Tanzanian traditional local foods

Tanzanian traditional local foods

[emoji106]
FB_IMG_17013727851513180.jpg
FB_IMG_17013727049274027.jpg
FB_IMG_17013720175618121.jpg
FB_IMG_17013503919407491.jpg
FB_IMG_17013503813173781.jpg
FB_IMG_17013503473043078.jpg
FB_IMG_17013503450426129.jpg
 
Waganda na wahaya wanaongoza kula kwa mpangilio wa kiasilia na tija
Kwa Tz wakurya wanaongoza kula vitu vya ajabu ugari mweusi na mavi ya ng'ombe(kichuri)

Unaonekana wewe ni muhaya hivyo unachojua ni utamu wa chakula apikacho mama yako pekee, ukweli ni kuwa kila jamii ina ubora wake katika tamaduni na vyakula vya asili.

Nimeiangalia video yako sijaona cha tofauti sana, Wahaya au Waganda ni jamii zinazopendelea kula ndizi, senene na samaki kulingana na mazingira yao,

wakati Wakurya ni jamii za wafugaji hivyo uwezi kuwafundisha chochote kuhusiana na nyama bora ungekuwa mmasaai ningesema sawa una haki ya kukosoa.

Kichuri si kinyesi cha mnyama bali ni ile juisi ya chakula kilichomeng'enywa katika tumbo la mnyama (ndani ya utumbo mdogo) kabla ya kusharabiwa mwilini, siku nyingine ukiwa hujui jambo uwe unauliza kwanza kabla ya kuhukumu.

Hakuna mafundi wa kuchoma nyama nchi hii kama wakurya ukitaka kujua hilo tembelea Tarime, kuhusu ugali pia kanda ya ziwa ndiyo kinara wa ugali wenye ladha nzuri wa muhogo na mtama au mahindi ukiiondoa Kagera ambao wao ni wabobezi wa pishi la matoke.

Kifupi kila kanda inavyakula vyao vya asili na ufundi wa mapishi ambao ni exceptional, leo hii uwezi kuwapindua watu wa pwani upande wa viungo katika mapishi, mapishi ya pilau, biriani, wali wa nazi, vitafunwa vya kila namna n.k

Kanda ya kusini pia ina vyakula vyake vya asili vingi tu, bila kusahau kaskazini kule wachanga na wapare wanautajiri mkubwa wa vyakula vya asili, usiwasahau kanda ya kati na kule Kigoma kwenye migebuka, hivyo kila jamii inatamba pande zake na hakuna jamii iliyobora kuliko nyingine.
 
Supu ya bone marrow-ina utajiri wa kolajeni ambayo uimarisha mifupa na kuipa afya ngozi, ina kampaundi ya glucosamine ambayo ni tiba ya matatizo ya miguu, maumivu kwenye maungio ya mwili na mzio, hivyo basi ni kosa kubwa hasa kwa mwanaume wa kitanzania kukosa supu ya mbupu,uboho na kidari kisha ukaja kulalamika mambo kulee hayaendi na kiuno kinakuuma[emoji23]
FB_IMG_17016930699749802.jpg
FB_IMG_17016930728520529.jpg
FB_IMG_17016930757150389.jpg
FB_IMG_17016930805259121.jpg
FB_IMG_17016930836653843.jpg
 
Back
Top Bottom