Waganda na wahaya wanaongoza kula kwa mpangilio wa kiasilia na tija
Kwa Tz wakurya wanaongoza kula vitu vya ajabu ugari mweusi na mavi ya ng'ombe(kichuri)
Unaonekana wewe ni muhaya hivyo unachojua ni utamu wa chakula apikacho mama yako pekee, ukweli ni kuwa kila jamii ina ubora wake katika tamaduni na vyakula vya asili.
Nimeiangalia video yako sijaona cha tofauti sana, Wahaya au Waganda ni jamii zinazopendelea kula ndizi, senene na samaki kulingana na mazingira yao,
wakati Wakurya ni jamii za wafugaji hivyo uwezi kuwafundisha chochote kuhusiana na nyama bora ungekuwa mmasaai ningesema sawa una haki ya kukosoa.
Kichuri si kinyesi cha mnyama bali ni ile juisi ya chakula kilichomeng'enywa katika tumbo la mnyama (ndani ya utumbo mdogo) kabla ya kusharabiwa mwilini, siku nyingine ukiwa hujui jambo uwe unauliza kwanza kabla ya kuhukumu.
Hakuna mafundi wa kuchoma nyama nchi hii kama wakurya ukitaka kujua hilo tembelea Tarime, kuhusu ugali pia kanda ya ziwa ndiyo kinara wa ugali wenye ladha nzuri wa muhogo na mtama au mahindi ukiiondoa Kagera ambao wao ni wabobezi wa pishi la matoke.
Kifupi kila kanda inavyakula vyao vya asili na ufundi wa mapishi ambao ni exceptional, leo hii uwezi kuwapindua watu wa pwani upande wa viungo katika mapishi, mapishi ya pilau, biriani, wali wa nazi, vitafunwa vya kila namna n.k
Kanda ya kusini pia ina vyakula vyake vya asili vingi tu, bila kusahau kaskazini kule wachanga na wapare wanautajiri mkubwa wa vyakula vya asili, usiwasahau kanda ya kati na kule Kigoma kwenye migebuka, hivyo kila jamii inatamba pande zake na hakuna jamii iliyobora kuliko nyingine.