Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,422
- 5,659
- Thread starter
-
- #101
Halafu mwisho wa siku wanakazana kushindilia vikombe vya alikasusu na vumbi la kongo kumbe tiba ni kula vyakula vya kiumeni, maana mkufu ukishalala hausimami hata ulishwe pweza.[emoji23]Kwa hizi magimbi, maboga, mamung'unya, mahindi ya kuchemsha kuna mavijana yanweza yakadhani meza imejaa vifaa vya ujenzi...[emoji13]
KabisaHuu msosi mashuzi yake ni kama mabomu ya Taliban....[emoji13] lakini ni msosi wenye afya sana, mavijana yangekula hizi food bilashaka mkongo dast usinge pata soko huku Tanganyika [emoji5]
Inaonekana huko makini sana mkuu na lengo la uzi, ni kweli kuna baadhi ya vyakula vichache nimetia udambwi udambwi lakini siyo vya asili ya jamii yetu ila ni kwa kuwa vinapendwa sana na vina walaji wengi ndiyo maana nikavitia pia humu.Mkuu..... huku Ibologelo, hii sambusa na mchuzi mix sijawahi kuiona walahi...[emoji2955]
Kama una picha za hivi vyakula ulivyovyitaja tafadhali tupiaVipi kuhusu Mbute, Makopa, Mchembe na Matobolwa...??
Asante kwa kutambua mchango wa vitumbua katika maisha yako.Vimenikuza na kunilea hivi.
Mnatutamanisha bila kuleta picha.Dah, Matobolwa ni Matamu sana.
Hahah..hii ndo asilia yenyewe...umenikumbusha nyumbanKishumba 🤣View attachment 2635531
Ndizi + maharage + magadi kidogo kwa ajil ya kuchachuaChakula hiki kinapikwa kwa kutumia nini na ni chakula cha tamaduni ipi hapa Tanzania?
Mtory uwekwe kwenye "kakidewa" alafu upate na "viazi vikuu" vya pale Kyeer Machame. Weeeeee, mambo sio mchezo.Mpk sasa sijaona mtori...
Wacha uzushi na Uongo.Ugali unadumaza akili na unasababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kiriba tumbo etc
Inaonekana huko makini sana mkuu na lengo la uzi, ni kweli kuna baadhi ya vyakula vichache nimetia udambwi udambwi lakini siyo vya asili ya jamii yetu ila ni kwa kuwa vinapendwa sana na vina walaji wengi ndiyo maana nikavitia pia humu.
Nikiona chapati napagawa😋
Chapati tamu mno ukijumlisha na ile aroma yake unaweza tafuna vidole[emoji23]Nikiona chapati napagawa[emoji39]
Napenda sana vyakula asili basi tu nilipo kuvipata ni kipengele, majiji makubwa hayana hizo vitu vya asili kwa wingi km huko vijijini, nikienda home msosi unakuwa hivi, na huwa natangaza kabisa sigusi ngano
asubuhi viazi vitamu/mihogo/magimbi/maboga ya kuchemsha kwa chai yenye mchai chai na mdalasini au tangawizi, ama maziwa mgando,
mchana ni ugali nyama choma, dagaa nk ama ndizi zile zipikwe kienyeji, na mboga za majani zilizochemshwa tu na chumvi matunda ama juice,
Usiku wali/ndizi/makande maharage, samaki mchemsho tu, nk na huwa najisikia kurudisha uhai,
Hata maji ya home yapo tofauti na haya ya huku, kwakweli ni mateso