji, na mboga za majani zilizochemshwa tu na chumvi matunda ama juice,
Usiku wali/ndizi/makande maharage, samaki mchemsho tu, nk na huwa najisikia kurudisha uhai,
Hata maji ya home yapo tofauti na haya ya huku, kwakweli ni mateso